Richmond: Sitta anahusika pia?

Tina

JF-Expert Member
Jul 9, 2007
572
579
WAKATI tukielekea katika Mkutano wa 17 wa Bunge unaoanza keshokutwa Jumenne Oktoba 26, 2009, tujikumbushe yaliyojiri Mkutano wa Kumi na Saba miezi michache iloyopita haswa Agosti mosi, 2009 siku ambayo Kamati za bunge ziliwasilisha taarifa zao ikiwamo ile kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. Kwa kuwa sasa gumzo ni Dk. Edward Hosea wa TAKUKURU, nimeweka msisitizo katika Azimio namba 20 la Bunge, ambalo kamati hiyo ilimsafisha Hosea, ili tuone kama watabadili msimamo wao ama watatoa maelezo?

Katika maelezo ya kamati yaliyosomwa na Shelukindo, walikubaliana na maelezo ya serikali kwamba hakukuwa na ukiukwaji wowote wa kisheria uliofanywa na TAKUKURU kwa kusema, "Mheshimiwa Spika Kamati inaridhika na taarifa hiyo."

Tuisome kwa makini taarifa hiyo tuone UADILIFU wa WABUNGE WETU.

Kwa heshima ya mdau mmoja hapa JF nimeambatanisha na barua ya Sitta kwenda kwa Gire (wakati akiwa TIC).

i870_SittatoGire.jpg
 
Attachments

  • KUELEKEA_BUNGENI_RICHMOND.pdf
    253.5 KB · Views: 533
Tina ahsante sana kwa kuiweka ripoti hiyo hapa. Nilitaka niiweke hapa lakini ni file kubwa sana lina page 78. Nimeisoma page chache za mwanzo lina mambo mazito sana inabidi kutafuta muda na kulisoma file lote. Kwa mara nyingine ahsante sana.
 
.... Kwa kuwa sasa gumzo ni Dk. Edward Hosea wa TAKUKURU, nimeweka msisitizo katika Azimio namba 20 la Bunge, ambalo kamati hiyo ilimsafisha Hosea, ili tuone kama watabadili msimamo wao ama watatoa maelezo?

Katika maelezo ya kamati yaliyosomwa na Shelukindo, walikubaliana na maelezo ya serikali kwamba hakukuwa na ukiukwaji wowote wa kisheria uliofanywa na TAKUKURU kwa kusema, "Mheshimiwa Spika Kamati inaridhika na taarifa hiyo."

Tuisome kwa makini taarifa hiyo tuone UADILIFU wa WABUNGE WETU.

Good job Tina;
Ninakubaliana nawe fika, hasa kuhusu swala la sisi watanzania wengi kutokusoma taarifa kwa makini. Nilifanikiwa kuipata nakala ya taarifa halisi aliyosiniwa na Mheshimiwa Shelukindo na kuisoma kwa makini hasa nikitafuta yale ambayo yanahusu yafuatayo:
1. Kuwepo kwa rushwa kwenye mchakato mzima wa ulioipa zabuni kampuni ya Richmond Development Company
2. Kuharibiwa kwa nyaraka halisi za usajili wa kampuni ya Richmond Development Company
3. Kuharibiwa nakubadilishwa kwa ripoti halisi ya uchunguzi kuhusu rushwa katika mchakato ulioipa kampuni ya Richmond Development Company zabuni ya kufua umeme.
4. Kutokuwepo kwa kampuni ya RDEVCO, LLC na ile Richmond Development Company.

1. Nashangaa kusoma kwenye ripoti ya kamati haya yafuatayo
"Mheshimiwa Spika, Kuhusu Bwana Singi Madata, katika utetezi wake, Mamlaka yake ya Nidhamu imeona kuwa, kwa mujibu wa maelekezo ya kazi waliyopewa ya kusaili Makampuni nane (8) yaliyoomba Zabuni ya kufufua Umeme wa dharura alieleza kuwa kazi hiyo ilifanyika kwa muda wa siku mbili.

Pamoja na utetezi huo, Mamlaka yake ya Nidhamu imeona kuwa muda huo ni mfupi na usingewezesha Kamati husika kukamilisha kazi hiyo kwa umakini na ufanisi, pamoja na kuwepo kwa hali ya dharura ya upungufu wa Umeme Nchini.

Hata hivyo, hapakuonekana dalili za mazingira ya rushwa wakati wa kufanya kazi hiyo. Hivyo, Mamlaka yake ya Nidhamu imetoa onyo kwake kwa kutokuwa mwangalifu katika eneo hilo. (Makofi)

Labda mimi ndiye sielewi linalosemwa na kamati na hata wabunge kulipigia makofi. Kama hapakuwepo dalili za rushwa wala mazingira ya rushwa wakati wa kufanya machakato, kazi aliyosimamia ndugu Madata na ni kwa kuhisi kuwepo kwa rushwa ndiyo maana TAKUKURU ilibidi waitwe kufanya uchunguzi. Sasa ikiwa wao wenyewe wanawasilisha taarifa inayosema kuwa hakukuwepo mazaingira na wala dalili za rushwa ni kwa vipi TAKUKURU na hasa Dr. Hoseah walililia damu yake?

2. Kamati inakubaliana na uchunguzi wa vyombo vya dola kuhusu allegations za kuharibiwa kwa nyaraka halisi za usajili wa Richmond Development Company na pia kuharibiwa na kughushiwa ripoti ya uchunguzi wa mazingira ya rushwa uliofanywa na TAKUKURU.
Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa Serikali: “Kamati ya Vyombo vya Dola imekamilisha uchunguzi wake kuhusiana na suala hili; na imebainika kuwa, sikweli kuwa Taarifa rasmi ya TAKUKURU iliyotoa matokea ya uchunguzi kuhusu mchakato wa suala la Richmond ilikataliwa na kuharibiwa na kutolewa nyingine kwa lengo la kuficha ukweli.

Vile vile, Taarifa ya Kamati ya Vyombo vya Dola inaonyesha baada ya upelelezi na uchunguzi wa kina kufanyika wameridhaka kuwa jalada halisi la Richmond lililokuwa BRELA halikuharibiwa na wala hakukuwa na jalada lingine lililowekwa kuficha ukweli wa jambo hili”.
Mheshimiwa Spika, Maoni ya Kamati; Kamati inaridhika na taarifa hiyo
.

3. La kusikitisha ni hili la kung'ang'ania kuwa kuna tofauti kati ya Richmond Development Company na REDVCO LLC; na kwa hili TAKUKURU wanasulubiwa eti walizembea kuona hiyo tofauti.

Naambatanisha copy ya nyaraka walizotumiwa BRELA na Ubalozi wetu Marekani ili kuliweka bayana hilo, na BRELA aidha wameminya au waliwawapa kamati na kamati imeshindwa kuliweka wazi kuwa, Richmond Development Company is an assumed name for REDVCO LLC.

Labda wataalamu washughuli za kusajili makampuni watusaidie kutueleza hili la assumed name, je lina maana kuwupe kwa makumpuni mawili au jina tu la kibiashara? TAKUKURU walisema hili nawakaambiwa hawajui kazi.

Kama vile Tina livyoshauri naomba mziangalie hizi nyaraka kwa uangalifu na kuona jinsi tunavyodanganywa na hizi kamati za kisiasa. Nyaraka hizi hata Bibie Condi Rice amezikubali kuwa ni authentic ila kamati ya waheshimiwa wa bongo wanasema ni za kughushi!

La mwisho ni la kujiuliza kuwa hivi ni nani aliyewaleta Richmond hapa nchi kwa mara ya kwanza, Rostam Aziz au Samwel Sitta. Hebu angalia kwa ungalifu (Zoom kweye kibao cha jina la Samwel Sitta likiwa limetinga mezani) na pichani akiwa amekaribishwa na Mohamed Gire kaka yake Adam Gire (mshatikwa wa Richmond hapa nyumbani). Picha zingeni nazihifadhi kwa sasa!

Ndugu Sitta wakati huo alikuwa ni CEO wa TIC na hapo anaonekana akikutana na wawekezaji wa Richmond kwenye ukumbi wa Greater Houston Convention and Visitors Bureau (GHCVB) ambao Mohamed Gire ni mmoja wa wamiliki wa ukumbi na bureau hiyo; http://www.rdevco.com/mohamedgire.html.

Pia naambatanisha copy ya FAX ambayo ndugu Sitta analimtumia Mohamed Gire wa Richmond Development Company na kumwambia andike hiyo barua ya recommendation aliyoiomba toka TIC kwenda AEC, yaaani aiandike jinsi anavyotaka yeye mwenyewe halafu yeye Sitta kama Executive Director wa TIC atamwaga sahihi tu! Inatisha, jama inatisha.

Ila ndugu Sitta analalama kuwa ndugu Gire pia ana mahusiano na Mr. Sela kitu ambacho inaonekana hakimpendezi bwana mkubwa! ........

Au ndiyo maana Mheshimiwa Spika alilivalia njuga sakata la Richmond?
Just a wild guess.

ZalendoHalisi

BTW AEC ni : African Economic Community na Tanzania ni washiriki wazito tu
 
Attachments

  • KUELEKEA_BUNGENI_RICHMOND-Edited.pdf
    33.4 KB · Views: 238
  • RichMond-01.jpg
    RichMond-01.jpg
    492.8 KB · Views: 122
  • Richmond-Brela.pdf
    232.9 KB · Views: 232
  • Sitta-Gire.pdf
    19.6 KB · Views: 242
Good job Tina;
Ninakubaliana nawe fika, hasa kuhusu swala la sisi watanzania wengi kutokusoma taarifa kwa makini. Nilifanikiwa kuipata nakala ya taarifa halisi aliyosiniwa na Mheshimiwa Shelukindo na kuisoma kwa makini hasa nikitafuta yale ambayo yanahusu yafuatayo:
1. Kuwepo kwa rushwa kwenye mchakato mzima wa ulioipa zabuni kampuni ya Richmond Development Company
2. Kuharibiwa kwa nyaraka halisi za usajili wa kampuni ya Richmond Development Company
3. Kuharibiwa nakubadilishwa kwa ripoti halisi ya uchunguzi kuhusu rushwa katika mchakato ulioipa kampuni ya Richmond Development Company zabuni ya kufua umeme.
4. Kutokuwepo kwa kampuni ya RDEVCO, LLC na ile Richmond Development Company.

1. Nashangaa kusoma kwenye ripoti ya kamati haya yafuatayo

Labda mimi ndiye sielewi linalosemwa na kamati na hata wabunge kulipigia makofi. Kama hapakuwepo dalili za rushwa wala mazingira ya rushwa wakati wa kufanya machakato, kazi aliyosimamia ndugu Madata na ni kwa kuhisi kuwepo kwa rushwa ndiyo maana TAKUKURU ilibidi waitwe kufanya uchunguzi. Sasa ikiwa wao wenyewe wanawasilisha taarifa inayosema kuwa hakukuwepo mazaingira na wala dalili za rushwa ni kwa vipi TAKUKURU na hasa Dr. Hoseah walililia damu yake?

2. Kamati inakubaliana na uchunguzi wa vyombo vya dola kuhusu allegations za kuharibiwa kwa nyaraka halisi za usajili wa Richmond Development Company na pia kuharibiwa na kughushiwa ripoti ya uchunguzi wa mazingira ya rushwa uliofanywa na TAKUKURU.

3. La kusikitisha ni hili la kung'ang'ania kuwa kuna tofauti kati ya Richmond Development Company na REDVCO LLC; na kwa hili TAKUKURU wanasulubiwa eti walizembea kuona hiyo tofauti.

Naambatanisha copy ya nyaraka walizotumiwa BRELA na Ubalozi wetu Marekani ili kuliweka bayana hilo, na BRELA aidha wameminya au waliwawapa kamati na kamati imeshindwa kuliweka wazi kuwa, Richmond Development Company is an assumed name for REDVCO LLC.

Labda wataalamu washughuli za kusajili makampuni watusaidie kutueleza hili la assumed name, je lina maana kuwupe kwa makumpuni mawili au jina tu la kibiashara? TAKUKURU walisema hili nawakaambiwa hawajui kazi.

Kama vile Tina livyoshauri naomba mziangalie hizi nyaraka kwa uangalifu na kuona jinsi tunavyodanganywa na hizi kamati za kisiasa. Nyaraka hizi hata Bibie Condi Rice amezikubali kuwa ni authentic ila kamati ya waheshimiwa wa bongo wanasema ni za kughushi!

La mwisho ni la kujiuliza kuwa hivi ni nani aliyewaleta Richmond hapa nchi kwa mara ya kwanza, Rostam Aziz au Samwel Sitta. Hebu angalia kwa ungalifu (Zoom kweye kibao cha jina la Samwel Sitta likiwa limetinga mezani) na pichani akiwa amekaribishwa na Mohamed Gire kaka yake Adam Gire (mshatikwa wa Richmond hapa nyumbani). Picha zingeni nazihifadhi kwa sasa!

Ndugu Sitta wakati huo alikuwa ni CEO wa TIC na hapo anaonekana akikutana na wawekezaji wa Richmond kwenye ukumbi wa Greater Houston Convention and Visitors Bureau (GHCVB) ambao Mohamed Gire ni mmoja wa wamiliki wa ukumbi na bureau hiyo; http://www.rdevco.com/mohamedgire.html.

Pia naambatanisha copy ya FAX ambayo ndugu Sitta analimtumia Mohamed Gire wa Richmond Development Company na kumwambia andike hiyo barua ya recommendation aliyoiomba toka TIC kwenda AEC, yaaani aiandike jinsi anavyotaka yeye mwenyewe halafu yeye Sitta kama Executive Director wa TIC atamwaga sahihi tu! Inatisha, jama inatisha.

Ila ndugu Sitta analalama kuwa ndugu Gire pia ana mahusiano na Mr. Sela kitu ambacho inaonekana hakimpendezi bwana mkubwa! ........

Au ndiyo maana Mheshimiwa Spika alilivalia njuga sakata la Richmond?
Just a wild guess.

ZalendoHalisi

BTW AEC ni : African Economic Community na Tanzania ni washiriki wazito tu

Mungu wangu, mimi simo naona mambo yanazidi kunoga kuelekea BUNGE LIJALO
 
sasa sijui kuna nini kipya kitaibuka huko, najua moto utawaka, na sasa hivi nasema CCM hakuna kuitana pembeni na kukanyana, safari hii ni unyama unyama tu. Wabunge okoeni nchi yenu jamani
 
Nadhani wengi hawajaona kilichomo humu ndani!!! Kazi kweli kweli
 
Jamani hata mzee Six???? Kumbe Rich Monduli ni dude la ajabu sana eheee??!!!! Haya tutaona mengi mwaka huu
 
Lakini hakuna jipya kutoka kwa wabunge. KWANI WAMESHALAINISHWA apunguze kasi ya kuisulubu Serikali.
 
Richmond kila siku kuna kitu gani kipya au kelele tu. Watu walioiba wawekwe jela, utaratibu wa tender ubadilishwe na bunge lianze kujadili vitu vya maana hatuwezi kutumia miaka zaidi ya miwili kuongelea kitu kimoja. Mikataba mibaya iko kila siku na si Richmond pekee!. I am sick of this shit
 
Jamani hata mzee Six???? Kumbe Rich Monduli ni dude la ajabu sana eheee??!!!! Haya tutaona mengi mwaka huu

huyu sita kila siku mi nasemaga hapa hana lolote la maana sasa kiko wapi.naye ni fisadi tu
 
Richmond kila siku kuna kitu gani kipya au kelele tu. Watu walioiba wawekwe jela, utaratibu wa tender ubadilishwe na bunge lianze kujadili vitu vya maana hatuwezi kutumia miaka zaidi ya miwili kuongelea kitu kimoja. Mikataba mibaya iko kila siku na si Richmond pekee!. I am sick of this shit

na huyo sita awekwe jela maana naye alikuwemo kwenye mchalato kumbe haaaaa
 
Jamani hata mzee Six???? Kumbe Rich Monduli ni dude la ajabu sana eheee??!!!! Haya tutaona mengi mwaka huu

Tina, nakupongeza sana kuhusiana na uchangiaji wako hapa ukumbini. Maana ni mmoja wa akina dada wachache sana hapa jukwaani wanaoshiriki sana katika jukwaa hili la siasa na hasa haya mambo ambayo yameikumba nchi yetu katika miaka hivi ya karibuni ya ufisadi.
 
Utekelezaji wa Serikali ulikuwa:- "Wizara ya Fedha na Uchumi na Benki Kuu ya Tanzania wamechunguza na kuona kuwa malipo ya US$ 4,865,000 yaliyolipwa kwa Kampuni ya Dowans Holdings S.A. iliyorithi majukumu ya Richmond Development Company LLC. ni halali. Malipo hayo yalilipwa tarehe 2 Februari, 2007 ikiwa ni gharama za ndege za usafirishaji wa mitambo ya kukodi ya umeme wa dharura, baada ya
kupokea Invoice Na. EFD786675.
Jamani sii katika maelezo ya kwanza ktk ununuzi wa mitambo ya Dowans tuliambiwa Dowans hawajapewa hata senti moja? hii tena imetoka wapi?..
 
Yanini twaandikia mate na wino upo, tuombe uzima na afya njema tutaona hayo yatakayojiri, kila la heri
 
Back
Top Bottom