Ridhiwani awapa siku 7 Dr. Slaa na Mtikila kukanusha utajiri wake

hizi data mnazotoa humu ndani zina evidence yoyote kuwa dogo ndio mmiliki??
 
Simple tu baada ya siku 7 ataenda mahakaman,.dr slaa na mtikila kama wanao ushahidi watatoa huko,maana ni kweli kama anavyosema NN kusema sema tu majina ya watu bila ushahid inachosha na itafika time wantanzania watamuita dr slaa mzee wa mabomu na watamamdharau
 
Thanks for the footage but where did he get his doctorate from?

Suprised?
Can be like Prof Majimarefu or Prof Dunga Eyeso.
As he helped alot (for his interest) Yanga and UVCCM, then was awarded honorary doctorate from Kivukoni Universty

If you live "kimjini mjini" title hizo ni common. Wengine hujiita Papaa, Prof, MD, ED, etc. Alwatan hawalitumii sana.
 
Siku saba.....ushahidi upo walete, ushahidi hakuna, walipe fidia au jela. hatutaki domodomo,hii ndio itakua fundisho kwa wanasiasa wetu, sio unapanda juu ya jukwa na kuropoka. Walete evidence na kama iko huyu dogo afungwe.
 
JAMANI WOTE TULIWAONA NA TUNAWAONA KINA MAKONGORO NA KINA MADARAKA AMBAO BABA YAO ALITAWALA MIAKA 23. HAWAJAWAHI KUWA NA HIZI KUFURU ...
DOGO HUJASEMA KITU
:A S-baby:
 
Inasikitisha sana mtoto wa mkuu wa nchi kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kuanza kuongea hovyo hovyo kiasi hicho!!! Inakuwaje anadiriki kusema wazi kuwa anaishi kimjini mjini na kuwa kutembelea magari ya kifahari haimaanishi kuwa ndiye mmiliki.

Inabidi watu watambue kuwa tabia ya mtu huoneshwa zaidi kwa matendo na aina ya marafiki wanaokuzunguka ama kuishi nao na sio kuongea kwa jinsi unavyofikiri.

Hoja iliyotolewa na akina Slaa ni nzito na haitakiwi kujibiwa kirahisi kama huyo dogo anavyofikiri. Naamini ameshurutishwa kutoa maelezo hayo na mtu ama watu fulani. Tumeshuhudia wengi wakitishia kwenda mahakamani lakini wakaishia kutoweka pasipo maelezo
 
Nakushauri acha kupiga kelele kuna mahakama nenda kafungue kesi slaa na mtikila walete evidence,kumbuka tayari watu wanaiona family yako kama watu wa maneno mengi,sasa ukijaribu kuongezea maneno tunaona ni mchezo wenu,mahakamani ndiko haki inapatikana,ina maana hujui na wee ni lawyer?au uliupata kwa bahati mbaya?
 
Naomba kutoa wazo mbadala tafadhali.
Huoni kuwa kafanya uungwana kuwapa siku 7 wathibitishe tuhuma waliozotoa? kama kweli DR slaa anaushahidi kwanini asiutoe hadharani au akamfungulie mashtaka?
kama siku 7 zikipita na Dr slaa hajasema chochote then riz aende mahakamani.
 
