Ridhiwani awapa siku 7 Dr. Slaa na Mtikila kukanusha utajiri wake

Tatizo ni kwamba hao wanaomtuhumu sidhani kama wana hard evidence.

Ngoja tusubiri NN. Ulitoka ushahidi hadi wa Mkapa kumiliki Kiwira. Si ajabu Dr Slaa ana ushahidi wa kuthibitisha hayo anayoyasema. Hili zoezi la kuvua gamba limesababisha makundi mbali mbali ndani ya chama chao waanze kuchafuana hadharani katika kuwania nafasi ya 2015.

"Hapa mjini jamani tunaishi kimjini si kila kitu unachomuona nacho mtu ni cha kwake," alieleza Ridhiwani katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumatatu Dar es Salaam.

DUh Wanajamvi hebu nisaidieni hapa, kuishi kimjini ndo nini?
 
Ngoja tusubiri NN. Ulitoka ushahidi hadi wa Mkapa kumiliki Kiwira. Si ajabu Dr Slaa ana ushahidi wa kuthibitisha hayo anayoyasema. Hili zoezi la kuvua gamba limesababisha makundi mbali mbali ndani ya chama chao waanze kuchafuana hadharani katika kuwania nafasi ya 2015.

Not to be too skeptical but I will not hold my breath on it because I have seen this movie before.
 
Awamu za uwazi na ukweli hizi AD! Kila mtu aliye kwenye ngazi za uongozi na familia yake inabidi waanike mali zao hadharani. Sasa atazikimbia mali zote na kusema si zake. Ngoja tuone kasheshe hii itaelekea wapi? Siku saba zikiisha labda atafungua kesi na hapo ndipo Dr Slaa ataanika mali zote za Ridhiwan na kuweka uthibitisho kwamba ni zake na Bin Kikwete atadai mali hizo si zake bali ni za Rostam, Al adawi na Mkono. Kazi kweli kweli!

ni kama mchezo wa mdura shule ya msingi
kwa kweli eti hawa ndo watu wanaotuongoza ..
sijui kama kwa mtindo huu tutafika popote....
Ningeshauri siku nyingine Ridhiwani aandikiwe
kitu cha kusema kwenye media hayo mautumbo hapo juu
yatamrudia muda si mrefu ...
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Tatizo ni kwamba hao wanaomtuhumu sidhani kama wana hard evidence.

Nakubaliana na wewe mkuu, tuhumu bila evidence, tena kutoka ngazi za juu sio suala zuri. Upande mwingine, kwa hizi system zetu, ushahidi utatoka wapi?
 
Maana yake ni kuishi kiujanja ujanja.

Kuishi kimjini mjini usipoangalia nafasi yako na nafasi ya familia yako katika masuala ya umma na kiserikali unaweza shtukia unajutia kuropoka, wanaoamua kukaa kimya si wajinga, ni busara.

Dr. Slaa alitaja orodha ya mafisadi muda mrefu tu serikali na ccm wakawa wanamkejeli na leo hii mmekuja na hili la kujivua gamba. Ridhiwani kama ana askili nzuri angefikiria yaliyojilia kujivua gamba kulikotokana na moto aliowasha Dr. Slaa. Na hata Mtikila naye anayoongea huwa ni ya kweli. Dogo usipoangalia na kujiona unajua sheria ulizosomea juzi zisijekukupeleka pabaya.
 
Nakubaliana na wewe mkuu, tuhumu bila evidence, tena kutoka ngazi za juu sio suala zuri. Upande mwingine, kwa hizi system zetu, ushahidi utatoka wapi?

Kwa nchi zetu hizi za Kiafrika mambo ya ushahidi yako nyuma vibaya mno.
 
Kuishi kimjini mjini usipoangalia nafasi yako na nafasi ya familia yako katika masuala ya umma na kiserikali unaweza shtukia unajutia kuropoka, wanaoamua kukaa kimya si wajinga, ni busara.

Dr. Slaa alitaja orodha ya mafisadi muda mrefu tu serikali na ccm wakawa wanamkejeli na leo hii mmekuja na hili la kujivua gamba. Ridhiwani kama ana askili nzuri angefikiria yaliyojilia kujivua gamba kulikotokana na moto aliowasha Dr. Slaa. Na hata Mtikila naye anayoongea huwa ni ya kweli. Dogo usipoangalia na kujiona unajua sheria ulizosomea juzi zisijekukupeleka pabaya.
Mtikila nchi nzima inajua ukimpa kidogo unamtuma kazi yoyote naogopa kama slaa atakuwa anamnukuu mtikila itamshushia hadhi.
 
alitueleza yafuatayo;
-yeye sio bilionea,
-ana kashamba kadogo tu ka ekari 1.5 kule Bagamoyo,
-ka gari kamoja kadogo aina ya Toyota Camry tena mtumba,
-vi akaunti vitatu tu kwenye benki za CRDB, Stanbic na NBC,
-wala sijasafiri nje tangu nimalize masomo yangu UK waulizeni Idara ya Uhamiaji kama nadanganya,
-sina maghorofa, sina malori, sina chochote zaidi ya hivyo nilivyovitaja,
-hata mimi huwa nachacha nakosa fedha hadi wakati mwingine hulazimika kwenda kwa baba kuomba msaada (mfano juzi nilikwenda kukopa kabilioni kamoja tu kwa mzee Duh!!!!) kwenye bold ni simulation yangu.
 
Back
Top Bottom