Richmond nyingine yazimwa Tanesco

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613


Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 22nd December 2009

MCHAKATO wa kutafuta wazabuni kwa ajili ya kununua mitambo miwili ya kuzalisha umeme wa jumla ya megawati 160 itakayowekwa Dar es Salaam na Mwanza, imebidi urudiwe baada ya kubainika kwamba tathmini iliyofanywa haikuzingatia vigezo muhimu.

Mitambo hiyo inayotarajiwa kununuliwa na ambayo serikali imetoa miezi mitatu kwa mchakato wa kuinunua uwe umekamilika, ni megawati 100 utakaowekwa Dar es Salaam na wa megawati 60 utakaokuwa Mwanza.

Miongoni mwa vigezo ambavyo havikuzingatiwa, ni kile ambacho Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema ni kutojumuishwa kwa ukamilifu gharama za uendeshaji, kwa mtambo wa megawati 60, ambazo kwa wastani ni kubwa.

“Pamoja na maelezo na ufafanuzi uliopatikana kwa barua na kupitia vikao kadhaa wizarani, ilikubalika kuwa tathmini ya Tanesco (Shirika la Umeme Tanzania) haikuzingatia vigezo vingine muhimu vya zabuni,” Ngeleja alisema jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema uamuzi wa kurudia mchakato wa zabuni huo, umeepusha pia mwanya wa kuingiza mambo mengine ambayo hayakustahili katika kufanikisha suala hilo.

Mwaka 2006, wakati wa ukame nchini, serikali iliagiza mitambo ya dharura ya kufua umeme nchini, ambayo baadaye ilikuja kugundulika kuwepo na ukiukwaji wa taratibu katika uingizwaji wake na kuzaa kile ambacho kwa sasa ni maarufu kama sakata la Richmond, moja ya kampuni zilizoshinda zabuni za kuleta mitambo hiyo.

Ngeleja ambaye hata hivyo alisisitiza kwamba siyo uzembe wa Tanesco, alisema kwa kuzingatia umuhimu wa kupatikana mitambo hiyo haraka, shirika limeshauriwa kutumia vipengele muafaka chini ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya 2004 kuanza mchakato mara moja na kupata mkandarasi ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa.

Alisema, “Serikali imeamua ni busara zabuni kurudiwa kwa kuwataka wazabuni wote waliofuzu kwenye mchujo na kuthibitika kuwa wana uwezo wawasilishe takwimu za kuwezesha kufanyika thathmini ya gharama za ununuzi wa mitambo, ujenzi na uendeshaji.”

Akielezea kilichojiri katika zabuni hiyo ya awali ambayo haikupitishwa, Ngeleja alisema kwa kuzingatia gharama za uendeshaji wa mitambo ya uzalishaji umeme, Tanesco iliishauri serikali ifikirie na kufadhili ununuzi wa mitambo hiyo ya Mwanza na Dar es Salaam.

Serikali ilikubali kulipia gharama za kuinunua. Aprili 21, mwaka huu, ilitangazwa zabuni kupitia magazeti huku makisio ya Tanesco kuhusu gharama za miradi hiyo ikiwa takribani Sh bilioni 267.

Tarehe ya mwisho ya kurudisha makabrasha ya zabuni Tanesco, ilikuwa Juni 6, mwaka huu, lakini muda ukaongezwa hadi Julai 3, ili kutoa muda wa kutosha kwa wazabuni kukamilisha makabrasha husika.

Ngeleja alisema wazabuni 30 walinunua makabrasha ya zabuni kwa ajili ya mitambo ya Dar es Salaam na wazabuni 28 kwa ajili ya mitambo ya Mwanza.

“Hata hivyo waliorudisha makabrasha yaliyokamilika kujazwa walifikia watano kwa mitambo ya Dar es Salaam ya megawati 100 na wanne kwa mitambo ya megawati 60,” alisema na kuongeza kuwa matokeo ya tathmini ya zabuni yaliwasilishwa wizarani Septemba 10, mwaka huu.

