Richmond: Sitta anahusika pia?

Anawakaribisha bila kujiridhisha na uhalali wa Kampuni yenyewe? Anyway, uwekezaji wenyewe nako ni "wizi in disguise", if you like! Mkapa mwenyewe anajuta kuwaalika wezi (jina zuri la wawekezaji) kuja kupora rasilimali zetu! Wakati Mkapa anajutia vitendo hivyo JK yuko busy kuwaalika wezi kuja kuendeleza uporaji! Hivi watu kabla ya kuingia Ikulu huwa wanaacha akili zao nje ya Ikulu na kuzirudia wakati wanatoka huko? Simwelewi kabisa JK kwa kuwaalika wezi kuja kupora mali zetu!
That is what it means to darling of west...ambao wewe unasema we cannot do without them..unachanganya comment zako...ndugu nchi hii itajengwa na watanzania kama india, china na malaysia zilivyojengwa na wao wenyewe..si lazima ujipendekeze kwa hao wezi wazungu ..
 
Kama Spika 6 ni msafi katika kuwasiliana na Kampuni hewa na kukaribishwa lunch na mmiliki wake, basi sioni sababu ya kumlaumu Rostam kwa kuwa anwani yake ilitumiwa na kampuni hiyo! Ni sawa na kumlaumu Hoseah kwa ripoti yake na kuisifu ile ya Mwakyembe pamoja na kwamba aliliambia taifa kwamba kuna mambo aliyaacha (haijulikani ameyahifadhi kwa ajili ya familia yake au kwa ajili ya kutumia kama fimbo ya kisiasa wakati utakapofika)! Tusiwe makengeza pindi tuhuma zinapoanza kuchukua mkondo mpya! Tupigane na ufisadi kama ulivyo na sio kupigana na watu (we against them)!

Japo hatusemi kama ni msafi moja kwa moja Ila Spika 6 atleast unaweza kuona alikuwa na sababu ya kuwasiliana na bwana Gire .... Ni yeye ndiye aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa TIC kipindi hicho,kwahiyo ni lazima awasiliane na wawekezaji wote. Bwana Rostam je?alikuwa ni secretary wa Gire?
 
Haya sasa kazi ya kutafuta mchawi imeanza tena yaani MIAFRIKA jamani hatuwezi kwisha Ujinga...

1. Richmond ni shrika feki haikuwa imesajiliwa mahala popote Houston iweje leo isomeke kwamba mawasiliano ya Sitta na Gire yalihusu mitambo ya Richmond wakati shirika hilo halikuwepo. Hata kama tukifuata site ya Richmond inasema shirika hilo limesajiliwa mwaka 2003, miaka ya nyuma wamekiri wenyewe kwamba Gire alikuwa na na a SMALL PRESS company huko Houston, Texas.

2. Mwaka 2001 au 2002 hapakuwepo na dharura ya umeme kiasi kwamba tulihitaji msaada wa kuzalisha umeme. Umeme ulikuwa haukatiki kama ilivyotokea mwaka 2005 hadi 2006 iweje mazungumzo ya Sitta na Gire yahusiane na Mitambo ya Richmond wakati hapakuwa na muswada wala tender yoyote iliyohitaji manunuzi ya mitambo ya umeme. Huyu Sitta angeweza vipi kuingiza mitambo hiyo pasipo kuwepo na mahitaji yake wala Tanesco hawaihitaji msaada huo! angeifunga huko TIC?.

3. Inashangaza sana kuona Sitta aliwasiliana na Gire lakini haishangazi kuona balozi na mawaziri wakitetea hoja nzima ya ununuzi wa mitambo ya Richmond wakifagiliwa!.. Kosa sii kuzungumza na mtu ila makosa ni pale matendo yanapotokea, hata kama Sitta alizungunmza na Gire kibiashara sii haramu ni mazungumzo tu ambayo yanaweza kubalika ama kukataliwa, ila Lowassa alokuja kutuingiza ktk mkenge basi makosa ni ya viongozi waliofanya hivyo..Na mbona haizungumziwi mawasiliano kati ya Lowassa na Mohammed Gire?..mbona sijawahi kuona barua ya aina hiyo ikitundikwa magazetini wakati inajulikana wazi kwamba ujumbe mkubwa wa viongozi wa serikali walikwenda Houston kuonana na Gire ambaye ambaye aliwaahidi hata kuleta City Transit buses kwa ajili ya mji wa Dar...

jamani jamani kama Sitta alikuwa na matusi yake TIC yatajwe hapa, kuongea na FISADI haiwezi kabisa kuwa sababu ya UFISADI wa mtu, tena basi kichekesho ni kwamba hawa hawa waandishi wa habari wanazipata habari hizi toka kwa mafisadi. Sijui nao tuwaite vipi?
 
