Ridhiwan Kikwete: Mimi si fisadi

“Ninatambua ninachokifanya na nina malengo. Ninachohangaika nacho kwa sasa ni kijishamba changu nilichoachiwa na babu yangu, nataka nikope fedha nikiimarishe. Sina fedha jamani, akaunti yangu haina hata milioni 10. Lakini nayajua madhara ya kuwa mwanasiasa ni kama haya, kuzushiwa. Sitasema kitu na hutanisikia nikisema kitu kuhusu hili,” alisema Ridhiwan kwa sauti ya masikitiko.
kwa wanaojua kusoma minds za watu, hapa yanayoelezwa ni mengi zaidi na kwa kifupi inaonekana kuwa jamaa hasemi ukweli. Kwani utajiri ni account ya benki tu? what about other assets? what about those which are in names of relatives. Even funny anasema kuwa haongei na waandishi wa habari wakati ameongea na Tanzania daima. Any way still si haki kumshutumu Ridhiwani, kwa sababu hata kama amepokea hela za EPA kupitia mkono wa tatu sio kosa lake hata sisi in one way or the other huenda zimetufikia bila kujijua
 
Fidel80 kauliza VX ni la serikali au la kwake?

Na unaposema ni kitu cha kawaida kwa mtoto wa Rais kuwa na masilahi yake kupitia Baba yake unaonyesha huelewi swala zima la ufisadi. Huo ndio ufisadi wenyewe tunaouongelea.

Kwa kuangalia ulivyo ongea hapo juu, nasema wewe ni fisadi la kutupwa.

Asante sana Mheshimiwa!
Hilo VX kama ni la serikali si'litakuwa limesajiliwa namba za serikali ama lina namba za ikulu?

Swala la ufisadi tusilifanye sasa kumnyima mtu haki zake za msingi, kitu kama shamba, tena liko bagamoyo tena la urithi ajabu nini hapo?

kwa mfano Sasa hivi akiugua sirias atatibiwa kwa gharama za nani? au rais yeye hakupewanafasi ya matibabu kwa familia yake kwa hiyo huo ni ufisadi!

Mimi siamini kama kuna mtu akiambiwa ataje mali zake zote alizonazo na jinsi alivyozipa na akafanya hivyo..lazima kunazingine atazikanyagia.

Tupambane na Mafisadi yaliyoota mizizi mpaka yakakubhu wala siyo vijifisadi mtoto!
Mimi siyo fisadi!!
 
JF kazi nzuri.
Chanzo cha mafisadi na kukua kwa mafisadi ni urithi, urithi wa ukiritimba na kujiamini kwamba hakuna atakayenifanya lolote. Kuanza kuzibana mbegu za ufisadi zisiote kabisa ni kazi nzuri. Atueleze kama fedha anapewa na babaye tujue au naye anatumiwa kutumaliza. Hii vita ni ngumu na anataka watu makini.

Ridhiwani amehusishwa na ufisadi wa IMMA na hii ni kweli masha anahusika na EPA na alikuwa amembeba mtoto wa muungwana. Sasa madhara ya viongozi kurisisha na kufundisha wezi tutayashudia baadaye. Ndio maana hakuna uchunguzi unaokamilika kwani kapu ni lile lile linalojichunguza. tusipo kuwa macho tumiliwa.
 
The Boy Is Dangerous In Featuere The Family In East Cost Make Sure Make Followup On Him Just Gather Any Thing About Him,in Feature Will Be Of Good Use For The Family,just Amewahi Ku Baka,steal,just Gather Information,

wewe unalako na mtoto wa watu.tunataka proof na si kuropoka.
 
tatizo letu ni kujikomba kwa wake na watoto wa viongozi as if hawa watatawala milele. kuna watu walidiriki kumtetea mama kikwete alivyokwenda kushuhudia mfame mswati akiwazalilisha wale mabinti wa kiswati eti mama ni bingwa wa utamaduni.
 
Alisema katika kipindi chote alichofanya kazi ya uwakili katika Kampuni ya uwakili ya IMMMA, akiba ya fedha alizonazo benki hazizidi shilingi milioni 10, jambo linalothibitisha kuwa yeye si fisadi wala hajawahi kumuibia mtu.

