Revealed: Kikwete hutuma watu kuhujumu wenzao

Status
Not open for further replies.
Wa kunyongwa nchi hii si yeye peke yake, wahujumu nchi hii ni wengi hawana idadi, nchi ilianza kufisidiwa na wananchi kuhujumiwa toka mwaka 1967 mpaka leo.. yani hata sijui watanzania wana roho ngumu kiasi gani!!!??

wapo watu leo wanaabudiwa na kusifiwa kwa mema walioitendea nchi hii huku ubaya wao ukigubikwa bila kuonewa haya.
Watanzania!!!

wapo waliotenda mema katika nchi hii, mazuri yao yalifunikwa na historia yao imepotea kwa sababu hawakuwa wenzetu!!
watanzania!!!

wapo waliofisidi kwa mlango mwingine na kisha wakawa wateule kwa mlango mwengine!!!
watanzania!!!

Hali hizo zimetufikisha kwenye ulemavu na utindio wa fikra, hatuwazi tunawaziwa, hatusemi tunasemewa, basi ikiwa kusoma hatujui basi hata mapicha yanatushinda kufahamu???

Iko siku itafika tutatambua kupembua mchele na pumba kwani sasa hatujui ni kipi tunakihitajia!!!

ndio maana kila jambo linakwenda msobemsobe kuanzia kwa raia mpaka mkuu wa kaya.
kwa maana hakuna anaeujua wajibu wake.

nimewafikishia ujumbe.

Rafiki uko chini ya anga hili? imekuwa siku nyingi pas kusikia wala kuona kutoka kwako

Nalifikiri labda usalama wa watifa wamekuficha kule kwenye gereza la siri au umewekwa chumba cha giza central police dsm!

Usichoke kuwaambia ukweli, usichoke kuwafanya wajitambue, usisite kuhimiza uzalendo wa nchi ambao ndio our priority number one!! Taifa kwanza !!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom