Request: Sua Graduate Entrepreneurs Success Stories

Developer

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
446
503
Dear SUA Graduate business owners,

I hope this message finds you well.
I am a founder of what we call Sokoine University Graduate Entrepreneurs Cooperative Society LTD (SUGECO). This organization was formed with assistance of Department of Agricultural Economics and Agribusiness, in the Faculty of Agriculture, SUA. The main objective of this organization is basically to organize and assist SUA graduates to take up the business opportunities in the country – start businesses to employ themselves and create jobs for others. Your company is doing that. This is an invitation to join SUGECO. Detail about membership is in the brochure. At the moment the organization is based at DAEA as a promoter and I am interim chair.
Most Important: SUGECO needs your help!

We have applied for a grant to help us startup business incubators and have endowment funds to backup loans that we will get from CRDB. There are good prospect that if we provide needed information we will get this grant. The organization requires us to provide success stories of SUA graduate who have invested in Agriculture/agribusiness and succeeded. Your company is one of them. I believe you will like to help your young brothers and sisters to get this help. If so, I am hereby request you to share will us a one-page narrative of your successes so that we can submit this for our grant application. If there is anyway you can show where SUA helped e.g. consultation with SUA members even for encouragement, or technology etc it will be very helpful. Unfortunately we need this information ASAP. Sorry for short notice – but I believe you already have it somewhere in your archives. Kindly provide us with the following information to assist us communicate success stories to our prospective donors.

The outline:
1. Name of company
2. History of the company include description of the business (business profile)
3. Status of the company now
4. Future plans
5. Challenges you faced after graduation and who facilitated your establishment and what role SUA played or could have played to
make things easier for you
6. What role can SUGECO play for: a. New graduates who aspire to start own businesses b. Existing graduate businesses like yourself

Thanks in advance

This request is from:

Dr Anna A Temu​

Department of Agricultural Economics and Agribusiness​

P. O. BOX 3007, Morogoro, Tanzania​

Attachments

  • sugeco Brochure final july11.pdf
    168.1 KB · Views: 335
Waliochangamkia hi fursa waje watupe mrejesho
Dear SUA Graduate business owners,

I hope this message finds you well.
I am a founder of what we call Sokoine University Graduate Entrepreneurs Cooperative Society LTD (SUGECO). This organization was formed with assistance of Department of Agricultural Economics and Agribusiness, in the Faculty of Agriculture, SUA. The main objective of this organization is basically to organize and assist SUA graduates to take up the business opportunities in the country start businesses to employ themselves and create jobs for others. Your company is doing that. This is an invitation to join SUGECO. Detail about membership is in the brochure. At the moment the organization is based at DAEA as a promoter and I am interim chair.
Most Important: SUGECO needs your help!

We have applied for a grant to help us startup business incubators and have endowment funds to backup loans that we will get from CRDB. There are good prospect that if we provide needed information we will get this grant. The organization requires us to provide success stories of SUA graduate who have invested in Agriculture/agribusiness and succeeded. Your company is one of them. I believe you will like to help your young brothers and sisters to get this help. If so, I am hereby request you to share will us a one-page narrative of your successes so that we can submit this for our grant application. If there is anyway you can show where SUA helped e.g. consultation with SUA members even for encouragement, or technology etc it will be very helpful. Unfortunately we need this information ASAP. Sorry for short notice but I believe you already have it somewhere in your archives. Kindly provide us with the following information to assist us communicate success stories to our prospective donors.

The outline:
1. Name of company
2. History of the company include description of the business (business profile)
3. Status of the company now
4. Future plans
5. Challenges you faced after graduation and who facilitated your establishment and what role SUA played or could have played to
make things easier for you
6. What role can SUGECO play for: a. New graduates who aspire to start own businesses b. Existing graduate businesses like yourself

Thanks in advance

This request is from:

Dr Anna A Temu

Department of Agricultural Economics and Agribusiness

P. O. BOX 3007, Morogoro, Tanzania​

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawakumbuka wale walioenda kuanzisha kitu kama hii kule Igunga wakatapeliwa na DC ambaye sasa ivi ni mbunge! Yaani kundi la graduates mnamtumia DC kuwatafutia masoko?
 