Kumbe ufisadi unathibitishwa pale akaunti ya benki inapozidi milioni 10?!
 
naridhika ridhwan si fisadi.nakubali kuwa anafanya siasa na kwa hili anapata changamoto na kusemwasemwa.kitu cha ziada ninachoona ni macho ya husuda kwa kuwa kwake mtoto wa rais.vijana wenzake wanachukulia hilo ili kumpa joto.
 
SOURCE: Sani, burudisho la wasomaji, Namba 500, Jumatano, Juni 04-06-2008

TOTOzzz-1.jpg
 
Kuwa mtoto wa rais sio kwamba hana haki ya kugombea uongozi katika nchi hii. ridhwan atasimama kama raia wa tanzania na kama mwanachana. Tatizo letu watanzania ni kuwa na wivu wa kijinga ( negative envy)
 
KiRidhiwani ni kifisadi kisicho kificho, hicho si kijicho.

Angalia kilivyopata kazi, angalia kinapofanya kazi palivyogubikwa na ukungu wa rushwa za EPA, angalia perception ya influence peddling katika chaguzi za umoja wa vijana CCM etc etc

Kinanuka.
 
MOJA ya mambo yanayonivutia ya wenzetu Weupe (Caucasians), ni namna wasivyopenda ‘kubebwa' au kupewa upendeleo wa aina fulani katika kutimiza ndoto zao maishani.

Chukulia mfano wa Peter Buffet. Huyu ni mtoto wa bilionea nambari tatu duniani, Warren Buffet, lakini amekataa kutumia mapesa ya baba yake katika mapambano yake ya kutimiza ndoto yake maishani.

Katika kitabu chake kinachoitwa "Life is what You Make it: Finding Your Own Path to Fulfillment", Peter anasimulia namna alivyokataa ushauri wa baba yake wa kutaka ajitose kwenye masuala ya fedha, na badala yake akapambana mwenyewe kutimiza ndoto yake ya kuwa mtunzi wa vitabu na mwanamuziki.

Peter anaeleza katika kitabu hicho kwamba; licha ya utajiri mkubwa wa baba yake (Buffet), yeye aliishi maisha ya kawaida kabisa na kuchapa kazi kuifanya ndoto yake kuwa kweli bila kumwagiwa mapesa na baba yake. Hivi sasa Peter Warren Buffet ana studio yake ya kisasa ya muziki na pia ni mtunzi wa vitabu.

Nasema nawaheshimu Caucatians kwa hilo; maana angekuwa ni Mwafrika mwenye utajiri wa Buffet, piga ua, angemlazimisha mwanawe ajifunze masuala ya biashara hata kama hana mapenzi nayo; ilimradi tu afuate nyayo zake!

Na ndiyo maana baadhi ya jamaa zangu inawawia vigumu, mpaka sasa, kuamini kwamba mtoto wa bilionea nambari tatu duniani, Peter Buffet, ni mwanamuziki tu wa kawaida anayeishi kwenye nyumba ndogo tu!

Inawawia vigumu jamaa zangu kuamini hivyo, kwa sababu sisi Weusi tukishakuwa na utajiri au kupata nafasi serikalini hatuna hulka wala utamaduni wa kuwaachia wanetu kupigania wenyewe kutimiza ndoto zao maishani bila ‘kubebwa' na wazazi.

Na baadhi ya wanetu nao wamebweteka kiasi kwamba hawajishughulishi kutambua vipaji na karama ambazo Mungu amewatunuku, na badala yake hung'angania kufuata mkondo wa shughuli za wazazi; hata kama hawana karama nazo.

Suala hili la vigogo ‘kuwabeba' watoto wao katika shughuli wanazozifanya maishani au hata katika ajira fulani fulani; licha ya kutokuwa na karama nazo, lina madhara kidogo katika shughuli au biashara ya familia, lakini lina madhara makubwa mno katika fani ya siasa au katika ajira za umma.

Madhara hayo makubwa katika fani ya siasa au kwenye ajira za umma yanatokana na kuwepo mgongano mkubwa wa kimaslahi (conflict of interest) kwa kigogo ‘anayembeba' mwanawe.

Na sote tunajua kuwa penye mgongano wa kimaslahi kuna uonevu, uminyaji haki na kukwazana kimaendeleo; iwe ni kwa mtu mmoja mmoja, kikundi au kwa jamii nzima.

