Hivi nyie watu, does it real matter mtu kuwa na degree ili awe kiongozi? Mbona tuna maprofessor kibao wamepewa nafasi wakafanya madudu kabisa? Si bora hata huyo Lukuvi ameonyesha kwa vitendo kwamba anao uwezo wa uongozi hata kama hana kisomo kikubwa?
Ndugu zangu kula sana kitabu hakuna uhusiano wowote na karama ya mtu katika uongozi. Tumpe nafasi, tupime ufanisi wake, then tulinganishe na shule yake.
Sasa Lukuvi anaangukia katika kundi gani hapo?Ni bora tukaongozwa na mtu ambaye tunajua hana viwango vya elimu lakini ana uwezo wa kuongoza badala ya kuongozwa na mdanganyifu wa elimu ilihali hajui kuongoza
mm sio mpanbe wa LUKUVI ila hii ndo info iliyo kwenye Mwananchi ya leo
Elimu: Stashahada ya Sayansi ya siasa, Urusi (Diploma in Political Science -USSR 1982 -1983 ), Cheti cha Ualimu, Cha Ualimu Tabora (1979) Chati cha Masuala ya Usalama, (Iringa Training in Defence and Security 1980)
sasa hii ya Washington International University - USA haikuonyeshwa
Inawezekana nao vyeti vya kughushi ndo maana hawawezi kumkamata mwenzao! In short hakuna wa kumfunga paka kengere! Ndo maana wanatumiwa hata kwenye shughuli nyingi za kihalifu kama kuiba kura... Lol poor My country TanzaniaMsanii, UWT ipo na tena ipo makini sana. Kwa kazi moja tuu,kuiba kura za wengine ili kuhakikisha waliopo madarakani hawaondoki hata kama wananchi hawawataki.
Hii ya sisi Watanzania kupenda sana kuona elimu za juu ndio inawafanya waheshimiwa wengi hata ku forge vyeti au kununua vyeti.
Elimu ni muhimu na inasaidia kwenye utendaji lakini sio the most important factor kwenye kuchapa kazi.
Si tumeona maprofesa wetu walivyochemsha kwenye wizara walizokuwa wanaongoza?
Nafikiri tuweke umuhimu mkubwa kwenye utendaji. Mrema alifanya kazi nzuri sana wakati hata hakuwa na degree. Tulivyoanza kutaka kulazimisha rais awe na degree Mrema akaamua kwenda kununua degree ya kwenye mitandao.
Yes elimu ni muhimu lakini kutokuwa na elimu kubwa sana sio kikwazo cha kufanya mtu ashindwe kufanya kazi za kuongoza nchi au kampuni.
Kama ushauri wa Usalama wa Taifa hauzingatiwi nini kinafuata??? ina maana anayeteua huliweka TAIFA hatarini ilihali UwT wameshamwambia kila detail ya anachotaka kukifanya.
Hii Usalama wa Taifa isiyo na meno inaboa sana. Kuna kitu kinapaswa kufanyika hapo ili iwe hai kama inavyotakiwa.
Viongozi wanawaburuza wananchi na kupumbaza dola isiwafanye kitu
Huyo Kikwete hana washauri, ichi chuo hatukijui wala kukitambua, jiuzulu haraka
Wote hawa wamefanyiwa "vetting" ya kutosha na bila shaka walipass.Halafu mniambie kuna usalama wa Taifa.