BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
paaaaah!...anaona nyota, anaona kihindihindi. Miguu yake haina nguvu imekuwa kama ya mtoto anayejifunza kutembea ambapo hawezi kusimama kabla ya kupiga mweleka. Anaona dunia yote inazunguka...anajaribu kusimama ili auonyeshe Ulimwengu kwamba lile sumbwi alilotandikwa usoni halijamuathiri...lakini miguu haishiki chini...anapiga mweleka tena. Pambano limekwisha na kidomodomo kimefungwa.
Huyu si mpiganaji ni mhuni tu ambae anapenda kuwashika wapinzani wake ili wasipate nafasi ya kurusha masumbwi yao. Ndondi kama ilivyo mchezo wowote ule una sheria zake na huyu jamaa alikuwa hafuati sheria hivyo ilibidi referee aingilie kila alipokuwa anazivunja sheria hizo. Siri yake imeshafichuka, mkono kwa mkono haoni ndani, anavizia kumuweka mpinzani kwenye kamba na kumshika ili afanye uhuni wake, lakini akikutana na referee makini basi atakuwa analalama kila siku.
Jamaa yuko kwenye usingizi mzito baada ya sumbwi la uhakika