Chukulia mfano wa malalamiko ambayo Mbunge wa Bumbuli, William Shelukindo, ameyafikisha makao makuu ya CCM dhidi ya Januari Makamba ambaye ni mtoto wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba na pia ni Msaidizi wa Rais Kikwete.

Shelukindo ameiandikia CCM makao makuu barua mbili za malalamiko kwamba Januari ameanza mapema kampeni za kuwania ubunge wa jimbo hilo kinyume cha taratibu, na kwamba baadhi ya viongozi wa CCM katika wilaya hiyo ‘wanambeba' na ‘kumlinda' kwa sababu tu ni mtoto wa Katibu Mkuu wa CCM (yaani bosi wao).

Ingawa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa, amekaririwa na gazeti hili akisema kwamba CCM imeunda kamati ya watu watatu kuhukumu kesi za wawania ubunge walizozipokea, ni vigumu kuamini kwamba Shelukindo atatendewa haki na kamati hiyo iliyoteuliwa na makao makuu ya CCM ambako baba wa mtuhumiwa ndiye Katibu Mkuu.

Ni vigumu kuamini vilevile kwamba Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, hataiingilia kamati hiyo, kwa njia moja au nyingine, ili tu ‘amlinde' mwanawe Januari Makamba dhidi ya madai hayo yanayoweza kupeperusha ndoto ya kumuona mwanawe anakuwa mbunge wa jimbo hilo.

Nimeangalia kwenye kamusi ya Kiingereza maelezo ya maneno conflict of interests (mgongano wa maslahi) na inasema hivi: A conflict between a person's private interest and public obligations; yaani "mgongano wa maslahi ya mtu binafsi na maslahi ya umma".

Katika hili la Januari Makamba vs William Shelukindo, ni dhahiri kuna mgongano wa kimaslahi kwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba; kwani yeye kama mtendaji mkuu wa CCM makao makuu, itamuwia vigumu ‘kuyabariki' na kuyapitisha maamuzi yoyote ya kamati hiyo dhidi ya mwanawe.

Kwa maneno mengine, uwezekano wa Shelukindo kunyimwa haki kwa sababu ya mgongano huo wa kimaslahi unaomkabili Katibu Mkuu Yusuf Makamba, ni mkubwa. Na si Shelukindo tu ambaye haki yake itabinywa; bali pia wapiga kura wa jimbo la Bumbuli.

Mfano mwingine ni ule unaomhusu aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Hamad Masauni. Huyu aliondolewa kwenye nafasi hiyo na mkutano mkuu wa umoja huo uliofanyika mjini Iringa, hivi karibuni, kwa tuhuma za kughushi (kudanganya) umri.

Lakini wanaofuatilia mambo ndani ya umoja huo wanasema kwamba Masauni ni mwathirika tu wa makundi mawili yanayosigana ndani ya umoja huo, na kwamba suala la kudanganya umri limetumiwa tu kama ‘silaha ya mwisho' ya kumuangamiza.

Inaaminika kuwa kundi lililopanga mikakati ya kumuondoa Masauni liliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa umoja huo, Benno Malisa na mtoto wa Rais Kikwete, Ridhiwan Kikwete.

Inafahamika vilevile kwamba ingawa Ridhiwan Kikwete ni mjumbe tu wa kamati ya utendaji ya chama hicho, lakini ana nguvu kubwa ndani ya umoja huo wa vijana kwa sababu tu baba yake ni Rais na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM!

Na ndiyo maana ilipofahamika kuwa Masauni ametofautiana na kundi la Malisa na Ridhiwan, wachambuzi wa mambo walijua kwamba ni suala la muda tu kabla Masauni hajapoteza kiti chake; maana huwezi kutofautiana na mtoto wa Rais na Mwenyekiti wa CCM wa Taifa, na kisha ukaendelea kubaki salama kwenye nafasi yako!

Hoja hii inakuwa na uzito hasa ukizingatia kwamba ni Rais Kikwete mwenyewe, wakati akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, aliyependekeza mwenyekiti wa UVCCM safari hii atoke upande wa Zanzibar, na hata kuridhia Masauni (anayetokea huko) agombee.

Kama hivyo ndivyo, je; Masauni hakufanyiwa uchunguzi wa awali (vetting) kabla Kikwete na kamati kuu yake hawajapitisha jina lake kugombea uenyekiti wa UVCCM?