Baada ya kutafakari ripoti ya Tanesco, Ngeleje alisema Oktoba 4, mwaka huu, wizara iliomba ufafanuzi kutoka shirika hilo kuhusu masuala kadhaa hasa gharama za uendeshaji zikiwemo mafuta na vipuri kwa umri wa mitambo unaokisiwa kuwa wa miaka 30.

Kwa upande wa mitambo ya Dar es Salaam, alisema zabuni ya Tanesco ilielekeza kuhitajika mitambo ya megawati 100 ya kutumia gesi asili, lakini mzabuni aliyependekezwa angeleta mitambo yenye uwezo wa megawati 130, kiasi ambacho hakikuwa katika makadirio ya bajeti, jambo lililochangia pia zabuni kurudiwa.

Alipoulizwa na waandishi wa habari iwapo kulikuwa na uzembe ndani ya Tanesco kiasi cha kushindwa kubaini kasoro hizo, Ngeleja alisema ni upungufu wa kawaida.

Aidha, alisisitiza mitambo hiyo italetwa mara moja baada ya kipindi hicho cha miezi mitatu kilichotolewa.

Alisema haitasubiri kuleta mitambo yote kwa pamoja; badala yake, itakayokuwa imekamilika hata ikiwa michache italetwa mara moja.

Uamuzi wa kuleta mitambo hiyo ya megawati 160, ulitokana na tathmini iliyofanywa na Tanesco mwanzoni mwa mwaka huu kuhusu hali ya uzalishaji wa umeme nchini. Ilithibitika kuwa mfumo wa uzalishaji umeme haukidhi mahitaji na kwamba unahitaji megawati zisizopungua 160 haraka iwezekanavyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Ngeleja aliwaambia waandishi wa habari kwamba hali ya upatikanaji wa bidhaa za petroli unaridhisha na usambazaji wake unaendelea vizuri.




Ilianza hivi:

A new Richmond is coming...


THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

CERTAIN businessmen-cum-politicians implicated in the infamous Richmond deal are now chasing up two brand-new contracts worth more than $100m (approx. 140bn/-) from the state-run Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) for the construction of power generating plants in Dar es Salaam and Mwanza, THISDAY can reveal today.

The two separate energy contracts involve the procurement of a 100-megawatts, gas-fired power plant at Ubungo in Dar es Salaam, and the purchase of a 60MW power plant in Nyakato, Mwanza, which will run on heavy fuel oil.

Government officials have confirmed that the same people said to be behind the 2006 Richmond scandal are now well-positioned to be awarded the contracts using a different company name.

TANESCO received bids for both projects in June this year, but the tender process has since been shrouded in apparent secrecy and controversy.

It is understood that the group of Richmond-tainted businessmen-cum-politicians, working as a syndicate of sorts, submitted bids for the two contracts under another company name, ostensibly in an attempt to hide the identities of the real owners of the firm.

The 'syndicate' is said to be using the same network of government officials who facilitated the Richmond deal, to ensure it stays ahead in the race to land the latest contracts.

"A new Richmond is coming...," a senior government official familiar with the latest TANESCO tenders told THISDAY.

According to government insiders, the bids submitted by the 'syndicate' for the contracts were inflated by more than $30m (approx. 40bn/-).

"These people received inside information on the tenders, and submitted bids for both. In fact, there are reports going around that both contracts have already been awarded to the same people who were behind the Richmond scandal," said the senior government official.

The 'syndicate' is said to have been doing lots of behind-the-scenes maneuvering since early this year to land the new contracts.

"These people have the audacity and dastardly courage to repeat the same methods of fraud, misrepresentation of facts, bribery and what-have-you that they deployed to secure the Richmond contract, this time around as well," said the government official.

Under tender number PA/001/09/HQ/W/016, TANESCO invited bids for the "supply, installation, testing and commissioning" of the emergency,gas-based 100MW power generation plant in Dar es Salaam, on a turn-key basis.

A turn-key project is a type of project that is constructed by a developer and sold or turned over to a buyer (in this case, TANESCO) in a ready-to-use condition.

On the other hand, tender number PA/001/09/HQ/W/018 involves the supply, installation, testing and commissioning of a 60MW power plant in Nyakato, Mwanza, that will use dual-heavy fuel oil for power generation. The proposed Mwanza power plant is also a turn-key project.

According to our government sources, the bid winner(s) for both projects was expected to be picked on the basis of experience, technical capacity, fulfillment of tender requirements, and other such aspects.

“But the word is now out that the one company already awarded both contracts...has never worked in Tanzania before, nor does it have any power generation experience in the whole of Sub-Saharan Africa," the sources said.

Contacted for comment, the Minister for Energy and Minerals, William Ngeleja, asserted that the TANESCO tender board is still in the process of assessing bids from various companies for the two tenders, and no formal decision has been made so far on the bid winner or winners.

“It's too early to comment on this matter now because the tender process is still in the early stages...," the minister told THISDAY.

The official deadline for submission of bids for the two tenders expired on June 5 this year, meaning that TANESCO has been processing the bids for almost six months now.




Source: THISDAY, November 30, 2009

Pinda ategwa bomu
kama la Richmond
.Ni zabuni ya bilioni 140 ya jenereta
.Wababe wa Richmond wako nyuma

WAKATI moto wa mradi wa umeme wa dharura ulioihusu kampuni ya Richmond Development LLC uliomng’oa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ukiwa haujapoa wahusika walioguswa katika sakata hilo wanataka kumtega Waziri Mkuu wa sasa Mizengo Pinda, kuhusiana na mradi mpya wa ununuzi wa majenereta ya kuzalisha megawati 160, KULIKONI limegundua.

Uchunguzi wa KULIKONI umebaini kuwapo taarifa za kukanganya kuhusiana na zilipo hasa nyaraka za zabuni ya ununuzi wa mitambo ya kufua umeme inayotarajiwa kufungwa Dar es Salaam na Mwanza kwa thamani inayofikia Shilingi bilioni 140, miezi zaidi ya miezi mine baada ya zabuni kufunguliwa.

Kumekuwapo taarifa za ndani ya serikali zikieleza kwamba nyaraka za zabuni hiyo sasa zimepelekwa Ofisi ya Waziri Mkuu, baada ya Wizara ya Nishati na Madini kuanza kuigopa zabuni hiyo huku kukiwa na habari za uhakika kwamba tayari kumekuwa na mbinu chafu zinazoendelea katika kutaka kuibua kashfa mpya.

Habari za ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, zimeeleza kwamba hadi mwishoni mwa wiki nyaraka hizo zilikuwa hazijawasilishwa katika ofisi hizo pamoja na watendaji chini ya Pinda kufahamu kuwapo kwa zabuni hiyo iliyotangazwa na Tanesco.

Uchunguzi wa KULIKONI umebaini kwamba ndani ya miezi miwili baada ya zabuni kufunguliwa, wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) walikabidhi mapendekezo yao ya kitaalamu kwa serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini.

Waziri wa Nishati na Madini aliliambia KULIKONI hivi karibuni kwamba mchakato wa zabuni hiyo unaendelea na kwamba hakuna kampuni iliyopatiwa zabuni hiyo, lakini hakuzungumzia kuwa ofisi yake imekwishapokea nyaraka na mapendekezo kutoka Tanesco.
Utata na ‘kiwingu’ kilichotanda katika zabuni hiyo, umeelezwa kutokana na vyombo vya usalama kushitushwa na taarifa za kuwapo kwa wahusika wa Richmond nyuma ya mchakato wa zabuni hiyo na hivyo kuwatahadharisha wahusika waepuke kuingia katika mtego unaoweza kugeuka na kuwa kashfa nyingine nzito.

“Unajua wameshachezea hiyo zabuni sasa wanataka wanawe mikono wamuachie Pinda na wasaidizi wake wachezee moto, kwa kweli hapa kuna mtego unaowekwa ukizingatia hali sasa si nzuri sana kisiasa na kuna watu hasa walioumizwa na kashfa ya Richmond wanataka kufa na mtu,” anasema Ofisa Mwandamizi wa serikali aliyezungumza na KULIKONI Ijumaa iliyooita.