Kama Spika 6 ni msafi katika kuwasiliana na Kampuni hewa na kukaribishwa lunch na mmiliki wake, basi sioni sababu ya kumlaumu Rostam kwa kuwa anwani yake ilitumiwa na kampuni hiyo! Ni sawa na kumlaumu Hoseah kwa ripoti yake na kuisifu ile ya Mwakyembe pamoja na kwamba aliliambia taifa kwamba kuna mambo aliyaacha (haijulikani ameyahifadhi kwa ajili ya familia yake au kwa ajili ya kutumia kama fimbo ya kisiasa wakati utakapofika)! Tusiwe makengeza pindi tuhuma zinapoanza kuchukua mkondo mpya! Tupigane na ufisadi kama ulivyo na sio kupigana na watu (we against them)!

Hatusemi kuwa Spika 6 ni msafi moja kwa moja ila kwa kipindi hicho alikuwa na kila sababu ya kuwasiliana na bwana Gire coz yeye ndiye aliyekuwa Mkurugenzi mtendaji wa TIC so sababu ya kuwasiliana isimuhukumu. Isitoshe hakukuwa na tenda za umeme wa Richmond kipindi hicho. kuhusu email ya rostam ni vizuri wakahoji ndio,kwanini itumike yake?Je yeye alikuwa secretary wa bwana Gire?
 
Anawakaribisha bila kujiridhisha na uhalali wa Kampuni yenyewe? Anyway, uwekezaji wenyewe nako ni "wizi in disguise", if you like! Mkapa mwenyewe anajuta kuwaalika wezi (jina zuri la wawekezaji) kuja kupora rasilimali zetu! Wakati Mkapa anajutia vitendo hivyo JK yuko busy kuwaalika wezi kuja kuendeleza uporaji! Hivi watu kabla ya kuingia Ikulu huwa wanaacha akili zao nje ya Ikulu na kuzirudia wakati wanatoka huko? Simwelewi kabisa JK kwa kuwaalika wezi kuja kupora mali zetu!
Inaonekana nguvu iliyo tumika kwenye Chama na Bungeni kumthibiti Sitta, bado haitoshi , sasa nguvu za mafisadi zimeelekezwa kwenye magazeti na kwenye Blog, kweli sitta anawanyima usingizi Mafisadi.
Naona sasa hata issue ya pango la nyumba ni hao hao mafisadi wamemtegeshea ili wawe na mahali pa kuanzia. Na mengi yanayo mtokea sitta kwa sasa ni mbinu chafu za mafisadi ili mwisho wa siku wawe ngoma draw na Spiki , ili akose morale authority ya kuwasema au kusimamia Ukweli.
 
Kwani hapo kunatatizo? sioni kama hapo kuna tatizo lolote, yawezekana aliwasiliana na richmond yenyewe siyo hii uchwara ya tz

ushabiki na umaskini wa watu wa aina yako ndo unaipeleka hii nchi pabaya..Richmond yenyewe ndo ipi?na Richmonf uchwara ndo ipi?Gire huyo huyo aliyeleta richmond unayoita uchwara ndo alimuandikia Sitta..acheni ushabiki wa hovyo hovyo..kwa kifupi Sitta he is in for it
 
hivi unavyo sema Sitta is in for it kwenye suala la Scandal ya kuleta umeme nashindwa kukuelewa au wewe unazungumzia Richmond as Richmond, hutofautishi ile ya uwekezaji way back 2001 na hii ya kufua Umeme?
Any way naomba ukasome remoteness of Damages, utaelewa ni jinsi gani Sitta alivyo mbali na issue hii. Au google tu hilo neno, maelezo yakitoka soma.
 
wewe ndo ukasome.shida yenu mko theoretical mno..kweli mna mahaba mazito sana na spika wenu 6.mkizidiwa mnaanza kuomba muongezewe ulinzi
 
