Rex Attorneys ni kashfa kubwa zaidi ya DOWANS

Hivi haiwezekani kwa TANESCO kushare hii hasara na hawa waliowaingiza mkenge? Au utaratibu ukoje unapoomba ushauri wa kitaalamu alfu huyo mtaalam mshauri akaamua kwa makusudi kukupotosha? hakuna liability yoyote kwa huyo consultant?
 
Naafikiri ukiajili mtaalamu alafu akashindwa kufanya kazi yake kitaalamu inabidi umwajibishe, Ila hili la tasnia ya sheria sijui linakwendaje
 
Kikwete jiuzulu hakuna namna hapa. Kama ingekungekuwa kweli kikwete hausiki lakini kikwete kahusika ikizingatiwa yeye ni mwenyekiti wa baraza la mawaziri. Kama kikwete ataendelea kutawala basi tanzania itaingia kwenye kaburi la sahau.
 
Hiv sisi watanzania tumekosa akil kwa kiasi kikubwa namna hyo! Mbona mim siamin kama sina akili, ila nkwamba sijui nfanye nn,ama km najua bas uwezo wa kufanya cna,ama cjui jins ya kuanza ama kuanzia. Ee Mungu tuondolee watawala (sio viongoz) wa ccm
 
Hivi kama Rex ndio walio washauri kuvunja mkataba si bora Tanesco wawashitaki ili professional indemnity insurance itumike kulipa hiyo fine

Umeongea point ya muhimu sana mkuu! umejitofautisha na wafuata mkumbo kwenye hii issue

Issue ya Dowans ilikosewa from first time, ili kujiokoa sio nguvu za kisiasa ni nguvu na ujanja wa kisheria unahitajika zaidi.

Deni hili likihamishiwa kwa REX attorney basi tumeula, ianze kesi mpya!!!

you have made my day
 
Waberoya, kabla hujafurahia zaidi. Subiri kidogo.

Kwa nini serikali ilirudi kwa mtu yuleyule aliyewashauri wavunje mkataba kumuomba ushauri kama walipe au
la?

Kwa nini aliyeshauri mkataba uvunjwe hakwenda ICC kuitetea serikali badala yake wanasheria wa Tanesco ndio walienda?

Je serikali itakuwa tayari kuwashtaki Rex Attorney kwa Professional Negligence? Sidhani. PM alishawasifia kwamba wamebobea. Bado serikali inawaamini ndio maana wameomba ushauri kwao karibuni tu kama walipe au la wakshauri serikali ilipe!!

Sasa unaweza kuendelea kufurahia kamanda: nisamehe kama nimeingilia furaha yako!
 
Sijapata bahati ya kuusoma ushauri wa Rex Attorney wala nakala ya Tuzo kuhusiana na kesi ya Dowans. Najihisi mgumu kwa sasa kutoa mchango wenye hitimisho katika nukta zote zilizojadiliwa.

Kwa upande mwingine sina tatizo sana na uwezo na uzoefu wa kampuni ya mawakili ya REX ATTORNEY katika anga za mikataba ya kimataifa na sheria za biashara za kimataifa kwa ujumla japo naelewa kwamba zipo kampuni nyingine chache za mawakili hapa nchini zenye sifa kama hiyo pungufu au zaidi.

Kwa mujibu wa mchokoza mada, msingi wa REX ATTORNEYS kuishauri serikali ivunje mkataba ni ukweli kwamba mkataba huo ulifanyika kwa kukiukwa sheria za nchi, hususani Sheria ya Ugavi (Public Procurement Act). Kwa maoni yao, kukiuka sheria za nchi kulifanya mkataba huo kuwa haramu kuanzia katika mizizi yake. Kwa kuwa mkataba wa ufahulishaji wa mkataba kutoka Richmund kwenda Dowans ulitokana na nguvu zilizopatikana katika mkatba haramu, kilichofutia nacho kilikuwa haramu, hiyo inaonekana kuwa hoja ya Rex Attorneys. Bila shaka hata katika utetezi wao walitumia hoja hiyo, pamoja na hoja nyingine, kuhalalisha kilichofanywa na serikali.

Kwamba mkataba ulikiuka sheria za nchi ni suala ambalo Mahakama ya Kimataifa, kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, ililibaini na kukubaliana nalo. Ubishi uliobaki katika hilo ni athari ya makosa hayo. Kwa mujibu wa mawakili wa Tanesco, athari ilikuwa ni kuufanya mkataba wote pamoja na vizazi vyake batili. Japo sheria sio hesabu kwamba moja kujumlisha moja lazima iwe mbili, hoja za mawakili wa TANESCO katika hili zilikuwa na nguvu. Tatizo ni kwamba waamuzi walikuwa na macho yao tofauti na ya mawakili wa Tanesco na waliona kwamba athari yake inawaangukia maafisa wa serikali waliohusika na kutoa tenda na sio Dowans.

Tatizo kubwa ni kwamba kwa mujibu wa makubaliano, pande zote mbili zilijifunga katika maamuzi ya waamuzi kwamba wasingeweza kukata rufani hata kama wasingeridhika na maamuzi. Kwa kufanya hivyo walibaki na mianya mitatu tu ya kuweza kupinga maamuzi hayo. Mosi, kama watathibitisha kwamba yalipatikana kwa rushwa au njia nyingine za udanganyifu na kama tuzo ilipatikana improperly. Yawezekana Rex Waliona hamna uwezekano wa kuweza kutumia mianya hii ya kisheria kupinga uamuzi.