Oooh Haki ya nanii sihami Tanzania
Yaani nyie SUGECO SUGECO mtabaki kuwa juu mawinguni

Kama hao enterpreneurs mlikuwa mnawaandaa nyie tokea miaka Hiyo........ na mnawapatia mitaji ya fedha na consultations.....leo hii mnakuja na bla blaaa sijui I hope such documents is already in your achieves we need it ASAP.

mnamaanisha nini kwa jamii? kwamba nyie Kama viongozi Wenye dhamana hamna data za wajasiriamali mliowatengeneza na kuwanoa kwa kodi zetu? Kama kweli ndio ukweli huo kwa dunia ya jana na leo hamfai kupata izo funds.

Bora wapewe TBC1 wafanye iyo kazi Juzi tu mwezi wa 2/2019 niliona kuna dada amemaliza BVM Sokoine kapewa mtaji na shirika fulani na alianzia huko kwenu SUGECO leo hii ana mbuzi zaidi ya 200 anapatikana kibaha, ndoto zake ni kuja kumiliki kiwanda cha nyama sijui nini na ranch. ......kuna giant mwingine 2013 kwa sasa ni young millionaire huko kaajiri na kujiajiri anamilki viwanda vidogo vidogo mlimpaa mtaji sijui ndio mkopo kwanza hujaeleweka vizuri kwa sababu ya ASAP amewekeza zaidi mpanda na singida ndani ndani uko sijui wapi......

hizi taarifa na misifa ya SUGECO na SOKOINE sijui Apopo na mapanya yakutegua mabomu na kudetect kifua kikuu naonaga kwenye vyombo vya Habari hasa TBC1 mtu akija kwenye makarabrasha yenu mnajinadi mmetoa waajiri wa agribusiness kadhaa tokea ianzishwe kumbe kiuhalisia msaada wenu kwa hao graduates upo zaidi kwenye makaratasi ndio maana mnashindwa kuzalisha graduates wa kutatua matatizo na changamoto za Jamii mnaishia kuzalisha wategemezi kwenye Jamii daily kuzunguka na bahasha wakati ana bachelor ya agribusiness

taarifa unazozihitaji zilipaswa kuwa kwenye achieves zenu pia ungepaswa utueleze ni kwa namna gani SUGECO imechangia kuinua pato la nchi? labda tokea muwepo mpaka leo mmetengeneza graduates wangapi Wenye kumiliki viwanda hapa nchini? SUGECO imetatua tatizo la ajira kwa asilimia ngapi mpaka sasa?

graduates siku hizi wanafanya forex Business ambayo inatengeneza maskini wengi Wenye majina makubwa na matajiri wachache wa kufikirika...... watu wanatafsiri charts utazani wana Phd za statistics SELL OR Get SOLD

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUMEZOEA MAJUNGU NA FITINA

Watu wamezoea kuishi kwa majungu na fitina. Naomba niwaambie kitu kimoja. Document hii haijaandikwa na mtu wa SUGECO. Imeandikwa na watu tu wenye nia mbaya na SUGECO, watu waliyozidiwa akili ambao wanatamani kuiona SUGECO ikichafuka na kupoteza haiba yake kwa umma wa Watanzania waliyoiamini kwa kazi kubwa wanayoifanya katika jamii. Kwa wanaoijua vizuri SUGECO hawawezi kukubaliana na uzushi huu. Kiukweli watu wa SUGECO ninaowajua mimi wako smart na wanajua wanachokifanya. Siyo watu wa kubabaisha kwenye mambo yao. Sema tu mambo mambo yao mengi wanayoyafanya hawayatangazi. Ni taasisi inayoongoza kwa kutoa mafunzo ya vitendo kwa vijana. Mafunzo ambayo yamekuwa nguzo muhimu.

Ukitaka kuamini SUGECO haiko kama baadhi wanavyotaka kuaminisha watu, nenda pale Mkongo wilayani RUFIJI kwenye Kambi ya Kilimo ya Vijana kwenye Majengo ya Rubada, sasa hivi kuna mafunzo ya ufugaji bora wa kuku, mafunzo ya Uzalishaji wa mbogamboga, mafunzo ya uanzishwa wa miradi na kuisimamia, na mambo mengine mengi yanaendelea kwenye kambi hiyo. Watu wa Rufiji, kibiti, ikiwriri na mkongo yenyewe ni mashahidi wa hili. Kama huamini nenda au tuma hata mtu akajionee kwa macho yake na mwisho atakuja kuwa balozi mzuri kwa wengine.

Katika mafunzo haya, Graduates nao wamepewa umuhimu wa kipekee. Wamekuwa wakifundishwa na wakitoka hapo wanapata mwamko na akili mpya ya kujitegemea badala ya kuendelea kulalamika juu ya ukosefu wa ajira.