Ukweli ni kwamba walichunguza na walilijua mapema suala hilo la kudanganya umri, lakini kwa wakati huo hawakuliona kuwa ni tatizo (kama ambavyo hawaoni baadhi ya mawaziri waliodanganya kuhusu viwango vyao vya elimu kuwa ni tatizo).

Hoja ni kwamba walikuja tu kulitumia suala hilo la umri kumng'oa Masauni madarakani pale alipoanza kutofautiana na kundi la kina Malisa na Ridhiwan ndani ya Umoja huo.

Kwa hiyo, kauli ya Rais Kikwete aliyoitoa Iringa wakati akihutubia mkutano huo mkuu wa UVCCM kwamba Masauni ilibidi ang'olewe kwa sababu alidanganya umri, ina utata.

Ina utata kwa sababu haiwezekani kwamba Kikwete na Kamati Kuu yake ya CCM hawakulijua hilo wakati wanaridhia Masauni agombee uenyekiti wa UVCCM.

Kwa yeyote mwenye kufikirisha bongo yake, ni dhahiri kwamba Kikwete aliunga mkono kung'olewa Masauni kwa sababu Masauni alitofautiana na kundi la UVCCM ambalo yupo mwanawe Ridhiwan; kundi ambalo linampigia kampeni achaguliwe tena kuwa rais kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Kwa ufupi, kulikuwa na mgongano wa kimaslahi kwa Rais Kikwete katika suala hilo la Masauni; kwa vile mtoto wake Ridhiwan alihusika nalo.

Vyovyote vile; Rais huyu asingetarajiwa kwenda kinyume na matakwa ya mwanawe kwenye suala hilo la Masauni. Na nina hakika, Masauni mwenyewe anajihisi kuonewa.

Tukiunganisha yote mawili (la Ridhiwan na Januari), ni dhahiri kuna juhudi za wazi za baba wa watoto hawa za ‘kuwabeba' ili wapande haraka ngazi za kisiasa wakati wangalipo madarakani. Binafsi nitashangaa kama Ridhiwan hatakuwa mbunge (kupitia UVCCM) katika ngwe ya mwisho ya urais wa baba yake!

Najua kuna watakaodai kwamba watoto hawa wa wakubwa wana sifa za uongozi wa kisiasa, na kwamba ‘hawabebwi' na baba zao, lakini nami nitawauliza: Nani alimjua Januari Makamba kama mwanasiasa kabla Yusuf Makamba hajawa Katibu Mkuu wa CCM? Nani alimjua Ridhiwan Kikwete kama ana sifa za uongozi wa kisiasa kabla Jakaya Kikwete hajawa Rais wa Tanzania?

Hata hivyo; nikimbilie kusema kwamba sina hakika kama ni Kikwete na Makamba wanaowalazimisha watoto wao kuwa wanasiasa au ni watoto wenyewe ndiyo wanaowashinikiza wazazi wao ‘wawabebe' kisiasa ili wawaache pazuri kabla hawajaondoka madarakani.

Vyovyote vile; kuna mgongano wa kimaslahi katika utekelezaji wa hatua za watawala wetu za ‘kuwabeba' kisiasa watoto wao. Na kama nilivyosema mwanzo, penye mgongano wa namna hiyo kuna uonevu na kunyimana haki si kwa mtu mmoja mmoja tu; bali kwa jamii nzima.

Sasa, najua ni vigumu watawala wetu kuwa na hulka za kina Warren Buffet za kuwaachia watoto wao wagundue wenyewe vipaji vyao na wapiganie wenyewe kutimiza ndoto zao, lakini vigogo wetu, angalau basi, wangesubiri kwanza waondoke madarakani ndipo watoto wao wajitose kwenye siasa.

Nina hakika hilo lingepunguza conflict of interests ninazozizungumzia na pia lingepunguza upendeleo wa watoto wa wakubwa (nepotism) hata katika ajira nyingine.

Ushauri wangu wa mwisho kwa watawala wetu, ni kwamba wawaachie watoto wao wagundue wenyewe karama na vipaji walivyopewa na Mungu badala ya kuwang'ang'aniza waingie katika siasa au katika ajira ambazo hawazipendi au wasizo na sifa nazo.

Na watoto nao wajitazame wenyewe na kujiuliza wanataka kufanya nini maishani, na kisha waanze wenyewe kupigania kutimiza ndoto zao hizo badala ya kusubiri ‘kubebwa' na wazazi wao; hata kama wazazi wana utajiri na hekima sawa na Mfalme Suleiman! Nawashauri wajifunze kutoka kwa Peter Warren Buffet – mtoto wa bilionea nambari tatu duniani.