Hata hivyo, taarifa za ndani ya ofisi ya Waziri Mkuu zinaeleza kwamba ofisi hiyo imeanza kufuatilia kwa makini kuhusiana na taarifa za kuwapo mkakati wa kuiingiza katika mtego wa zabuni hiyo ambayo ililenga kupunguza tatizo la umeme nchini kwa serikali kutoa fedha kwa ajili ya kunulia mitambo hiyo.

Jumla la kampuni nane za kigeni zimeomba kupatiwa zabuni ya kuingiza mitambo hiyo na tayari kampuni mbili tofauti zimependekezwa kuwa ndizo zinazofaa huku kukiwa na mkakati mahususi wa kufanya mabadiliko katika mapendekezo hayo ili kuhakikisha kampuni zinazosimamiwa na watu wazito zinapata.

Kampuni zilizoomba zinatoka Canada, Norway, Finland, Korea Kusini, China, Ujerumani na Misri na sasa juhudi zinafanywa ili kampuni mbili kutoka nchi moja ndizo zipewe zabuni zote mbili, ile ya megawati 100 ya Ubungo, Dar es Salaam na megawati 60 ya Nyakato, Mwanza.

Habari zinaeleza kwamba kumekuwapo na mbinu za kutumia hesabu za matumizi ya mafuta kulingana na mwinuko kutoka usawa wa bahari, hesabu ambazo zimekuwa zikichezewa kwa nia ya kuvuruga mapendekezo ya wataalamu.
Uchunguzi wa KULIKONI umebaini kampuni zilizoomba mradi wa megawati 100 za Ubungo ni pamoja na; Aaneen Power Cooperating ya Canada, Jacobsen Elektro (Norway), Wartsila (Finland), Kolon & Samsung (Korea Kusini), na China National ya China.

China National wao wameomba wakitoa makadirio ya juu ya gharama za mradi wakiwa wamekadiria kutumia Dola za Marekani milioni 149.5 (wastani wa Shilingi bilioni 200), wakati Jacobsen Elektro wamependekeza euro 95,711,730 (karibu Sh bilioni 193).

Kampuni ya Aaneen Power Cooperating wao wamewasilisha gharama za euro millioni 94.95 (wastani wa Shilingi bilioni 191.7), wakifuatiwa na Kolon & Samsung's Shilingi bilioni 133. Kampuni ya Wartsila wao wameonyesha kupanga kutumia euro milioni 62.5 (Sh bilioni 126). Wartsila wameelezwa kutumia uzoefu wao katika biashara nchini Tanzania katika kucheza na hesabu za kibiashara.

Kwa upande wa mradi wa Nyakato, kampuni ya MAN Diesel iliwasilisha kutumia gharama za euro milioni 77.6 (Sh bilioni 156.6); Wartsila nao wameomba tena kwa kuonyesha kutumia gharama za euro milioni 49.8 (Sh bilioni 100); UNATRAC euro 67,681,467 (Sh bilioni 136.6); na Semco Maritime/Rolls Royce Marine wao wamepanga kutumia Sh bilioni 102.

Tanesco ilitangaza zabuni hiyo kupitia tangazo la zabuni namba PA/001/HQ/W018 kwa jenereta ya megawati 60 itakayofungwa eneo la Nyakato, Mwanza na zabuni namba PA/001/09/HQ/W/016 kwa ajili ya jenereta ya megawati 100 itakayofungwa eneo la Ubungo, Dar es Salaam.

Lakini tangu zabuni hiyo ilipokamilika kupokewa nyaraka Juni mwaka huu, mchakato wa zabuni hiyo, vimedokeza vyanzo vya kuaminika, umekumbwa na mizengwe huku kukiwa na kampuni zinazoungwa mkono na wanamkakati walioipigia chepuo Richmond mwaka 2006.

