Rev. Mtikila yu wapi jamani?

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,259

Mzee wa mabomu, saa ya ukombozi ni sasa!
Mchungaji Mtikila anayesifika kutia magadi kwenye sabuni, mbona yu kimya sana sasa hivi?
Yu wapi?
 
GrEatThinkers,

Mtikila ni Mtanganyika wa kweli aliyeidai Katiba mpya wakati wengine tunakoroma usingizini na kumbeza.

Mtikila ni Mtanganyika aliyeshitukia Magabachori kuwa ni wezi wa kutupa, tukamuona hafai.

Mtikila ni Mtanganyika ambaye aliishaona tunapoona leo toka mwanzoni mwa miaka ya Tisini.

Mtikila ni Lulu, Fikilieni ni kitu gani ambacho leo tunakidai yeye hakukidai miaka hiyo.

:ranger:Shukrani Rev.Mtikila kwa Uzalendo na Utanganyika wako.:ranger:
 
Ameachana na siasa?

Siasa zake amehamishia ukumbi wa habari maelezo na mahakamani, in simple way you can say Mtikila is no longer exsist. mbaya zaidi alichukuwa sh million 10 kwa rostam Aziz, na rostam akathibitisha mbele ya media petty cash vocha aliyosaini Mtikila. amepoteza public sypathy,
 
Baada ya kuumbuliwa RA kwa kuonyeshwa petty cash voucher ya kuvuta kitu kidogo, amenywea! Kwani aliambiwa hiyo ni moja tu, ukianza firimbi zako tena, tutaweka zingine mbaya zaidi! akaona maji yamemzidi kimo bora aufyate!
 
Na ishu ya kutumiwa na CCM kuipakazia Chadema kuhusu kifo cha Chacha Wangwe ndiyo ilikuwa kaburi lake, hatunaye tena kwenye mapambano. Kifupi ni kuwa aliuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kama ilivyokuwa kwa Esau katika Biblia.
 
Mtikila ni mmoja kati ya watanganyika walio lilia mali zetu zisiibiwe tangu zamani,

Leo hii upo unabung'aa na kurubunika kwa visenti vya magabachori shauri yako.

Kama na wewe ni Gabachori fisadi fahamu siku zako zinahesabika.

Japo mlikuwa mnampoza,mlikuwa mnampatia nauli za kufika mikoani na kuutalifu umma.

Amefanya kazi kubwa, hatuwezi kumtupa kihivyo.
 
Hapo ndipo alichemka kwa kweli.

mwacheni apumzike, hatumhitaji kazi aliyofanya tunijua IN & OUT
 
Mtikila ni mmoja kati ya watanganyika walio lilia mali zetu zisiibiwe tangu zamani,

Leo hii upo unabung'aa na kurubunika kwa visenti vya magabachori shauri yako.

Kama na wewe ni Gabachori fisadi fahamu siku zako zinahesabika.

Japo mlikuwa mnampoza,mlikuwa mnampatia nauli za kufika mikoani na kuutalifu umma.

Amefanya kazi kubwa, hatuwezi kumtupa kihivyo.

Mkuu spencer, pamoja kwamba mimi sipendi wala kukubaliana na Dar es salaam katia mlengo wake, ila kwenye hili tumtendee haki, alichopost ndio ukweli wenyewe,uwezi kumuita mtu fisadi halafu wewe huyohuyo unatokea mlango wa nyuma unakwenda kuchukuwa pesa kwa mtu huyo huyo, hapana siwezi kumsapoti mtu wa namna hiyo. kuhusu watu waliosimama front kupigania nchi wako wengi na kila zama na kitabu chake, kuna watu tangu wazaliwe hawajawahi kuwa wanachama wa ccm, kwahiyo sometime think Big, first appointment ya kwanza ya ajila ya mtikila ni ikulu enzi za mwalimu, sitaki kujaza ukarasa nitawachosha wasomaji. lakini mtikila kwishnei.
 
Yuko busy anadraft katiba mpya soon ataisambaza kuwapunguzia kazi wa TZ.
 
Mzee wa mabomu, saa ya ukombozi ni sasa!
Mchungaji Mtikila anayesifika kutia magadi kwenye sabuni, mbona yu kimya sana sasa hivi?
Yu wapi?

MKuu umesahau mshindo wa kimya kirefu?
Huyu Rev. Mtikila ataibukia mahakamani na kesi lukuki, si mnamjua na hiki kimya anaandaa documents
 
Mkuu spencer, pamoja kwamba mimi sipendi wala kukubaliana na Dar es salaam katia mlengo wake, ila kwenye hili tumtendee haki, alichopost ndio ukweli wenyewe,uwezi kumuita mtu fisadi halafu wewe huyohuyo unatokea mlango wa nyuma unakwenda kuchukuwa pesa kwa mtu huyo huyo, hapana siwezi kumsapoti mtu wa namna hiyo. kuhusu watu waliosimama front kupigania nchi wako wengi na kila zama na kitabu chake, kuna watu tangu wazaliwe hawajawahi kuwa wanachama wa ccm, kwahiyo sometime think Big, first appointment ya kwanza ya ajila ya mtikila ni ikulu enzi za mwalimu, sitaki kujaza ukarasa nitawachosha wasomaji. lakini mtikila kwishnei.

Hizi ndio siasa za wanasiasa wengi.
Mchana majukwaani wanawaponda mafisadi, usiku wanaenda kubembelezea pochi!!
 
Wana JF Bado nitamtetea Mtikila.

Namtetea kwa yale mema aliyoyafanya kwa nchi hii, kuthubutu kukatiza katika Msitu wa Mnene.

Jasho likimtoka kutaka kuamsha watunzania waliokunywa maji ya bendera,

Enzi hizo, hata mimi nilikuwa Siipati picha sawa sawa pale alipokuwa anambana Rajan,

Lakini leo namuenzi, inawezekana Hiyo Cheque walipeleka kama sadaka kanisani kwake wakti wa Harambee,

Hata kama hapo alitereza, Ametufanyia mema mengi watanzania kuliko kupokea Checque na bado akaendelea kutuamsha.:ranger:
 
Uko sahihi kabisa hata Rostam Aziz ameajili watanzania wenzetu wengi sana kwahiyo tumthamini mana tukimtia lupango watanzania wenzetu watateseka, verry good.
 
Inaonekana kweli una Lisence ya kuua maskini.

Naona Avatar yako jinsi mnavyowarubuni maskini na kuwekeza kwa umaskini wao.

Hawajaamka tu lakini nenda kule Meatu ukaweke hilo li picha la Mtalii.

Kule wameamka, Operation Sangara imefanya kazi kubwa.

Inakuja Operation Katiba mpya, Januari hii isikilizie kama hutabaki wewe maana hata dodoma itafika.

Vitabu vyenye heshima yake vimeandika:

"Karibisha mgeni nyumbani kwako lakini usikubali akutawale"

Tumetenda dhambi kubwa kuiacha Nchi na Rasilimari zetu mikononi mwao.

Usiwe MS namba 2.
 
Wana JF Bado nitamtetea Mtikila.

Namtetea kwa yale mema aliyoyafanya kwa nchi hii, kuthubutu kukatiza katika Msitu wa Mnene.

Jasho likimtoka kutaka kuamsha watunzania waliokunywa maji ya bendera,

Enzi hizo, hata mimi nilikuwa Siipati picha sawa sawa pale alipokuwa anambana Rajan,

Lakini leo namuenzi, inawezekana Hiyo Cheque walipeleka kama sadaka kanisani kwake wakti wa Harambee,

Hata kama hapo alitereza, Ametufanyia mema mengi watanzania kuliko kupokea Checque na bado akaendelea kutuamsha.:ranger:

Huyu jamaa alianza kuongelea katiba mpya, na kudiriki kulipeleka swala hili mahakama kuu kabla wengi wetu hakujapambazuka.
Sijui kama yeye vile vile ni mwanaJF lakini he is a Great Thinker.
 
Mzee wa mabomu, saa ya ukombozi ni sasa!
Mchungaji Mtikila anayesifika kutia magadi kwenye sabuni, mbona yu kimya sana sasa hivi?
Yu wapi?

Amekaa kimya kama alivyokaa kimya Slaaa, kwani wote hao ni viongozi ambao walihubiri siasa za udini. Na mara nyingi huwa hawadumu kwenye siasa viongozi wa aina hiyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom