Rich Mavoko kusaini Wasafi Classic Baby

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Staa wa Africa na Bongo flava, Diamond Platnumz ameendelea kuonyesha nia yake ya kuwasaidia wengine kukua kimuziki baada ya kufikia hatua kumsainisha Rich Mavoko kwenye lebo yake ya Wasafi.

“Rich Mavoko mara ya mwisho nilikuwa natakiwa nimsaini wasafi, Rich mavoko alitakiwa awe signed wasafi kabla ya nyimbo yake hii kutoka, ilitakiwa ikitaka awe chini ya wasafi, lakini kuna vitu vilichelewesha kwasababu kulikuwa na project namalizia kwanza,”

Diamond aliiambia Ayo Tv, “Nikamwambia, alikuwa anazungumza na uongozi wangu, kwahiyo wakamwambia kwasababu ishafika time unatakiwa utoe wimbo basi itoe tu hii nyimbo alafu then after hapo ikiwezekana kuanzia next project ndo anaweza akawa anatoa nyimbo akiwa chini ya wasafi.” Alielezea.

Hadi sasa waanii ambao wapo chini ya label hiyo ni pamoja na Harmonize na Raymond.
 
Ngoma Inogile! WCB imeanza kukua..

vokoooo.jpg

Msanii kiwango wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platnumz, ameeleza mpango wake wa kumsaini msanii mkali ambaye nyota yake imefifia kimtindo kiwandani, Rich Mavoko chini ya label yake ya Wasafi ‘WCB’..

Diamond amefunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanyiwa na boss wa brand ya AYO-TV ambaye pia ni straika wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Millard Ayo kama ifuatavyo;

“Rich mavoko mara ya mwisho nilikuwa natakiwa nimsaini wasafi.. Rich mavoko alitakiwa awe signed wasafi kabla ya nyimbo yake hii kutoka, ilitakiwa ikitoka awe chini ya wasafi, lakini kuna vitu vilichelewesha kwasababu kulikuwa na project namalizia kwanza,” Diamond aliiambia Ayo Tv.

“Nikamwambia, alikuwa anazungumza na uongozi wangu, kwahiyo wakamwambia kwasababu ishafika time unatakiwa utoe wimbo basi itoe tu hii nyimbo alafu then after hapo ikiwezekana kuanzia next project ndo anaweza akawa anatoa nyimbo akiwa chini ya wasafi.”Alielezea.

Hadi sasa wasanii ambao wapo chini ya label hiyo ni pamoja na Harmonize (Aiyola), na Raymond..

Habari imefika?!
 
Tusaidiane hivyo hivyo kueleweshana, wengine miziki tunajua kuisikiliza tu. Nini umuhimu au matokeo ya kusaini lebo fulani?
 
Tusaidiane hivyo hivyo kueleweshana, wengine miziki tunajua kuisikiliza tu. Nini umuhimu au matokeo ya kusaini lebo fulani?

Kusainiwa kwenye label haina tofauti na kusimamiwa kazi zako za muziki...

Usimamizi unaanzia kwenye ratiba ya kawaida ya msanii, utoe nyimbo ipi? umshirikishe nani? na itoke wakati upi? watasambaza vipi nyumbani hadi kimataifa? Shows upate vipi na kulipwa mtonyo upi wenye maslahi kwako? Na vingine vingi sema tu inatofautiana na jinsi wewe msanii na management mnamakubaliano yapi? na u serious wenu kwenye kuyatimiza...

Hii muhimu sana, kwamfano Diamond yupo zake bongo sasahivi huku anaendelea kupika ngoma fulani fulani, Mmoja wa manager wake karibia wiki mbili hivii hayupo Tanzania, kaenda Ulaya kwaajili ya kupiga promo tour ya diamond itayoanza march hadi april kwa zaidi ya nchi 7 zilizotangazwa mpaka sasa, huku wengine wakisukuma gurudumu bongo kusimamia mambo mengine ikiwemo ofisi za WCB n.k haya yote huwezi kufanya pekeyako msanii, lazima uwe na usimamizi

Kingine chukulia mfano wa Harmonize, hakuwa na wimbo uliochezwa hata redioni na mkwanja ilikuwa shida sana kusema arekodi audio na video... Ila usimamizi wa WCB umemfanyia yote hayo huku video ikiwa so kitoto hadi MTVBASE dogo anatisha, na kibindoni ana video mpya chini ya godfather, ana dancers wake binafsi, ana mpigapicha wake, n.k
 
Rich Mavoko namkubali sana huyu jamaa!