Ningeomba kama kuna yoyote ana nakala ya Tuzo ya Mahakama ya Kimataifa atuwezeshe kuipata ili niweze kupata meno zaidi ya kuchangia.
 
Jamani kuna mtu anajua jinsi kampuni ilivohusika na uandaji wa sheria hii mpya ya madini lakini hata ile ya zamani? there are rumours that these guys were used by mining companies in influencing the formulation of mining laws?. I am told both donors, mining companies and the governemnt were using these guys to ensure that they influence the final product
 
Jamani mwenye data atusaidie, hii kampuni ililipwa na serikali kiasi gani cha pesa kwa kutoa ushauri wa kuvunja mkataba na hata sasa walipotoa ushauri wa kuwalipa Dowans.
 
Huyu Mwanaidi Majaar Senare ni yule Balozi wa Tanzania nchini Uingereza. Ni swahiba mkubwa sana wa JK, Rostam na Lowassa. Ana undugu kikabila na Lowassa. Ndiye leading partner wa Rex, yeye na mdogo wake Hawa Senare. Kampuni yao kupata kazi za serikali si jambo la kuuliza.

Wanafikiri wako smart saana, but there comes a day. A hell for them all.

Mungu wabariki maskini wa Tanzania.:Cry:
Ndege wafananao huruka pamoja
 
Hivi kama Rex ndio walio washauri kuvunja mkataba si bora Tanesco wawashitaki ili professional indemnity insurance itumike kulipa hiyo fine
Huyu mama leo katangaza eti kujiuzulu uananchama CCM utadhani alipoingia alitutangazia kuwa anajiunga na CCM au TANU,naona wengi wameshaanza kutimka CCM kwa kuhofia zama za Magufuli,hawa ndio wameiingiza mkenge Tanesco kwa undumila kuwili wa Dowans,chezea wengine si Magufuli naamini kwenye mipenyo ya fedha rahisi itafungwa MAKUFULI na Magufuli
 
Narudia tena wito wangu nilioutao kwenye mjadala wa Home Shopping Center, watoto wasienda shule waliogundua kuwa Rais Kikwete na viongozi wake ni wapumbavu na waroho wa kula mno midomo yao haifungi, mwizi mkubwa na adui namba moja wa taifa letu, wakakaa nao wakaazimwa nchi kwa miaka kumi, watoto wao wa miaka minne wakawa wanacheza kwenye mabega ya mkuu wa nchi, (imagine what udhalilishwaji wa mtu na ofisi namba moja ya nchi tajiri sana duniani). Kwa namna ile ile wanasheria wazalendo vijana wachanga tokeni fungueni kesi level A sisi tuko nyuma yenu twendeni mahakama kuu wakitupige tutaenda ya kimataifa tuangushe hili dudu mara moja, Jumuia ya Wafanya biashara wamefanya wamelitupa huko dudu linaitwa private sector association inayoongozwa na waajiriwa, leo wako wvijama karibu 5000 wenye nguvu watakaokwenda kufanya maajabu nchini hapa. wanasheria tokeni jamani tutengeneza historia hawa watu lazima wafungwe, donors wako upande wetu, mataifa makubwa yako upande wetu, let us move
 
Huyu mama leo katangaza eti kujiuzulu uananchama CCM utadhani alipoingia alitutangazia kuwa anajiunga na CCM au TANU,naona wengi wameshaanza kutimka CCM kwa kuhofia zama za Magufuli,hawa ndio wameiingiza mkenge Tanesco kwa undumila kuwili wa Dowans,chezea wengine si Magufuli naamini kwenye mipenyo ya fedha rahisi itafungwa MAKUFULI na Magufuli

Hivi kwanini hampendi kushughulisha akili zenu badala yake wengine wanafikiri kwa niaba yenu....Yaani MTU mwizi ahame CCM daah......kweli CCM imehasi akili za watu kiasi kwamba wamebakiwa nazakuvukia Barabara tu
 
Rekebisho kidogo, Dr. Hawa ndie mkubwa, Mwanaidi ni mdogo mtu.

Wajameni nawaombeni sana tujiangalie tujegeuka hate preachers. Ushauri wa kisheria 'legal opinion' ni professional job na inafuata kanuni za due diligency.

Dr. Sinare amenifundisha Investment Law pale UD, na kusema kweli, she was one of my inspirational, kwanza ana utu, ndiye mwalimu pekee kati ya miaka yangu 4 ya sheria pale UD ambaye somo lake, aligharimia kila kitu kwa fedha zake za mfukoni, huu ni utu wa zida.

Alikuja kufundisha, sio ili apate mshahara, (kwa pesa gani pale Ud), bali alijitolea tuu ili ku impart vast knowledge yake kwa wengine.
Ndie aliyenifungua macho kuhusu wanasheria corporate lawyers na hawa wa litigation nadhani ndio maana mpaka leo sisi wengine tumejikuta ni wazito sana kukanyaga mahakamani, degree ya sheria imeishia kabatini, huku tunaendelea kuchezea key board newsroom!.

Hata wanasheria mabingwa, kuna wakati wanashindwa kesi, na kuna washeria wa hovyo kabisa na wanashinda kesi.

Naamini Huyu Mama ni mmoja wa wanasheria vichwa funika bovu tulionao humu nchini.

Mkuu nakuunga mkono kwani pia huyu mama alinifundishia pia investment law Udsm, she is very bright
 
Tozo tumeishalipa.
P
 
Back
Top Bottom