Wakifanya hivyo, watapata furaha maishani; hasa watakapovuna jasho lao wenyewe na kufurahia taaluma walizojichagulia na ambazo Mungu aliwatunukia karama.

Kwa hakika, wakati mwingine huwa najiuliza (kwa mfano) iwapo Waziri wa Ulinzi, Hussein Mwinyi (mtoto wa Rais wa zamani, Ali Hassan Mwinyi) anafarijika kitaaluma kufanya kazi hiyo badala ya ile aliyoisomea ya udaktari wa tiba.

Hivi mtu anawezaje kusota kwa miaka saba akisomea udaktari wa tiba, na kisha anapohitimu akubali kuwa Waziri wa Ulinzi na kujishughulisha na masuala ya makombora, vifaru, AK 47 nk ambayo ni mbali kabisa na taaluma yake? Nina hakika Hussein Mwinyi angekuwa daktari mzuri tu wa tiba kuliko alivyo Waziri wa Ulinzi!

Tafakari.

Imeandikwa na Johnson Mbwambo wa Raia Mwema

Nimevutiwa sana na makala hii..Sijui wenzangu mnasemaje!
 

Tukiunganisha yote mawili (la Ridhiwan na Januari), ni dhahiri kuna juhudi za wazi za baba wa watoto hawa za ‘kuwabeba' ili wapande haraka ngazi za kisiasa wakati wangalipo madarakani. Binafsi nitashangaa kama Ridhiwan hatakuwa mbunge (kupitia UVCCM) katika ngwe ya mwisho ya urais wa baba yake!


Tatizo lipo hapo kwenye pink UVCCM hawana kiti cha wanaume.....hoja ipo katika makala hii. Mmmmh madhara ya umaskini ni makubwa kuliko tunavyoyajua.

Yote hii GS ni umaskini tu....hofu ya badae tusijie kufa njaa na kuchekwa! hakuna la zaidi....mentallity ya kimaskini inaweza kukufundisha kuwa baada ya miaka 10 unaweza ku lost hebu mweke mwanao kwenye system ili usijeumbuka fainali uzeeni au ili kama ukiharibu basi mwanao awe kwenye system watu waogope kukufix badae ...hebu fikiria mzee mwinyi leo hii angekuwa na kesi ya ufisadi mwanae ndiyo huyo mngemuanzia wapi????

Mix with yours
 
Ntashangaa sana kama baada ya miaka ishirini ijayo bado Tanzania tutaendelea kupata viongozi ati kwasababu baba na mama zao pia walikuwa viongozi. Kama hawa vijana ni viongozi hodari basi wanaweza kuwa viongozi, lakini sitegemei yatakuwa ni mambo yale yale ya kutumia kujuana hata kwa watu wasio na sifa za kutuongoza. Gharama yake imeshakuwa kubwa mno kwa Taifa.
 
Namheshimu sana Ndugu Mbwambo. Hivyo napenda kumpa zoezi moja. Ajitahidi kuwajua kina Ridhwan na January Makamba kama wao na sio watoto wa "wakubwa" halafu ndio atoe judgment yake. Pia kuhusu suala la Hussein Mwinyi na elimu yake ya udaktari, napenda kuuliza kuwa ni wanasiasa ama viongozi gani na wangapi wamesomea sayansi ya siasa ama utawala? Hivi hakuna wahandisi ambao ni mawaziri tena wa wizara tofauti na elimu zao? Hivi kaka Mbwambo katika maisha yake yote amefanya kazi ile tu inayoendana na elimu ama fani aliyosomea tu? Lakini pia yeye kama mwandishi asingependa kuona mwanawe mmojawapo anakuwa muandishi na akapata mafanikio kama yeye? Lakini pia anaposema kuwa wazungu hawapendi kubebwa anaamini hivyo ama ni njia ya kurembesha maandiko yake? Hivi kweli mfano wa mtoto wa Buffet ambaye baba yake anajulikana duniani kote kuwa ni tajiri asiye na makuu ndio uwe mfano wa wazungu wote?

Ni hayo tu...

Omarilyas
 
Namheshimu sana Ndugu Mbwambo. Hivyo napenda kumpa zoezi moja. Ajitahidi kuwajua kina Ridhwan na January Makamba kama wao na sio watoto wa "wakubwa" halafu ndio atoe judgment yake. Pia kuhusu suala la Hussein Mwinyi na elimu yake ya udaktari, napenda kuuliza kuwa ni wanasiasa ama viongozi gani na wangapi wamesomea sayansi ya siasa ama utawala? Hivi hakuna wahandisi ambao ni mawaziri tena wa wizara tofauti na elimu zao? Hivi kaka Mbwambo katika maisha yake yote amefanya kazi ile tu inayoendana na elimu ama fani aliyosomea tu? Lakini pia yeye kama mwandishi asingependa kuona mwanawe mmojawapo anakuwa muandishi na akapata mafanikio kama yeye? Lakini pia anaposema kuwa wazungu hawapendi kubebwa anaamini hivyo ama ni njia ya kurembesha maandiko yake? Hivi kweli mfano wa mtoto wa Buffet ambaye baba yake anajulikana duniani kote kuwa ni tajiri asiye na makuu ndio uwe mfano wa wazungu wote?

Ni hayo tu...

Omarilyas

Wewe unayewajua hebu tuambie opinion au judgement yako.
 
Kutumia caucasians kama mfano unakuwa umekosea.

Mfano hai na rahisi sana ni The Bush family (Baba na mtoto) and the Kennedy family in the U.S. (Karibu ukoo mzima hahaha) Mara nyingi ukizaliwa kwenye familia ya viongozi watoto huishia huko huko. Ni sawasawa tu na ukiwa umezaliwa kwenye familia ambayo baba ni daktari mama daktari unashangaa mtoto anakuwa na nia ya kusoma masomo ya sayansi na wakati mwingine kutaka kuwa daktari kama wazazi wake.

Kweli kwamba hili ni tatizo haswa ikiwa mtoto anadhani ni HAKI YAKE kuwa kiongozi badala ya wajibu unaohitaji kushughulikiwa kwa kujinoa. Hili sio tatizo kwa nchi masikini tu au kwa Tanzania tu ni tatizo kwenye jamii nyingi kila kona ya dunia.

Swali ni je wanao uwezo wa kuongoza na wanajinoa vipi kufanya vizuri katika uongozi.
 
Mwandishi akija na hoja hiyo ya urithi katika politics na kwa mfano aliotoa wa Caucasian Buffet, wengine watakuja na mifano ya akina Bush, Kennedy, Benigno Aquino, Corazon Aquino etc.

Vipi tukihoji kwanini Engineer John Pombe Maghufuli (I like uchapaji kazi wa huyu jamaa....) apewe maswala ya uvuvi.

Hivi kuna siri ya kuwaweka madaktari katika wizara ya ulinzi..?Nakumbuka Prof Sarungi alipewa hii wizara,wakati jamaa ni mashine ya mifupa
 
Namheshimu sana Ndugu Mbwambo. Hivyo napenda kumpa zoezi moja. Ajitahidi kuwajua kina Ridhwan na January Makamba kama wao na sio watoto wa "wakubwa" halafu ndio atoe judgment yake. Pia kuhusu suala la Hussein Mwinyi na elimu yake ya udaktari, napenda kuuliza kuwa ni wanasiasa ama viongozi gani na wangapi wamesomea sayansi ya siasa ama utawala? Hivi hakuna wahandisi ambao ni mawaziri tena wa wizara tofauti na elimu zao? Hivi kaka Mbwambo katika maisha yake yote amefanya kazi ile tu inayoendana na elimu ama fani aliyosomea tu? Lakini pia yeye kama mwandishi asingependa kuona mwanawe mmojawapo anakuwa muandishi na akapata mafanikio kama yeye? Lakini pia anaposema kuwa wazungu hawapendi kubebwa anaamini hivyo ama ni njia ya kurembesha maandiko yake? Hivi kweli mfano wa mtoto wa Buffet ambaye baba yake anajulikana duniani kote kuwa ni tajiri asiye na makuu ndio uwe mfano wa wazungu wote?

Ni hayo tu...

Omarilyas

Hivi hata ukiamua kumjua Ridhiwani na Januari kama wao na si watoto wa wakubwa,unafikiri utaona nini katika maisha yao?Tuache unafiki!
 
Back
Top Bottom