Ridhiwani JK, ona na hawa!!

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
HII NDIO TOFAUTI YETU:



RIDHIWANI, sijajua vigezo vilivyotumiwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (The Tanzania Education Authority) kuwapata wahamasishaji wa kuchangia mfuko wa kununulia vifaa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum (students with disabilities) na hata pia mazingira ya kuandalia matangazo haya ambayo yanaonyesha hali halisi ya utofauti wa maisha katika familia za watanzania (ukiwa katika ofisi ambayo ina kila dalili ya neema na vitendea kazi).

Labda pengine katika hali njema kama hapo ulipo, ebu jaribu pia kutupa jicho lako binafsi huko chini ili kuona tofauti ya matabaka tunayojaribu kuyatengeneza katika nchi hii ambayo ina zaidi ya miaka arobaini ya kujitawala, ebu waone pia hawa ambao ni watanzania kwa kuzaliwa na wamekuwa wakiitumaini Serikali hii hii ambayo inawawezesha wengine kuwa na hali bora hata ya kuweza kuonekana katika mazingira ya gharama: ZUNGUMZA NASI KWA MZINGIRA HALISI YA KITANZANIA ILI IMAANISHE KWELI TUPO PAMOJA NA "KWA PAMOJA IWEZEKANE KWA KILA MMOJA WETU KUFURAHIA MATUNDA YA UHURU WETU KWA MAANA YA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA!!":

wanafunzi+hawana+madawati-kinole.JPG

Wanafunzi wa shule ya Msingi Kinole, katika halmashauri ya wilaya ya Morogoro, wakiwa wamekaa chini kutokana na uhaba mkubwa wa madawati unaoikabili shule hiyo

Juakali-Chunya.jpg


Mwalimu, Albert Juakali wa shule ya msingi Iboma iliyopo kijiji cha Udinde Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya akifundisha wanafunzi wa darasa la kwanza chini ya Mti wa Mbuyu

safe_image.php

3583548_orig.jpg


4360527_orig.jpg

safe_image.php

Shule ya Msingi Juhudi - Kigoma Vijijini, Tanzania
 
Last edited by a moderator:
Kwa kweli usemi wa maisha bora kwa kila mtanzania is a fantasy not a reality!!!!!
 
wadau, kwa kweli hiyo avator ya mkereketwa imenichekesha kupita kiasi. stress zangu kidogo zimepungua kwa kucheka. ama kweli laugher is the best medicine on earth!
 
Sasa, Mamlaka ya Elimu ya Juu (or whatever its called) ina maana gani kumtumia R J Kikwete kwenye hili tangazo? Hata kama wana nia njema, WHO IS RIDHIWANI KIKWETE???

Sasa yale mambo ya maana ya kutumia wasanii wenye influence katika jamii ndio wanaweka watoto wa viongozi.

Nonsense!
 
Sasa, Mamlaka ya Elimu ya Juu (or whatever its called) ina maana gani kumtumia R J Kikwete kwenye hili tangazo? Hata kama wana nia njema, WHO IS RIDHIWANI KIKWETE???

Sasa yale mambo ya maana ya kutumia wasanii wenye influence katika jamii ndio wanaweka watoto wa viongozi.

Nonsense!

Ni mtoto wa mfalme, ni kijana ambaye ana influence kuliko vijana wote, msomi kuliko vijana wote, ana kazi nzuri na anayefuata nyayo za Baba

Ikumbukwe ma architectures wa haya mambo wanajikomba kwa mzee na kwakuwa Nchi ishakuwa ya kifalme dogo lazima aingie kwenye siasa ili one day aje kukalia kiti cha mzee by the way wametoka kwenye familia ya kichief - Tz kila kitu kinawezekana ili mradi tu uwe connected
 
I like your sarcasm P Son.

Halafu ndio nini kuongea na yale mawireless headsets na madudu mengine? Ndio usomi? Au ndio uchapakazi au? Lakini labda waliokuwa wanashoot hilo tangazo hawakumshauri mwenzao vizuri, wangeshoot walau kwenye mazingira ya shule moja wapo aliyochangia na mmoja wa hao watoto.

Still, I am not impressed. I am pissed!
 
