Retrechment ya ndoa;kuwe na mafao yake!!!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,138
Jamani kuna ndoa za ajabu ajabu watu wanaoana siku mbili wanaachana wengine miezi miwili wanaachana kwa ujumla hakuna tofauti na retrechment ya makazini.....
sasa basi nikaona vyema kama retreachment za makazini zinatolewa mafao vivyo hivyo inabidi yule anaemwacha mwenzake kuwepo na makubaliano ya mafao kwa yule anaeachwa...vinginevyo kutakuwa na kuachana kama mbwa kila siku...je mafao yanaweza kupunguza ongezeko la kuvunjika kwa NDOA??
 
Kwa Tanzania sheria inasema kile mlicho chuma mkiwa pamoja ndo kinagawanywa sawa kwa sawa kama hamna watoto, lakini kama mna watoto yule anayekaa/kutunza watoto ndo anapewa robo tatu ya mali. Hii inamaanisha watoto nusu ya mali, baba robo na mama robo.

Na hii haiangalii nani anazalisha zaidi ilimradi tu mali hizo mmezipata mkiwa pamoja. Nadhani wanaoachana baada ya miezi hawastahili hata kuwa na kesi yoyote kwa sababu kila mtu anaweza kuondoka na alichokuja nacho. Ikiwa mmoja atamkataa mwenziwe basi asidai chochote, na yule anayekataliwa ana haki ya kushitaki ili alipwe fidia na yule anaye mkataa, na sheria zipo (za madai)
 
Nadhani kuachana huku kunasababishwa na kukosa subra. Maana katika process za group (couple) formation inachukua hadi a year sometime kwa watu kuelewana na kuamua kuwa pamoja. Vijana wanashindwa kuvumilia kipindi cha mwanzo ambacho wakati katika baadhi ya ndoa huwa rahisi na nyingine huwa ni kipindi kigumu.
Hata hivyo, cha msingi kisiwe namna watakavyogawana bora wafikirie namna watakavyoimarisha ndoa yao. Ikitokea basi ni sheria ti zinazowasimamia zifuatwe ila kuita retranchment benefits, Mh!!!
 
Back
Top Bottom