Ridhiwani Kikwete afichuka kukandia Millya

Ridhiwani anafikiria nadharia ya uridhishwanaji wa utawala wa kupokezana vijiti, asahau Tanzania ye leo, watu wameamka, bora afikirie tu kuendesha biashara za malori aliyoanza na vituo vya mafuta.

Yaah unasema kweli, lakini katika hali ya sasa, anajaribu kuplay na vyote, mwaka 2015, aatchagua kimoja.
 
Kama kweli wizi ungekuwa kosa huko CCM leo hii tusingukuwa kwenye hii sintofahamu ya mawaziri kutojiuzulu. Na hizo taratibu anazosema Ridhiwani kwa nini asimshauri baba yake kuhusu mabilioni yaliyooneshwa kwenye report ya CAG? Tshs 2 milioni ni kitu gani mbele ya mabilioni yanayoliwa na wateule rais?
 
Yeye Ridhiwani hadaiwi na taasisi na watu binafsi kibao?
alishalipa mkopo wa bodi ya......
 
Sikujua kama vçcm wamefilisika kihivyo 2m ni hela ya kuita vyombo vya habari na kutangaza duu kazi ipo.
 
Ridhwani kama unanisoma hapa JF. Tatizo sio Millya wala vijana wengi wanaowakimbia bali tatizo lipo nyumbani kwenu CCM.. Kambi ya Lowassa imekuwa na nguvu kubwa kiasi kwamba watu wengine hawataki kuwa mamluki..Utawala wetnu umezungukwa na makundi unafiki nakadhalika hivyo asiyependa kuwa ktk kambi hizi za mashindano anajitoa taratibu..
 
kwanza hatutakiwi kujadili huyu mdudu mwenye magamba mwili mzima! hizo milioni 2 ni nyingi kuzidi pesa wanazo iba kila siku yeye anatumiwa kama chachu yas wizi!
 
Ni busara ya kawaida tu dogo angetulia na kuendelea na mambo yake, huo mdomo na wino vitamgharimu huko mbele, siasa mchezo mchafu.
 
RidhiwanKikweteJr.jpg

Ridhiwani Kikwete


Ridhiwani amshukia Millya

Mtoto wa Rais, Dk. Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete amemshukia aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Arusha, James Ole Millya.Millya alijiengua kutoka CCM na kujiunga CCM kutokana na kile alichoeleza kuwa chama tawala kimekuwa mfano wa gari lililosheni pancha, hivyo halifai kwa safari.

Hata hivyo, baada ya Millya kuondoka CCM, taarifa zilizopatikana mkoani humo zilieleza kwamba aliondoka akiwa na takribani Shilingi milioni 2, mali ya UVCCM. Taarifa hizo ndizo zimemuibua Ridhiwani akichangia katika mtandao wa kijamii wa Tunuru la Afrika na kusema Millya asubiri utaratibu unafuata. Ridhiwani aliandika maneno hayo juzi kupitia simu yake ya mkononi na kuyatuma kwenye mtandao huo akisema, “nilidhani utani, kumbe James (Millya) tunamdai hela za Umoja wa Vijana mkoa wa Arusha.”
Aliongeza, “nawashukuru vijana makini wa mkoa wa Arusha kwa umakini wa hali ya juu. Utaratibu waja bwana Millya kama unasoma post hii.

Hata hivyo ujumbe huo wa Ridhiwani ulichangiwa na washiriki mbalimbali, wengi wao wakimpinga na kumhusisha (Ridhiwani) na familia yake kwa tuhuma zenye nia ovu. Baadhi ya tuhuma hizo zimewahi kuchapishwa na kutangazwa kwenye vyombo vya habari, zikikariri vyanzo tofauti.


Millya alitangaza kujiudhuru uwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha hivi karibuni na kuhamia rasmi katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). Aidha, siku iliyofuata viongozi wa CCM kwa nyakati tofauti walikaririwa na vyombo vya habari wakimwelezea Millya kuwa, alikuwa gamba na mzigo ndani ya chama umoja huo.

IPPMedia

wana JF
Kwa wale wasiojua vyema jinsi UVCCM inavyo ongozwa naomba someni hapa chini ili msikurupuke ktk kutoa maoni juu ya hili


Ibara ya 82 Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Wa Mkoa

1.ataongoza mkutano wa vijana wa ccm wa mkoa,baraza la vijana wa ccm la mkoa na kamati ya utekelezaji ya baraza la mkoa
2.ktk mikuitano anayoongoza zaidi ya kuwa na kura yake ya kawaida,mwenyekiti wa vijana wa mkoa atakuwa na kura ya uamuzi iwapo kura za wajumbe wanaoafiki na wasioafiki zitalingana
3.mwenyekiti wa vijana wa ccm wa mkoa atachaguliwa na mkutano mkuu wa mkoa.atashika nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitano ya uongozi lakini anaweza kuchaguliwa tena baada ya muda huo kumalizika,endapo anazo sifa za uongozi

4.atakuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya ccm mkoa
5.atakuwa ndie msimamizi mkuu wa siasa za viajana ktk mkoa


zipo nyingi sana kazi za MWENYEKITI WA UVCCM MKOA

lakini hakuna sehemu anapotajwa kuwa atahusika ktk kushika pesa za uvccm hata kuzisimamia


Ibara ya 83 inamtaja katibu wa vijana wa ccm mkoa kuwa (d) atatunza fedha na kumbukumbu za umoja wa vijana wa ccm ktk mkoa wake


hivyo basi SYSTEM YA UVCCM INAMTAKA KATIBU WA UVCCM AWE NDIYE MTUNZA PESA ZA UMOJA NA SI MWENYEKITI

na mala nyingi mwenyekiti si mtendaji kazi zote hufanywa na katibu na pia ndiye MHASIBU

Sasa bado sipati picha iweje leo hii Arusha watake kusomewa mapato na matumizi na mwenyekiti na si katibu? je katibu nae kajitoa uvccm?
 
Ridhiwan unajitaftia matatizo,babako jambaz,mamako jambazi kupitia wama,wewe jambaz umepora ardhi ya watu wa arsh,ole wako tukukamate tutakutaili kwa mara ya pili
 
Mwizi huyoooo!!!!!!!!!
Ridhiwani subiri ujambazi wako ulioufanya hapa Arusha kwa kuwanyang'anya wananchi wa Arusha ardhi yao.
Siku itakapofika labda uhame hii nchi. kwa sasa tunaanza na baba yako anayewatetea wezi wa mali ya umma.
Badala ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Pinda kibao kinamgeukia Baba yako!

Mimi namshangaa huyu Riz 1 ni mshenzi wa tabia, kwani Millya anashida gani na 2m? Yeye mwizi mkubwa anaekula hela za watanzania hapa Arusha nani hamjui???? akachukue hela alizoweka kwa Gody Mwalusamba then ndio aje na ushenzi wa 2m. Kwanza thubutu yako ukanyage Arusha ndio utajua maana ya PEOPLES POWER..... Nakuchukia sana wewe kijana mdogo na ole wako tuchukue nchi wewe na baba yako lupango inawahusu sana sana wewe, kijana mdogo unapata wapi billions of money??? na ukumbuke Rais ni baba yako na sio wewe. Eti uvccm Taifa... my foot.
 
wana JF
Kwa wale wasiojua vyema jinsi UVCCM inavyo ongozwa naomba someni hapa chini ili msikurupuke ktk kutoa maoni juu ya hili


Ibara ya 82 Mwenyekiti wa Vijana wa CCM Wa Mkoa

1.ataongoza mkutano wa vijana wa ccm wa mkoa,baraza la vijana wa ccm la mkoa na kamati ya utekelezaji ya baraza la mkoa
2.ktk mikuitano anayoongoza zaidi ya kuwa na kura yake ya kawaida,mwenyekiti wa vijana wa mkoa atakuwa na kura ya uamuzi iwapo kura za wajumbe wanaoafiki na wasioafiki zitalingana
3.mwenyekiti wa vijana wa ccm wa mkoa atachaguliwa na mkutano mkuu wa mkoa.atashika nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitano ya uongozi lakini anaweza kuchaguliwa tena baada ya muda huo kumalizika,endapo anazo sifa za uongozi

4.atakuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya ccm mkoa
5.atakuwa ndie msimamizi mkuu wa siasa za viajana ktk mkoa


zipo nyingi sana kazi za MWENYEKITI WA UVCCM MKOA

lakini hakuna sehemu anapotajwa kuwa atahusika ktk kushika pesa za uvccm hata kuzisimamia


Ibara ya 83 inamtaja katibu wa vijana wa ccm mkoa kuwa (d) atatunza fedha na kumbukumbu za umoja wa vijana wa ccm ktk mkoa wake


hivyo basi SYSTEM YA UVCCM INAMTAKA KATIBU WA UVCCM AWE NDIYE MTUNZA PESA ZA UMOJA NA SI MWENYEKITI

na mala nyingi mwenyekiti si mtendaji kazi zote hufanywa na katibu na pia ndiye MHASIBU

Sasa bado sipati picha iweje leo hii Arusha watake kusomewa mapato na matumizi na mwenyekiti na si katibu? je katibu nae kajitoa uvccm?

Asante kutupa ufafanuzi, swali hili nimeliuliza hapo nyuma kwani kwa ufahamu wangu kawaida mwenyekiti hahusiki na masuala ya utunzaji wa fedha ingawa anaweza kuhusika katika uidhinishaji wa matumizi ya fedha. Hapo CCM wanacheza mchezo kipofu na hawajui goli litafungwa kwao.
 
Huyu dogo Hana fikira pevu kabisa, mi ningeomba atume sms kumuuliza Muttasin Ghadafi na watoto wengine wa Ghadafi waliouawa na walio Hai atapata majibu kwa nini wameuawa na wengine kwa nini wanataabika atapata jibu
 
nasikia ole millya hana kazi wala sehemu ya kuishi inadaiwa anashinda katika club moja inaitwa via via nina clip ya viongozi wa ccm ebu nisaidieni jinsi ya kuiingiza humu maana nifanyeje ili kila mmoja aisikilize mwenyewe

wasiliana na mod
 
We are serious! wewe na babako tambueni ars si salama tena kwenu! na iwepo machafuko yakitoke vitega uchumi vyenu vyote tunavifahamu hapa a town tutaviteketeza wezi nyie.

Inashangaza kusikia miliya ameondoka na hizo fedha za mchango wa uvccm wa mwaka 208 lakujiuliza walikua wapi kudai au kumchukulia hatua miaka yotehiyo?hayo nimaneno ya mfamaji
 
Dogo anatakiwa afunguke kuhusu wizi wakina ngereja lakini yeye anakuja na masuala ya milioni 2? akasome ripoti ya mkaguzi mkuu ajuwe ni sh ngapi serikali ya baba yake wamekula.
 
Watanzania acheni Majungu Jamani!! Kuwa mtoto wa Kiongozi haina maana kwamba anapoteza haki yake ya uraia wa Tanzania! Kisha nimeona hapa watu wanachangia ki ushabiki na hakuna hata ukweli wa kumtia katika ubaya unaozungumzwa hapa!! Kwa nini nasema hivyo??
Mosi., chanzo cha taarifa. Mtoa hoja amesema taarifa ameitoa facebook kwenye tanuru la Afrika! Ninavyojua mimi facebook ni mtandao wa kijamii, na mtu yeyote anaweza kutoa mchango wake vile anavyojiona inafaa...... Sasa sioni ubaya juu ya Riz1 kutoa maoni yake huko!

Pili. Facebook si moja kati ya Media of communication ya ccm, kwa hiyo, taarifa kutoka kwenye mtandao huo si reliable kuifanya iwe official kama ndio taarifa ya Uvccm.

Tatu, Riz1 ndiye Mtunza hazina wa mali zote za umoja wa vijana Taifa, na alichaguliwa na Baraza kuu Uvccm taifa, Na Millya akiwa mmoja wao, kwa hiyo ni halali kwake kuhoji juu ya kuwepo kwa upotevu wa fedha za Jumuiya!

Pia, Riz1 tofauti na wachangiaji wanavyoropoka hapa jukwaani, ni kiongozi katika jumuiya na chama. Kwa mfano, yeye ni mjumbe Baraza kuu UVCCm Mkoa wa Pwani, na Taifa, mdhamin wa mali za uvccm taifa, mjumbe halmashauri kuu ccm wilaya Bagamoyo! Na hizo nafasi zote ni za kuchaguliwa na si upendeleo!!
 
Back
Top Bottom