Inaonekana nguvu iliyo tumika kwenye Chama na Bungeni kumthibiti Sitta, bado haitoshi , sasa nguvu za mafisadi zimeelekezwa kwenye magazeti na kwenye Blog, kweli sitta anawanyima usingizi Mafisadi.
Naona sasa hata issue ya pango la nyumba ni hao hao mafisadi wamemtegeshea ili wawe na mahali pa kuanzia. Na mengi yanayo mtokea sitta kwa sasa ni mbinu chafu za mafisadi ili mwisho wa siku wawe ngoma draw na Spiki , ili akose morale authority ya kuwasema au kusimamia Ukweli.

haya ndo ninayoyaita mawazo ya kitoto..babu zima na akili zake unasemaje eti wamemtegeshea.hivi nyie watu mkoje au mmelewa
 
Hafai. He is one of them. Tunahitaji damu mpya sasa. Hawa wazee sasa imetosha. They should all go back to their villages na kusubiri kufa. Wamefanya madhambi makubwa sana kwa taifa hili changa. And I mean all of them. We should stop thinking about recycling any of these unscrupulous and heartless mediocre. Rev. Kishoka, you should consider vying for presidency. Stop counting on these baby-boomers. Hawa wazee tufike mahali tuanze kukumbushia madhambi yao na kuwaadhibu, regardless of their age. Watu wachache hawa hawawezi kubabaisha watu million 40 na zaidi. Mara wazidishe bei ya mazulia, mara mapazia, mara samani za ofisini, yaani they are everywhere for their own personal gains. Sasa, mtu anazidisha bei ya mazulia, then unamfikiria kuwa anaweza kuwa rais wa nchi. And you know what, anaweza kweli kuukwaa urais. Our electorate are in bad shape. They have no idea whatsoever about how best to use their vote to punish corrupt and stupid leaders. Sad!
 
Kigogo,
Mkuu wangu weee.... Haihusu!
Sisi tunazungumzia issue na sii Sitta mwenyewe. haya maswala ya mapenzi yametoka wapi tena kama sio chuki yako mwenyewe. Mkuu hakuna ushahidi hata wa kutunga unajionyesha wazi kwamba Sitta alihusika na deal la Richmond..Richmond ilianzishwa 2003 kama shirika (wanavyodai kina Gire), na Tatizo la Umeme limetokea mwaka 2005 na tender wamepewa Richmond mwaka 2006, Sitta hakuwa hata mjumbe ndani ya vikao vyote vilivyotoa tender hiyo..Ebu wewe tu connectie hizo dots!
Inahusiana vipi na mawasiliano ya Sitta/Gire mwaka 2001 hadi 2002!..
 
Ninachozidi kukijua sasa ni kwamba Watanzania wengi ni wajinga (samahani situkani ila tunapashana ukweli). Kama mtu mwenye uwezo na access ya internet na kuingia JF, tena akaandika na tumaneno twa kingereza kwa mbali bado anashindwa kuelewa hili?

Tatizo letu ni ujinga, na tutazidishiwa ujinga ili werevu waendelee kufaidi. Hapa ni kuondoa ujinga kwanza ndo tunaweza kuendelea, vinginevyo ninakata tamaa.
 
Kigogo,
Mkuu wangu weee.... Haihusu!
Sisi tunazungumzia issue na sii Sitta mwenyewe. haya maswala ya mapenzi yametoka wapi tena kama sio chuki yako mwenyewe. Mkuu hakuna ushahidi hata wa kutunga unajionyesha wazi kwamba Sitta alihusika na deal la Richmond..Richmond ilianzishwa 2003 kama shirika (wanavyodai kina Gire), na Tatizo la Umeme limetokea mwaka 2005 na tender wamepewa Richmond mwaka 2006, Sitta hakuwa hata mjumbe ndani ya vikao vyote vilivyotoa tender hiyo..Ebu wewe tu connectie hizo dots!
Inahusiana vipi na mawasiliano ya Sitta/Gire mwaka 2001 hadi 2002!..
Kula sita ndugu... Hawa jamaa hawaelewi kabisaaaaa........... Siyo kila aliyewasiliana na Richmond alishiriki kwenye huo ufisadi. Cha msingi ni kuangalia uliwasiliana na hiyo RICHard Monduli lini na ukiwa na nia gani. Kwa nafasi ya sitta na mwaka aliowasiliana na hao ndugu wala haitii shaka.

Mbona hamsemi chochote kuhusu ZOMBE..??? Alishiriki kwenye mauwaji lakini aliyempa hicho cheo kabla ya kushiriki kwake wala haguswi na kuzungumziwa. AU tabia ya mbunge kulala bungeni.. halaumiwi mwananchi aliyempa kura......
 
Tunachagua kwa curent merit, sio past legacy, nikikuuzia sera za kwenye ilani yangu, ukanikubali, hii ijajustfy kunichangua, issue ni kama nikishindwa kutekeleza kile nilichoahidi. JK bado hajashindwa ila amechelewa kidogo tuu, hiyo miaka mitano ijayo tutampa tena ili amalizie na kuacha legacy.
Legacy ya Nyerere ni Freedom na Unity
ya Mwinyi ni Mzee wa Ruhksa
Ya Mkapa ni Mr Clean
Tusubiri ya ya JK aka Mr. Trips.

Historia yetu ni kua anayepitishwa na NEC ya CCM ndio atakua raisi wa Serikali ya CCM, na ndio anafaa. Je Sita anaweza pitishwa na NEC? NEC si makini hivyo 'ndio', yaani 'anafaa'.
Mimi (sijaridhika na CCM) naamini CCM haitakuja ikatoa RAISI mzuri kwa maana wote huko CCM hawafai, na ni system ya huko CCM itayomfanya hata mzuri kugeuka na kua mbaya ambaye ni mbinafsi na hajali watu na Nchi kwa ujumla.
 
Enyi wadanganyika, hebu fikirieni tena kidogooooo tu nanyi mtaelewa na pia mtafunuliwa yale yaliyojificha.
 
Kigogo,
Mkuu wangu weee.... Haihusu!
Sisi tunazungumzia issue na sii Sitta mwenyewe. haya maswala ya mapenzi yametoka wapi tena kama sio chuki yako mwenyewe. Mkuu hakuna ushahidi hata wa kutunga unajionyesha wazi kwamba Sitta alihusika na deal la Richmond..Richmond ilianzishwa 2003 kama shirika (wanavyodai kina Gire), na Tatizo la Umeme limetokea mwaka 2005 na tender wamepewa Richmond mwaka 2006, Sitta hakuwa hata mjumbe ndani ya vikao vyote vilivyotoa tender hiyo..Ebu wewe tu connectie hizo dots!
Inahusiana vipi na mawasiliano ya Sitta/Gire mwaka 2001 hadi 2002!..

hahaaaa kiongozi niliposema mahaba sikumaanisha mapenzi ..nilimaanisha kuwa mfuasi wa sitta....ndo mahaba yenyewe hayo..hahaaa
 
That is what it means to darling of west...ambao wewe unasema we cannot do without them..unachanganya comment zako...ndugu nchi hii itajengwa na watanzania kama india, china na malaysia zilivyojengwa na wao wenyewe..si lazima ujipendekeze kwa hao wezi wazungu ..

Hujanipata ndugu kwenye comment zangu! Kuwa na uhusiano na nchi za Magharibi ni kitu kimoja na kuwaita kuja kupora mali zetu ni kitu kingine! Hata hao India, China na Malaysia wana uhusiano vilevile na Marekani au nchi za Magharibi lakini sio uhusiano wa kuwaita mpaka waingie kwenye "Master Bed Room" halafu mwenye nyumba ahamie "sebuleni!" Wake up please!
 
That is what it means to darling of west...ambao wewe unasema we cannot do without them..unachanganya comment zako...ndugu nchi hii itajengwa na watanzania kama india, china na malaysia zilivyojengwa na wao wenyewe..si lazima ujipendekeze kwa hao wezi wazungu ..

India wana mpango wa kukaribisha wawekeja kwa hali na mali kwa ku-sacrifice. Hata China imejengwa na wawekezaji ambapo ili uwapate wengi lazima ku-sacrifice yaani kuwapa utajiri. Sasa hivi China imejikomboa na wawekezaji, na policy yao ya uwekezaji si ya ku-sacrife sana tena kama mwanzo. Hata mishahara imepanda na mazingira ya kazi yameinuliwa, pension na health insurance ni lazima. Vyote hivi havikuwepo walipoanza EPZ huko Zhuhai nk.

Tatizo si wawekezaji, ila kama TZ imeamua ku-sacrifice na kuvuta wawekezaji, je hayo mapato kidogo tupatayo yanaweza kua mtaji? Jibu ni: Haiwezekani kwa ajili ya ufisadi kama Ku-EPA. Hivyo tolea mbali wawekezaji kwa kua kuna ufisadi na CCM. Uwekezaji lazima kuwe na uongozi wa uwajibikaji, kitu ambacho CCM hawana.
 
Back
Top Bottom