Ila sioni kama ni best move, nilitamani kungeibuka Management nyingine inayoweza kusimamia wasanii tukaona ushindani kwenye muziki.

Wasanii kama kina Belle9 mzee wa Masogange, Shetta, Ali Kiba, Abdu Kiba, Mr Blue, Steve R&B etc ni wasanii wakali sana tatizo ni management inayoweza kupambana kwenye soko la muziki.

Babu Tale na Mkubwa Fella wamekamata hili soko kiasi kwamba ni kazi kweli kushindana nao.
 
Kwa Tanzania yetu kupata management nzuri ni bahati ya mtende
 
Kwa Tanzania yetu kupata management nzuri ni bahati ya mtende

Sasa na Msanii kama Richie Mavoko kuwa chini ya WCB naona kama ni kuua kipaji, ataanza kuwekewa ratiba wakati alitakiwa awe kwenye label ambayo inamsikiliza zaidi ya anavyoisikiliza.

Kibongo bongo dogo yuko vizuri, ila ngoja tuone itakuwaje. Ninahisi pia atakuwa hawajafika bei ndo maana kaamua kurelease hiyo ngoma yake nje ya label. Ikihit atasikilizia kwanza ila ikibuma atajiunga na jamaa very fast.
 
Kimsingi hata mimi ningemshauri hivyo
 
Ila fitna za muziki wetu nazo ni katisha tamaa, watu wameshikilia industry vibaya mno.

Ngoja tuone itakuwaje.
Sio Bongo pekee, hata majuu ipo hiyo. Music industry ni moja kati ya sehemu ambayo ukiingia vibaya unaweza kunywa sumu. huwezi kuamini pale utakapo sikia mwanamziki kama Chris Brown analalamika kuwa anapigwa pini sna na wenye industry yai kias kwamba anaona kuwa haoni faida halisi ya miziki. Ni industry noma kwa unyonyaji.
 
Sheria taratibu na kanuni zinafanyiwa kazi sasa zitekelezwe kwa vitendo na si ubabaishaji kama mwanzo

Mkuu mimi sioni hili likifanikiwa, maana serikali yetu yenyewe haina vipaumbele. Ni watamkaji wazuri wa ilani na mikakati ila siyo watekelezaji. Kwa hiyo usishangae hili nalo likapita hivi hivi.
 
Mkuu mimi sioni hili likifanikiwa, maana serikali yetu yenyewe haina vipaumbele. Ni watamkaji wazuri wa ilani na mikakati ila siyo watekelezaji. Kwa hiyo usishangae hili nalo likapita hivi hivi.
Hapana Raimundo tusikate tamaa unajua huu mziki umeipaisha Tanzania na umekuwa sehemu ya ajira kwa vijana wetu
Tuzidi kuibana na kuipigia serikali kelele kwenye hili ipo siku (na si mbali sana)tutafanikiwa
 
Yaani mimi nikiwafikiria wasanii kama Late Ngwair, Daz Mwalimu, Ferouz, Mb Dogg etc naona kabisa muziki wetu hauko fair.

Kuna vipaji kibao vimepotea, vingi sana.
 
Yaani mimi nikiwafikiria wasanii kama Late Ngwair, Daz Mwalimu, Ferouz, Mb Dogg etc naona kabisa muziki wetu hauko fair.

Kuna vipaji kibao vimepotea, vingi sana.
Nipo Kampala jana nilikuwa Nairobi nyimbo za Ngwair RIP na Mb Doggy bado zinabamba huku lakini wenyewe maskini ukiacha Ngwair hawafaidiki na wamezima pengine moja kwa moja INAUMA
 
Back
Top Bottom