Rest In Peace Prof Leonard Shayo

RIP Prof Shayo jamaa alikuwa ana nia thabiti ya kuitumikia nchi urasimu na ubinafsi wa viongozi wetu vikamfrustrate. Jamaa alikuwa na akili ya aina yake.
 
When someone mentions the name Prof. Shayo.......one quick memory clicks in my medula oblingata and this is his ''Advanced Mathematics Book'' which we referred to it several times at high school! We will miss this talent!

RIP Prof. Shayo
 
Poleni sana mungu watienguvu,ila imeshatolewa kwenye matangazo na watu walishaanza kutoa rambirambi kabla ya uhakika ,,tunashukuru kwa kutuhakkikishia!!!
Innalilah rajuuuune
 
Mods I suggest this thread is combined with another one with same information ''RIP Prof. Shayo)........!

Cheers
 
NA SAID NJUKI, ARUSHA

MWANASIASA na msomi aliyegombea urais wa Tanzania mwaka 2005, Profesa Leonard Shayo, amefariki dunia.

Profesa Shayo ambaye pia alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Hisabati katika wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, alifariki dunia jana saa 5.30 mchana katika hospitali ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Profesa Shayo ambaye alikuwa mmoja wa wataalamu wachache wa Hisabati na Sayansi pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia Makini (MAKINI) ambacho kilimsimamisha kugombea urais mwaka huo.

Kwa mujibu wa mdogo wake, Bwana Habibu Mandari, Profesa alilazwa Ijumaa iliyopita baada ya kuzidiwa akiwa mjini hapa kikazi.

"Profesa aliugua ghafla na alipopelekwa hospitalini, waligundua kuwa na shinikizo la damu, kisukari na homa ya mapafu. Walifanikiwa kuishusha sukari lakini Mwenyezi Mungu aliamua kumchukua," alisema Bwana Habibu.

Alisema mwili wake umehifadhiwa kwenye mochari ya hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, kabla ya kusafirishwa kwenda nyumbani kwake Sinza, Dar es Salaam kwa ajili ya mipango ya mazishi.

Profesa Shayo katika kampeni za urais mwaka 2005 alikuwa kivutio kikubwa kwa wapiga kura, kwani tofauti na wagombea wengine, yeye aliendesha kampeni akitumia gari dogo na kipaza sauti bila wapambe.

Katika uchaguzi huo, mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, alishinda kwa kuzoa kura zaidi ya milioni tisa kati ya 10,590,016 zilizopigwa, huku marehemu Shayo akiambulia kura 17,O33.

Wengine ni Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF aliyepata 1,317,220, Bwana Freeman Mbowe wa CHADEMA aliyepata kura 671,780, Bwana Augustino Mrema wa TLP kura 84,131, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP (39,990), Bwana Edmund Mvungi wa NCCR-Mageuzi(56,423).

Wagombea wengine walikuwa ni mwanamke pekee Bibi Anna Senkoro wa PPT Maendeleo (18,741), Bwana Paul Kyara wa SAU (16,380) na Dkt. Emmanuel Makaidi wa NLD (21,525).

Marehemu Shayo alizaliwa katika kijiji cha Mamba Kotela na kukulia Rombo mkoani Kilimanjaro. Ameacha mjane na watoto wanne, watatu wakiwa ni wa kike.

Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikowahi kufanyakazi marehemu, Profesa Rwekaza Mukandala, alishitushwa na kifo hicho na kumwombea marehemu alazwe mahali pema peponi na kuahidi kutoa taarifa baadaye kupitia kwa wasaidizi wake kwani hakuwa amepata taarifa kuhusu kifo hicho.
 