Imeelezwa mbinu na mkakati uliotumika wakati wa kuipatia Richmond ndio zinazotumika sasa, huku mkakati mzito zaidi ukilenga kuwaingiza katika mtego viongozi wa sasa wa juu serikalini.

Mbinu hizo zimeelezwa ni pamoja na kuchukua taarifa za ndani ya zabuni na kuzipa kampuni zinazosimamiwa na watu wazito na kuifanya ishinde zabuni zote mbili.

<!-- /* Font Definitions */ @font-face {font-family:&quot;Lucida Sans Unicode&quot;; panose-1:2 11 6 2 3 5 4 2 2 4; mso-font-charset:0; mso-generic-font-family:swiss; mso-font-pitch:variable; mso-font-signature:-2147476737 14699 0 0 63 0;} /* Style Definitions */ p.MsoNormal, li.MsoNormal, div.MsoNormal {mso-style-parent:&quot;&quot;; margin:0in; margin-bottom:.0001pt; mso-pagination:none; mso-hyphenate:none; font-size:12.0pt; font-family:&quot;Times New Roman&quot;; mso-fareast-font-family:&quot;Lucida Sans Unicode&quot;; mso-fareast-language:#00FF;} @page Section1 {size:8.5in 11.0in; margin:56.7pt 56.7pt 56.7pt 56.7pt; mso-header-margin:.5in; mso-footer-margin:.5in; mso-paper-source:0;} div.Section1 {page:Section1; mso-footnote-position:beneath-text;} -->
TANESCO'S 160MW power projects: Bidders revealed

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

A total of eight foreign companies have submitted proposals to the Tanzania Electric Supply Company (TANESCO) for the construction of two power plants in Dar es Salaam and Mwanza regions with a combined capacity of generating 160 megawatts of electricity.

It is envisaged that once completed, the two plants will give a much-needed boost to the national power grid, and bring an end to rolling blackouts for the time being.

The companies bidding for the lucrative projects with a combined value of over $100 million (approx. 140bn/-) are from Canada, Norway, Finland, South Korea, China, Germany, and Egypt.

The two separate contracts involve the procurement of a 100MW, gas-fired power plant in Ubungo, Dar es Salaam, and the purchase of a 60MW power plant in Nyakato, Mwanza, which will run on heavy fuel oil.

The official deadline for submission of bids for the two tenders expired on June 5 this year, but it is understood that processing of the bids has been going on at TANESCO for the past six months now, under a cloud of mystery.

Sources familiar with the tenders say five companies submitted proposals for the construction and sale to TANESCO of the 100MW power plant in Dar es Salaam; Aaneen Power Cooperating of Canada, Jacobsen Elektro (Norway), Wartsila (Finland), Kolon & Samsung (South Korea), and China National (China).

China National apparently submitted the highest project cost proposal of $149.5 million (approx. 200bn/-), while Jacobsen Elektro proposed the second-highest project costs at 95,711,730 euros (approx. 193bn/-).

Aaneen Power Cooperating submitted a bid of 94.95 million euros (approx. 191.7bn/-), followed by Kolon & Samsung's bid of around 133bn/-. Wartsila's proposed project cost is 62.5 million euros (approx. 126bn/-)

On the other hand, according to the sources, four bidders submitted proposals for the 60MW power plant slated for Mwanza. They are Germany's MAN Diesel with a bid of 77.6 million euros (approx. 156.6bn/-); Wartsila again with 49.8 million euros (approx. 100bn/-); Egypt's UNATRAC with 67,681,467 euros (approx. 136.6bn/-); and Semco Maritime/Rolls Royce Marine of Norway with a bid of approximately 102bn/-.

The two contracts involve the supply, installation, testing and commissioning of emergency power plants in Dar es Salaam and Mwanza, both on what is known as a 'turn-key' basis.

This basically means that the project developer – in this case, the winning bidder(s) – will be entrusted with the task of setting up the plants and the selling or turning them over to a buyer - in this case, TANESCO - in a ready-to-use condition.

