Richmond watimka na bilioni 23 za walipa kodi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,009
Siri ya wizi mkubwa Richmond

Mwandishi Wetu Januari 28, 2009
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Watimka na mabilioni ya walipa kodi

Walichotewa kabla hata ya kazi​

WAKATI Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisubiriwa na wabunge kuwasilisha taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge kuhusu kampuni ya Richmond Development, kampuni hiyo iliyorithiwa na kampuni ya Dowans, ilitokomea na zaidi ya Sh. bilioni 23, Raia Mwema imebaini.

Kinyume cha maelezo yaliyowahi kutolewa na baadhi ya viongozi wakuu serikalini katika Bunge, kwamba Richmond haikuwahi kupewa fedha za Serikali, ukweli ni kwamba kampuni hiyo ilichotewa zaidi ya Sh. bilioni 30 (Dola 30,696,598 za Marekani).

Kiasi hicho ni sawa na asilimia 35 ya gharama ya kodi ambayo msingi wake ulikuwa kufanikisha mchakato wa ufunguaji wa hati ya muamana (letter of credit) kati ya kampuni hiyo na Benki ya Biashara.

Malipo hayo ya asilimia 35 ni utekelezaji wa makubalino yaliyofikiwa awali, kati ya Serikali na wawakilishi wa kampuni ya Richmond Development.

Uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa baada ya kupewa kitita hicho cha zaidi ya Sh bilioni 30, Richmond ilipewa masharti ya kurejesha fedha hizo serikalini katika malipo ambayo yangefanyika kwa awamu tatu.

Hesabu zilizofanywa ni kwamba Richmond ilitakiwa kurejesha serikalini dola 1,279,044 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 1.3), kila mwezi, lakini katika mikupuo (awamu) mitatu.


Hesabu hizo zinabainisha kuwa kama makubaliano hayo yangefanyika bila ukorofi au kasoro yoyote, Richmond ingefanikiwa kurejesha serikalini fedha ilizopewa katika miaka miwili. Kwa tafsiri nyingine ni kwamba, Richmond ingelipa deni hilo serikalini ndani ya muda wa uhai wa mkataba wake na Serikali, ambao ni miaka miwili.

Lakini uchunguzi zaidi wa Raia Mwema umebaini kuwa malipo ya awali yalipaswa kuanza kufanyika Novemba, mwaka 2007. Hata hivyo, kutokana na utata wa kampuni ya Richmond hasa kwa upande wa uwezo wake kiteknolojia na utendaji, kampuni hiyo iliuza shughuli zake kwa kampuni nyingine binafsi ya Dowans.

Imebainika kuwa wakati mchakato wa uuzaji wa shughuli za kampuni hiyo kwa Dowans unafanyika, Richmond ilikuwa haijarejesha fedha ilizopewa na Serikali na kwa kuwa Dowans ndiyo iliyobeba mikoba, ilipaswa kuendeleza urejeshaji huo wa fedha.

Kutokana na hali hiyo ya fedha za Serikali kubaki kwa 'wawekezaji' hao waliopasiana mpira wa uwajibikaji, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia timu ya watalaamu wa sheria, ilichunguza mkataba kati yake na Richmond ambao ulirithiwa na Dowans.

Taarifa ya timu ya wanasheria wa TANESCO ilibaini kuwa mkataba huo hauna nguvu za kisheria na kuamuru uvunjwe. Mkataba ukavunjwa rasmi Agosti mosi, mwaka 2008.

Hata hivyo, wakati mkataba huo unavunjwa uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa fedha zilizopaswa kurejeshwa Serikali hazikuwa zimerejeshwa zote.

Imebainika kuwa fedha zilizorejeshwa hadi mkataba unavunjwa ni jumla ya dola 7,674,186 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 7.7), huku dola za Marekani 23,022,412 (zaidi ya Sh. bilioni 23) zikibakia kwa Richmond na mrithi wake Dowans.


Taarifa zaidi za kiuchunguzi zinaeleza kuwa kutokana na hali hiyo Bodi ya TANESCO pamoja na uongozi wa shirika hilo umekwisha kuchukua hatua.

Hizo ni pamoja na maagizo ya Bodi ya TANESCO kwa uongozi wa shirika hilo kuchukua hatua zinazostahili kuhusu deni hilo na kutokana na maagizo hayo, uongozi wa TANESCO ulilazimika kutoa taarifa rasmi serikalini ili hatimaye ijulikane namna fedha hizo zitakavyorejeshwa.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), imechunguza mchakato huo na kubaini kuwa Serikali ilitoa fedha hizo kwa Richmond.

Ofisi hiyo ya CAG, katika taarifa yake ya ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka ulioishia Desemba 31, mwaka 2007, imeweka bayana kuwa fedha hizo bado hazijarejeshwa serikalini.

"Tunafahamu kutokana na taarifa za uongozi kwamba mkataba kati ya TANESCO na Dowans ulivunjwa Agosti mosi, 2008. Matokeo yake ni kwamba kiasi cha fedha kilichotolewa na kutakiwa kurejeshwa kinaweza kuwa hasara kwa TANESCO au Serikali," inaeleza sehemu ya waraka rasmi wa ofisi ya CAG kwa serikali ambao Raia Mwema imeuona.

Kampuni ya Richmond Development ilipewa zabuni tata na Serikali kuagiza mitambo ili kuzalisha umeme wa dharura nchini.


Kutokana na utata wa zabuni hiyo, Bunge lililazimika kuunda Kamati Teule kuchunguza na kubaini upungufu ambao hatimaye ulimgharimu aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri Nazir Karamagi na Dk. Ibharim Msabaha waliojiuzulu Februari 2008.

Mbali na viongozi hao kujiuzulu, Kamati ya Bunge iliwasilisha mapendekezo 23 yanayohitaji kufanyiwa kazi na Serikali. Mapendekezo hayo ni pamoja na kuwawajibisha baadhi ya watendaji wa Serikali na baadhi ya vyombo nyeti, akiwamo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

Katika mkutano wa Bunge ulioanza wiki hii, Serikali inatarajiwa kuwasilisha taarifa yake kuhusu utekelezaji wa mapendekezo hayo. Taarifa hiyo inatarajiwa kuwasilishwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.


 
Waiting for the Prime Minister to tell us what actions have been taken so far as per Ushauri wa Kamati ya Bunge.
 
Eeh! makubwa haya si Hosea na wakubwa kibao walitwambia kwamba serikali haikuingia hasara yoyote maana hawa jamaa hawakulipwa kitu?????????

Who are we going to trust in this govt????? Kweli usanii na ulaji in the making!!!!!!!!!!
 
And the President lied to us. Remember when he said that not a single cent had been paid to Richmond by the government?
 
Eeh! makubwa haya si Hosea na wakubwa kibao walitwambia kwamba serikali haikuingia hasara yoyote maana hawa jamaa hawakulipwa kitu?????????

Who are we going to trust in this govt????? Kweli usanii na ulaji in the making!!!!!!!!!!

Mkuu, sasa kama mabilioni haya waligawana ulitaka wayaite hasara kweli!!!!!
 
Back
Top Bottom