Mdau
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,789
- 470
- Thread starter
- #61
Namfahamu vizuri sana mkuu...........
George hafanyi biashara ya drugs,namfahamu tangu udogo wake....Alianzia kwenye Udigala(ununuzi wa dhahabu) taratibu akawa anakua katika biashara yake hiyo kiasi cha kuanzisha kampuni yake ya Two Drums G&C Company ambayo inajihusisha na ununuaji wa madini.....Baadaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha wachimbaji wadogowadogo wa mkoa wa Mbeya(MBEREMA)...
Hayo mengine ni uzushi tu a.k.a MAJITAKA
Ndugu Balatanda,
Majina aliyokabidhiwa JK yalitoka mikoa yote nchini...Mwaikela jina lake lilikuwapo toka mkoani Mbeya..anayeweza kutudhibitishia usafi wake ni yeye mwenyewe, hakuna muuza unga au muovu anayejitaja kwa jina, ni wananchi ndio waliopiga kura na wanawajua watu wanaoishi nao...kama anadeal au ha-deal na drugs, wewe si wa kumuwakilisha humu, waliompigia kura ndio wenye haki..tusirukie neno MAJITAKA kama wanasiasa uchwara, tunaangalia FACTUAL situations, JK apeleke majina polisi/vyombo vya usalama watoe majibu ya mwisho...