Huyu mtu alikuwa akifikiri tofauti nawengine,na hauwezi kulijua hilo mpaka umesoma makala zake.Kwa kweli alikuwa ni mtu katika watu na kichwa katika vichwa.
Mungu ampumzishe kwa amani
 
Mimi iwa nachukizwa sana na tabia ya binadamu kumwaga sifa kemkem kwa marehemu.
Alipo kuwa hai hizo sifa mlikuwa hamzioni???Mbona mlikuwa hamwagi sifa hizo?Kesha rudi kwa mola mnamwaga sifaa kibao hii ni nini sasa?Unafiki au nini?Mtu mpeni sifa zake akiwa hai msisubili mola kesha mchukua mnaanza ooh alikuwa mchapa kazi sifa kibaoo.
Pumnzika kwa Amani babu yangu Shayo.Amen.
 
r.i.p prof shayo...huyu ni kati ya watanzania waliokuwa na akili sana na muumini wa kweli wa ujamaa...alikuwa rafiki na mfuasi mkubwa wa philosophy za mwalimu,naye pia alikuwa na philosophy zake[someni makala zake mwananchi zinabeba ujumbe yeye ni nani na anatetea nini...,alikuwa mtunzi mahiri wa sera vile vile,hakuwa muumini wa mali]

idea ya kuwa na kijiji cha sayansi na teknelojia ilikuwa ya mwalimu...na prof shayo alikuwa archtect wa ule mradi......aliweka kila kitu..na kuweka mikakati...

lengo la mradi wa kijiji cha sayansi na teknelojia ilikuwa kuchukuwa watoto wenye vipaji maalum tanzania na kote afrika [duniani]...na kuwalea tangu wanakuwa wadogo...katika mazingira ya kisomi...hadi chuo kikuu .nadhani mwalimu alikuwa anaota kuwa na vijana wanaoweza kuja kubuni NASA tanzania au hata kuajiriwa huko.

mradi ule ulikufa na mwalimu...mkienda pale tume ya sayanzi...na wizarani..wamebaki na maandishi ya prof shayo ,ramani etc....

cha kushangaza south africa wamekuja na idea kama ya mwalimu na prof shayo na inakata mbuga...na tayari wamepewa eneo arusha wajenge tawi...kitaitwa NELSON MANDELA ..ACADEMY....

HUYU MUHASHIMIWA ALIKUWA MWANASAYANSI..LAKINI PIA ALIKUWA NA AKILI ZA ZIADA ALIZOAMUA AZITUMIE KUAMCHA WATANZANIA ........SIASA ALIKUWA ANAFANYIA WITO AU HOBBY!!

Ile idea ya Kiki cha Sayansi ilikuwa Bab kubwa!
Baada ya msiba wa Baba wa Taifa nilipata kumuuliza swali kuhusu huu mradi maana nilipata kuwa mwanafunzi wake wa Hisabati Udsm.. akanijibu kwa masikitiko.. Sijui kwa kweli, labda nikiwa Rais!
Tanzania imepoteza kichwa cha maana sana!
 
Apumzike kwa amani. Nakumbuka vile vitabu vya hesabu vya A-Level tuliosoma Advanced Mathematics tutavikumbuka sana, vilianzia kwenye huo mradi wa IVST.
 
Kwangu mimi nina m-rate kama the most professor wa sayansi na hisabati aliyefanya vitu adimu, may be is the only one to date

KAMA KUNA PROFESSOR MWINGINE WA SAYANSI NA HISABATI ALIYEFIKIA RANK YA KUFANYA ALIYOYAFANYA SHAYO AJITOKEZE AU NIELEZWE!
 
Mwenyezi Mungu aliyemuumba Prof. Leonard Shayo hatimaye imempendeza amemrudisha kwake.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina la Bwana libarikiwe. Amen

Poleni wafiwa, hasa mke na watoto na wanafamilia wote.
 
Waberoya said:
Kwangu mimi nina m-rate kama the most professor wa sayansi na hisabati aliyefanya vitu adimu, may be is the only one to date

KAMA KUNA PROFESSOR MWINGINE WA SAYANSI NA HISABATI ALIYEFIKIA RANK YA KUFANYA ALIYOYAFANYA SHAYO AJITOKEZE AU NIELEZWE!

Waberoya,

..labda kwanza ungetuelimisha kuhusu mchango wa Prof.Leonard Shayo.

..binafsi nimefurahi kusikia kwamba aliandika kitabu cha hesabu kwa ajili ya vijana wa high-school.

..namuweka ktk kundi moja na wana hisabati na waandishi wa hisabati kama Michael Kinunda, Mishael Muze, Geofrey Mmari...
 
..nani anaweza kuweka link ya makala ya mwisho ya marehemu kwenye gazeti la mwananchi,ilikuwa inasema....JE,MALUMBANO YA KUJIUNGA NA OIC NI LAZIMA?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom