Richmond: Ofisi na anuani yao Tanzania anayefahmu! Tuwashtaki!

Albert Msando

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
1,019
171
Nimetafakari sana baada ya kupitia hoja mbalimbali zinazotolewa na wanaJF. Kwa kiasi kikubwa naona tunajiuliza maswali wenyewe na tunajijibu wenyewe. Inawezekana ujumbe wetu unafika au unafikishwa. Lakini anayeufikisha na unafikishwaje hatujui. Hatua gani zinachukuliwa hatujui.

Nimeamua kutoa wazo na kukaribisha maoni na ushauri. Kwa sasa hivi niko kwenye mchakato wa kulifikisha suala la kampuni feki ya Richmond mahakamani. Haiwezekani uhalali wao kisheria uwe una walakini halafu wahamishe (assign) mkataba kwenda kwa kampuni nyingine sisi tulipe! Kama Richmond ilikuwa 'feki' mkataba wake na Tanesco hauwezi kuwa halali. Kama mkataba wake na Tanesco haukuwa halali hawakuwa na 'haki halali' za kuhamisha kwenda Dowans.

Kwa yeyote mwenye nakala ya Mkataba kati Tanesco na Richmond, Mkataba kati ya Richmond na Dowans anipatie au mwenye taarifa wapi tunaweza kupata anijuze.

Ikishindikana naangalia sheria inasemaje kuhusu haki ya mwananchi kudai nakala ya mkataba kutoka serikalini. Wenye uelewa wa sheria tuelimishane ili HAKI ipatikane. Hatuwezi kuibiwa halafu tuendelee kukaa kimya. Kulalamika pekee haitatusaidia. Lazima tutafute suluhu haraka.

Pia anayejua zilipo au zilipokuwepo ofisi za Richmond anifahamishe. Mzee Mwanakijiji msaada wako ni muhimu katika hili!
 
Alberto,
Wasiliana na Invisible kama unataka mkataba huo. Ninayo copy niliyopakua hapa JF siku za nyuma kidogo.
 
Alberto,
Wasiliana na Invisible kama unataka mkataba huo. Ninayo copy niliyopakua hapa JF siku za nyuma kidogo.

Ukiweza nirushie kwenye email. albert@albertmsandolegal.com.

Naendelea kufuatilia docs nyingine. Naamini naweza zipata mahakamani kwenye faili ya Kituo cha Haki za Binadamu kupinga malipo!
 
Back
Top Bottom