Hebu wandugu mjiulize yale mapesa walikuwa wakichangushana ili kukomba jimbo la moshi si wangesaidia watoto hawa?
Au nakosea wandugu? Hebu tukubaliane basi
 
Hebu wandugu mjiulize yale mapesa walikuwa wakichangushana ili kukomba jimbo la moshi si wangesaidia watoto hawa?
Au nakosea wandugu? Hebu tukubaliane basi

Shida ya nchi hii ndugu yangu ni namna ya kuchagua priorities. Wao wanachojua na kukipenda ni kuchukua maelfu ya shilingi kama imprest za safari za mikoani na ughaibuni wakati wananchi wakiwa na hali duni za maisha.

Tatizo jingine ni kuwa sisi wananchi tunadanganyika na kusahau kwa haraka sana, na kama tungekuwa makini, CCM haingekuwepo madarakani leo!
 
Ni mtoto wa mfalme, ni kijana ambaye ana influence kuliko vijana wote, msomi kuliko vijana wote, ana kazi nzuri na anayefuata nyayo za Baba

Ikumbukwe ma architectures wa haya mambo wanajikomba kwa mzee na kwakuwa Nchi ishakuwa ya kifalme dogo lazima aingie kwenye siasa ili one day aje kukalia kiti cha mzee by the way wametoka kwenye familia ya kichief - Tz kila kitu kinawezekana ili mradi tu uwe connected

Ongezea ana madaraka kuliko baadhi ya Mawaziri!
 
Mawe 005.JPG
Hiyo ni shule ya Msingi mojawapo huko Sikonge, Tabora. Eneo hili ni maarufu kwa uaribifu wa mazingira kupitia kilima cha tumbaku. kupitia uaribifu wao Halmashauri (W) Sikonge inapata mamilioni ya ruzuku kutoka kwa wanunuzi wa tumbaku huku wakulima wakibaki na madeni ya pembejeo.
 

Attachments

  • Mawe 007.JPG
    Mawe 007.JPG
    137.1 KB · Views: 53
Siku hizi Mh. Rais anaiogopa kauli mbiu yake ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania kama ukoma.

Ni kipindi kirefu sasa sijamsikia akitamka kauli hii, sijui safari hii atakuja na kauli mbiu gani???
 
Re: Ridhiwani JK, ona na hawa!! Originally Posted by Prodigal Son Ni mtoto wa mfalme, ni kijana ambaye ana influence kuliko vijana wote, msomi kuliko vijana wote, ana kazi nzuri na anayefuata nyayo za Baba Ikumbukwe ma architectures wa haya mambo wanajikomba kwa mzee na kwakuwa Nchi ishakuwa ya kifalme dogo lazima aingie kwenye siasa ili one day aje kukalia kiti cha mzee by the way wametoka kwenye familia ya kichief - Tz kila kitu kinawezekana ili mradi tu uwe connected
Ongezea ana madaraka kuliko baadhi ya Mawaziri!

MENE MENE TEKELI NA PERES....sijui kama nimepatia, ila anguko la ufalme huu litakuwa kuu kuliko mnavyodhani. Gharama ya kuingiza watoto wote kwenye siasa za uzandiki kama hizi si ndogo. Ikitokea mapinduzi, ndo kizazi kizima kitaisha...inanikumbusha Bushelvic Revolution kule Russia, ambapo Czar na familia yake walifyekwa wote. Na hata waliosalimika hawathubutu kutumia jina la ukoo ule wa kifalme, maana watmalizwa. Siwaombei mabaya, ila kuna watu wameizunguka hii familia na hawairuhusu ipate mahali pa kuwaza kwa maslahi yao. Mke yuko busy kwenye siasa, baba, watoto, nani wa kuwashauri? Mwisho watajikuta wote wamo katika kila kashfa...na endepo anguko lao litatoke ( na si mbali) basi litakuwa kuu. Hapo ndipo mtashuhudia familia nzima ikisimama kwenye mahakama kwa aibu kuu. Ni maneno yanyoudhi, ila haihitaji PHD kuona mwisho wa ufalme huu. JK yabidi atafakari......washauri wake ndio wanamuingiza king, hawaonekani wao, ila yeye na familia. La UVCCM ni dokezo ya haya
 
Back
Top Bottom