According to reports received by THISDAY, certain businessmen-cum-politicians implicated in the infamous Richmond power generation fiasco are now making decisive in-roads towards securing both of the latest energy contracts, but under a different company name.

Well-placed government officials have confirmed that the same people said to be behind the 2006 Richmond scandal, have succeeded in positioning themselves quite advantageously in the race to grab the Dar and Mwanza contracts.

With the entire tender process reportedly shrouded in secrecy and controversy, there are heavy indications of undue influence and interference being exerted by senior officials in the Ministry of Energy and Minerals and elsewhere in government - much like in the Richmond scandal.

It is understood that the group of Richmond-tainted businessmen-cum-politicians, working as a syndicate of sorts, submitted bids for the two contracts under another company name, ostensibly in an attempt to hide the identities of the real owners of the firm.

The Minister for Energy and Minerals, William Ngeleja, has told THISDAY that the TANESCO tender board was still assessing bids from various companies for the two projects, and insisted that the government has yet to award any of the tenders to any company.

Ends

.
 
Nini kinawazuia kuwataja wote walio-submit tenda na wale ambao tenda zao zimekubaliwa ? Wakati wa kufungua tenda vyote hivi vinasomwa wazi. Na wale ambao tenda zao zimekataliwa ziwekwe wazi. Hakuna haja ya siri.

Amandla.......
 
mzabuni ambaye Ngeleja alimtaka ameenguliwa. Hii kitu ni kama ile ya vitambulisho vya Taifa na Ngeleja hapa kawa kama Masha. Mwandishi ameripoti kama kasuku bila kuhoji kwa ndani.
Wizara haina mamlaka na zabuni ya taasisi iliyo chini yake katika mchakato na hawana mamlaka ya kuagiza zabuni kurudiwa isipokuwa PPRA.

Muhimu kujua mzabuni wa Ngeleja alikuwa nani?
 
Sources familiar with the tenders say five companies submitted proposals for the construction and sale to TANESCO of the 100MW power plant in Dar es Salaam; Aaneen Power Cooperating of Canada, Jacobsen Elektro (Norway), Wartsila (Finland), Kolon & Samsung (South Korea), and China National (China).

China National apparently submitted the highest project cost proposal of $149.5 million (approx. 200bn/-), while Jacobsen Elektro proposed the second-highest project costs at 95,711,730 euros (approx. 193bn/-).

Aaneen Power Cooperating submitted a bid of 94.95 million euros (approx. 191.7bn/-), followed by Kolon & Samsung's bid of around 133bn/-. Wartsila's proposed project cost is 62.5 million euros (approx. 126bn/-)

On the other hand, according to the sources, four bidders submitted proposals for the 60MW power plant slated for Mwanza. They are Germany's MAN Diesel with a bid of 77.6 million euros (approx. 156.6bn/-); Wartsila again with 49.8 million euros (approx. 100bn/-); Egypt's UNATRAC with 67,681,467 euros (approx. 136.6bn/-); and Semco Maritime/Rolls Royce Marine of Norway with a bid of approximately 102bn/-.

Hapo juu kuna kampuni ambayo Ngeleja kahongwa au kaahidiwa kuhongwa na imetupwa nje ya zabuni. Kuwarudisha wote ni mtindo aliotaka kutumia Masha kwenye Vitambulisho na waandishi wa habari wakashughulika vya kutosha akashindwa. Katika hili pia Vyombo vya habari makini kama Raiamwema vifuatilie ili kumzuia huyu bwana mdogo kuturudisha Richmond.

PPRA waulizwe kama uamuzi wa wizara ni sahihi?
 
Re-float tender, Tanesco told
16412.jpg
The minister of Energy and Minerals, Mr William Ngeleja, addresses reporters in Dar es Salaam yesterday on power tender issues. Right is his deputy Mr Adam Malima.By Tumsifu Sanga

The Government has ordered the Tanzania Electricity Supply Company (Tanesco), to re-float tenders for production of 100MW for Dar es Salaam and 60MW for mwanza.

The minister for Energy and Minerals, Mr William Ngeleja, told reporters in Dar es Salaam yesterday that the decision was reached after it was established that analysis done by Tanesco after receiving some tenders, were nor done properly.

He said after receiving the go ahead from the Government, Tanesco floated tenders for the production of 160MW and several companies applied.

However, he said, an analysis on the 60MW power plant for Mwanza, Tanesco overlooked a key aspect of running cost, which are huge and could impact on the implementation of the project if it is not included from the initial stages.

He said the Government has ordered Tanesco to contact those who had applied and were pre-qualified to present fresh data indicating their ability to purchase, install and maintain the generators.

"It has been established that analysis done by Tanesco experts did not look into all important aspects of the tenders," he said.

Mr Ngeleja said Tanesco was required to take into consideration the running cost for Mwanza generators whose capacity is to produce 60MW.

He said Tanesco was also supposed to verify that the bidder was capable of installing generators with life span of 30 years.

He said public utility firm had estimated to use $80 million for the 60MW plant and $120 million for the Dar es Salaam 100MW generators, making the total cost of the two generators $200 million or about Sh267 billion.

Mr Ngeleja told reporters that some 30 companies took documents for the Dar es Salaam tender and 28 others showed interest for the Mwanza power plant.

However, those who returned tender documents were five for Dar generators and four for the Mwanza plant.

Mr Ngeleja urged Tanesco to expedite the process and adhere to the 2004 Public Procurement Act.

He said the Government agreed to the two tenders early this year after Tanesco own analysis indicated that there was a need for 160MW to supplement the current power production.

kuna kitu hapa kinafichwa katika hii zabuni. Ama serikali inataka wachelewe ili kununua dowans maana miradi hii ilikuwa ni ya haraka kama tulivyoambiwa. Au kama nilivyosema awali kampuni yao imekosa.

Tittle kutokana na habar za nyuma za thisday na kulikoni iwe NGELEJA ALILIA RICHMOND yake.

Maana kusema imezimwa ni kana kwamba ngeleja ndio kazima wakati yeye ndio anataka mzabuni wake.

Hii ni Masha style
 
He said the Government has ordered Tanesco to contact those who had applied and were pre-qualified to present fresh data indicating their ability to purchase, install and maintain the generators.

"It has been established that analysis done by Tanesco experts did not look into all important aspects of the tenders," he said.

Mr Ngeleja said Tanesco was required to take into consideration the running cost for Mwanza generators whose capacity is to produce 60MW.

He said Tanesco was also supposed to verify that the bidder was capable of installing generators with life span of 30 years.

Swali ni kuwa kama vyote hivi vilikuwemo katika matakwa ya tenda. Na kama havikuweko, kwa nini havikuweko? Kwani ilikuwa tenda ya kununua vitunguu! Hatuwezi kuhamisha magoli katikati ya mechi.

Amandla.....
 
Swali ni kuwa kama vyote hivi vilikuwemo katika matakwa ya tenda. Na kama havikuweko, kwa nini havikuweko? Kwani ilikuwa tenda ya kununua vitunguu! Hatuwezi kuhamisha magoli katikati ya mechi.

Amandla.....

hapo sasa. na watanzania na hasa waandishi wanaandika walichoambiwa tu na ngeleja
 
Miongoni mwa makosa waliyotuhumiwa nayo Lowassa na Karamagi ni kuingilia utaratibu wa zabuni ya Tanesco.
Hivi ngeleja haoni kwamba anafuata mkondo uliowaondoa wenzie?
 
hapo sasa. na watanzania na hasa waandishi wanaandika walichoambiwa tu na ngeleja

Pamoja na kupinga kusogeza magoli katikati ya mechi lakini ni muhimu mwaliko wa tenda uangaliwe kama uliandaliwa kukidhi maslahi ya taifa letu. Maswali aliyouliza waziri ni ya muhimu lakini yalitakiwa kuulizwa kabla ya tenda kutangazwa. Na kama haikuwa hivyo basi tenda irudiwe.

Amandla........
 
Back
Top Bottom