Tofauti na yule mtoto wa maskini aliyekuwa akiiba sukari na kumletea mama yake (hakuwa na baba) upo uwezekano wa kuwa na mtoto anayeishi kwa kula sana vya watu wa nje kwa sababu yeye ni mtoto wa kizito au kigogo?Huyu kijana sio yule ambaye dola elfu kumi kwake zilikuwa hazichukui wiki tena wakati anasoma hapa Uingereza, sheria, baada ya kushindwa kusoma na kufaulu kwao huko Tanzania ?What is really nagging me, is his association with people who have been declared persona non grata here in UK. He has link with the most noveau - riches in Tanzania popularly known or uknown ? as 'fisadis' some of them who never even reached secondary schoool level decently.Bwana mdogo anajaribu kujikosha lakini nadhani kila mtu aliyeitazama channel 10 jana wallahi ana maswali mengi zaidi ya majibu:Kwanza, kwanini ana vitabia vya kujihusisha na matajiri na watu wenye miradi inayofadhiliwa one way or the other na ikulu au wizara za serikali? Nini uhusiano wake na kina kaka na oilcom ingawa mzee wao pengine hamjui? Nini uhusiano kati yake na tajiri wa malori Tanzania leo ambaye eti katajirikia kupitia mshindano wa urembo? Halafu hawa wanasheria ambao tunasikia anafanya nao kazi baadhi yao sio mafisadi ingawa TANZANIA CORRUPTION PROMOTION BUREAU, chini ya Bw. Hosea ambaye kakosa aibu na kaacha kujiuzulu baada ya kumhujumu bosi wake tunajua!!! Kweli unaweza kukuta majengo hayo si yake, lakini kajitakia mwenyewe kujihusisha na watu ambao wana maghorofa ya kukodisha ambayo yanaingiza mabilioni (na kwa kuwa wanasaidia CCM na viongozi wake) hata kodi hawalipi!!!Nyerere, kaka, hakuwa mjinga kuwatenga wanawe na siasa, watoto wake ndio wamepotea kwa kushindwa kujua kwamba baba yao aliwataka wawe huru na wafuate ndoto zingine zinazoweza kuwa za heri kwao kuliko za kisiasa. Aliyaona ya Kina Mubarak na kina Gaddafi -maana mali, siasa na watoto katika dunia hii ni mitihani mikubwa ambayo itatufanya wengi twende motoni kwa dhuluma au kushindwa kutenda kilicho haki.Alipokuwa hapa sikuzote nilikuwa nikijiuliza hivi huyu bwana alikuwa akilipiwa fees zake na gharama zake za maisha na nani. Maana, ninavyomjua mzazi wake siamini kwamba alikuwa akimwagia fedha hivyo. Baba, mtoto kajichanganya na mafisadi na katika trei la mayai mabovu ukiwemo basi bahati mbaya nawe ukiitwa yai bovu na kutupwa jalalani. Kinachouma ni kule kuuma mkono unaokulisha na kurudisha inda, tadi na ulafi kwa wale wanaokupenda na kukutakia mema. Naam, hakika Masauni katika hili ni 'malaika' na wabaya wake ni mashetani tu!!!Hivi ni nani yule aliyewahi kusema kwamba : ' Usicheze na mbwa maana kuna siku atakufuata hadi msikitini!'
 
PHP:
riz mdogo wangu hukumwona baba yako mkubwa mkapa alikaa kimya ikamsaidia kusavaivu jaribu kufuata nyayo ya kukaa kimya kabla hujanyea kambi.:evil:
 
HTML:
Nakushauri acha kupiga kelele kuna mahakama nenda kafungue kesi slaa na  mtikila walete evidence,kumbuka tayari watu wanaiona family yako kama  watu wa maneno mengi,sasa ukijaribu kuongezea maneno tunaona ni mchezo  wenu,mahakamani ndiko haki inapatikana,ina maana hujui na wee ni  lawyer?au uliupata kwa bahati mbaya?


point taken
 
HTML:
Naomba kutoa wazo mbadala tafadhali.
Huoni kuwa kafanya uungwana kuwapa siku 7 wathibitishe tuhuma  waliozotoa? kama kweli DR slaa anaushahidi kwanini asiutoe hadharani au  akamfungulie mashtaka?
kama siku 7 zikipita na Dr slaa hajasema chochote then riz aende mahakamani.

Kazi ya kutoa notisi ni ya wanasheria si ya mdai...................................kwa masuala yanayodhaniwa kueleka mahakamani.....ni vyema RIzi akachanja mbuga kuelekea mahakamani kama Manji ambaye anadai fidia ya TSHS 1 tu......hataki nyingi kwa sababu ameshiba.......
 
Non sense .... ni mara ngapi ushahidi umetolewa kwenye mambo wazi kabisa ila isichukuliwe hatua yoyote....kwanza huyu bwana mdogo ujasiri wa kuwapa watu wazima "siku saba" anaupata wapi! hakufunzwa adabu? kwani hana wakubwa kwao?
 
Hebu tusubiri mwanahalisi la kesho...labda litakuwa na mi data na evidence.
 
Tatizo ni kwamba hao wanaomtuhumu sidhani kama wana hard evidence.
hata kwa ushahidi gani Rz 1 HAWEZI KUKUBALI UBILIONEA.
rada,richmond,epa zote zilikataliwa ila baadae ikawa proved kuwa ni kweli

Takukuru ipo kwa ajili ya kumsafisha RZ 1 incase
 
Evidence zitakuwepo, watu si wanamjua huyu kajiroga mwenyewe...bora angekaa kimya.
 
Back
Top Bottom