Tatizo letu Watanzania tunaendekeza fitina na majungu yasiyokuwa na maana wala kichwa na ndiyo maana wengi wetu tunashindwa kufika tunakokutaka. Yaani tukimwona mtu kafanikiwa utajiribu kila namna umshushe.

Tafuteni taarifa sahihi za SUGECO Msije na taarifa hizo za kupikwa. Kuna watu wanawashangaa.

Hebu fikiria SUGECO ndiyo waliyoanzisha program ya kuwapeleka vijana Graduates kujifunza Kilimo kwa vitendo Israel. Hadi sasa jumla ya vijana 120 wahitimu wa vyuo vikuu wamekwisha kuenda huko na kuweza kurudi wakiwa na ujuzi tele wa teknologia mbalimbali za kilimo na wengine 45 bado wskiwa nchini Israel wakiendelea na mafunzo. Na sasa hivi serikali kwa kuuona kuwa ni mpango mzuri na wenye manufaa makubwa kwa vijana na hasa wahitimu wa vyuo, wameamua kuwaunga na kwamba kwa kwasasa mpango huu unaratibiwa kwa pamoja kati ya wizara ya kilimo, SUGECO pamoja na Serikali ya Israel.

Na hii ndiyo SUGECO
 
Oooh Haki ya nanii sihami Tanzania
Yaani nyie SUGECO SUGECO mtabaki kuwa juu mawinguni

Kama hao enterpreneurs mlikuwa mnawaandaa nyie tokea miaka Hiyo........ na mnawapatia mitaji ya fedha na consultations.....leo hii mnakuja na bla blaaa sijui I hope such documents is already in your achieves we need it ASAP.

mnamaanisha nini kwa jamii? kwamba nyie Kama viongozi Wenye dhamana hamna data za wajasiriamali mliowatengeneza na kuwanoa kwa kodi zetu? Kama kweli ndio ukweli huo kwa dunia ya jana na leo hamfai kupata izo funds.

Bora wapewe TBC1 wafanye iyo kazi Juzi tu mwezi wa 2/2019 niliona kuna dada amemaliza BVM Sokoine kapewa mtaji na shirika fulani na alianzia huko kwenu SUGECO leo hii ana mbuzi zaidi ya 200 anapatikana kibaha, ndoto zake ni kuja kumiliki kiwanda cha nyama sijui nini na ranch. ......kuna giant mwingine 2013 kwa sasa ni young millionaire huko kaajiri na kujiajiri anamilki viwanda vidogo vidogo mlimpaa mtaji sijui ndio mkopo kwanza hujaeleweka vizuri kwa sababu ya ASAP amewekeza zaidi mpanda na singida ndani ndani uko sijui wapi......

hizi taarifa na misifa ya SUGECO na SOKOINE sijui Apopo na mapanya yakutegua mabomu na kudetect kifua kikuu naonaga kwenye vyombo vya Habari hasa TBC1 mtu akija kwenye makarabrasha yenu mnajinadi mmetoa waajiri wa agribusiness kadhaa tokea ianzishwe kumbe kiuhalisia msaada wenu kwa hao graduates upo zaidi kwenye makaratasi ndio maana mnashindwa kuzalisha graduates wa kutatua matatizo na changamoto za Jamii mnaishia kuzalisha wategemezi kwenye Jamii daily kuzunguka na bahasha wakati ana bachelor ya agribusiness

taarifa unazozihitaji zilipaswa kuwa kwenye achieves zenu pia ungepaswa utueleze ni kwa namna gani SUGECO imechangia kuinua pato la nchi? labda tokea muwepo mpaka leo mmetengeneza graduates wangapi Wenye kumiliki viwanda hapa nchini? SUGECO imetatua tatizo la ajira kwa asilimia ngapi mpaka sasa?

graduates siku hizi wanafanya forex Business ambayo inatengeneza maskini wengi Wenye majina makubwa na matajiri wachache wa kufikirika...... watu wanatafsiri charts utazani wana Phd za statistics SELL OR Get SOLD

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu umeandika kwa mihemko sana, hamna hoja, unakurupuka tu sijui unataka kuzungumzia nini....
 
Mkuu hujui SUGECO Bali nahisi ulisimuliwa tu ila kwa tunaoifahamu tunaona Kama umeandika kitu tofauti kabisa ambacho hakiendani na elimu yako. NIPO karibu Sana na hii SUGECO na inafanya poa Sana na pia uongozi wake Ni imara na wenye vision kubwa Sanaa na wala sio wabwabwajaj Kama wewe.

Kama unataka kuielewa SUGECO vizuri nakushauri uende pale Sua utembelee ofisi zake pale department of Agribusness. Harafu ndo urudi Tena.
 
*SUGECO IMEFUNGUA NJIA KWA VIJANA WAJASIRIAMALI KATIKA SEKTA YA KILIMO BIASHARA*

Vijana wengi wa Tanzania tuna shida kubwa katika bongo zetu. Tumegeuka kuwa jamii ya kulaumu na kulalamika badala ya kuchukua hatua.Tunapenda urahisi. Tunasahau kuwa zama zimebadilika. Hatufikirishi vichwa vyetu kujaribu kutumia japo sehemu ndogo ya elimu tuliyoipata chuoni kutafuta fursa za kukamata.

Badala yake tumekaa tukibweteka tukiamini siku moja tutapata kazi ya ndoto zetu huku siku zikizidi kuyoyoma bila mafanikio. Tumekuwa mizigo kwa wazazi wetu badala ya kuwa msaada. Hakuna mawazo mapya tunayotoa. Zaidi tunatamani utanashati bila kuwa na pesa mfukoni. Kazi za kuchafuka hatuzitaki tena hata kama zinatengeneza pesa kiasi gani. Usomi wetu umetufanya tuchague kazi.

Kijana asiyeenda shule, unakuta ana uwezo mkubwa zaidi wa kutengeneza pesa, kuliko msomi aliyehitimu chuo kikuu. Kijana asiyefika chuo kikuu hachagui kazi na vilevile yuko tayari kumtumia msomi kuuliza kitu asichokijua, lakini msomi yeye kwa upande wake hayuko tayari kujifunza kutoka kwa kijana asiyebahatika kufika chuo kikuu.

Tuna tatizo kubwa sana. Vijana wengi tumekosa mawazo mapya ya Ujasiriamali. Bongo zetu zimelala. Hatuoni fursa mpya pamoja na kwamba fursa hizo zimejaa tele mtaani. Tunahitaji kufunguliwa vichwa vyetu na macho ili tuweza kuondolewa tongotongo zinazotufanya tushishindwe kuona fursa.

Changamoto ya kushindwa kuona fursa haiwakabili tu vijana wasomi waliyohitimu vyuo mbalimbali pekee yao bali hata wazee wetu waliyostaafu kutoka kwenye utumishi wa umma au sekta binafsi nao wanakabiliwa na tatizo hili.

Utastaajabu kumwona mstaafu namna anavyohangaika mtaani kuyakabili maisha yake mapya. Hawezi kufanya kazi nyingine zilizo nje ya fani yake. Matokeo yake baada ya kustaafu utumishi wake, anakuwa hana uwezo tena wa kuratibu na kusimamia mradi utakaompatia pesa na kumwezesha kuishi maisha yanayofanana na yale aliyokuwa akiyaishi alipokuwa kazini.

Mstaafu anaishi maisha ya ajabu kabisa pamoja na kwamba, alipatiwa mafao yake yote na mfuko wake wa hifadhi ya jamii. Amekosa elimu ya ujasiriamali. Pesa za mafao yake ya kustastaafu, anaingiza kwenye miradi mfu. Matokeo yake anapata anguko kubwa lisilo kuwa na mfano.

Lakini yote hii ni kwa sababu kulikuwa hakuna taasisi au watu waliyojitoa sawasawa kunoa bongo za watu wengine ili wawe na uwezo kujitegemea mara baada ya kustaafu au kumaliza viwango mbalimbali vya elimu.

Ushirika wa Wahitimu Wajasiriamali wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUGECO), kwa upande wao waliliona hili na kuamua kwadhati kabisa kujitoa kuwasaidia wahitimu wa vyuo mbalimbali na vijana wasiyowahitimu ili waweze kujiajiri wao wenyewe katika sekta ya Kilimo Biashara.

Kupitia SUGECO, vijana wamekuwa wakifundishwa stadi mbalimbali za kilimo biashara ikiwemo mbinu bora za kuendesha kilimo cha kisasa, kilimo chenye tija, ufugaji bora, Uongezaji wa thamani wa mazao ya Kilimo na mifugo, Usindikaji wa bidhaa mbalimbali za kilimo, uendeshaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo na kuondoa tongotongo katika bongo za vijana, kuwawezesha vijana wahitimu wa vyuo kuwa na miradi yao binafsi na kupata fursa ya kusimamiwa kwa ukaribu na hatua kwa hatua hadi mradi utakaposimama.

Si hivyo tu bali pia SUGECO wanajishughulisha na utoaji wa ufadhili wa mashamba Kitalu au Greenhouse kama ilivyozoeleka na wengi kwa vijana ili kuwawezesha kuendesha shughuli za kilimo chenye udhibiti wa magonjwa. Kana kwamba haitoshi, SUGECO wanaendesha programu kabambe ya kuwapeleka vijana nchini Israel kushiriki mafunzo kwa vitendo katika sekta ya Kilimo. Kila mwaka kuna kundi la vijana wasiyopungua 30 wanapelekwa Israel.

Ukikaa na vijana waliyopata fursa ya kwenda nchini Israel na ukasikiliza shuhuda zao, utabaini wazi kuwa sisi watanzaia bado hatufanyi kazi kabisa. Tunapoteza muda wetu mwingi kizembezembe. Wenzetu kule wanachunga sana muda wao na kujali zaidi kazi. Kwao siku zote muda huwa huwatoshi kutekeleza majukumu yao, hivyo wanajitahidi kuitumia kila dakika inayopatikana kufanya kitu kinachoonekana. Muda kwao una thamani kubwa sana hivyo haupaswi kuchezewa hata kidogo.

Siku zote waisrael wanaamini kuwa hakuna mtu atakayekufa kwa kufanya kazi. Kwa hiyo ukiwa Israel masaa mengi utayatumia kwa ajili ya kufanya kazi. Siku ya mapumziko kwao ni siku moja tu katika wiki na ni siku ya jumamosi ambayo pia siku hiyo wanaitumia kwa ajili ya kukufanya Ibada.

Kuwa meneja Israel ni tofauti sana na kuwa meneja katika nchi zetu za afrika ambapo meneja anakuwa anaongoza kwa kula bata, kule ukiwa meneja hakuna kula bata, bali meneja unakuwa kama manamba mkuu, unaingia kazini wa kwanza na kutoka wa mwisho na ukiwa kazini hakuna ubosi wewe meneja ndiyo unaokuwa mstari wa mbele kufanya kazi mwanzo mwisho. Hayo ni maelezo kwa ufupi sana kutoka kwa vijana waliyobahatika kwenda huko kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo. Mfumo huu wa Israel ndiyo unaotumiwa na SUGECO katika utoaji wa mafunzo ya kilimo kwa vitendo kwa vijana wetu wa Kitanzania.

Mapema mwezi wa kumi mwaka huu, SUGECO kwa kushirikiana na wizara ya kilimo kupitia iliyokuwa Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji (RUBADA) walifanikiwa kuendesha mafunzo ya Mnyororo wa thamani wa Kuku na Sungura katika Kambi ya Vijana ya Kilimo kwa Vitendo katika Kijiji Cha Mkongo wilayani Rufiji. Vijana kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu walikuja kambini hapo kuhudhuria mafunzo hayo ambayo huendeshwa kwa muda wa wiki mbili kwa kila darasa moja.

Kwa namna mafunzo hayo yalivyoratibiwa na kuendeshwa kwa ustadi mkubwa, kila anayepita kambini hapo bila kujali kiwango chake cha elimu na umri, amekuwa akinolewa vizuri na kumwezesha kutoka na elimu itakayomfanya aweze kujitegemea yeye wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa.

Hadi sasa ni awamu mbili tayari zimeshapita katika kambi hiyo ya vijana ya Mkongo Rufiji. Katika awamu ya pili ya mafunzo yaliyofanyika mwezi wa kumi, nami nilipata fursa ya kuwa mmoja wa wawezeshaji katika semina hiyo na kupitia mafunzo hayo niliweza kuwafundisha vijana mnyororo mzima wa thamani wa kuku pamoja na Sungura.

Katika mafunzo hayo, kwahakika nimejionea kwa macho yangu ni kwa namna gani programu hii ya SUGECO inavyowanufaisha Watanzania.
Kwakweli hizi ni aina ya programu ambazo kimsingi kama nchi tunapaswa kuziunga mkono ili Vijana wetu wapite katika kambi hizo ili waweze kujifunza kilimo kwa vitendo pamoja na stadi mbalimbali zinazotolewa katika kambi hiyo zenye lengo la kuwatengeza vijana wawe sababu ya kujiajiri wao wenyewe na kuajiri wengine.

Mfumo wetu wa elimu haumwezeshi moja kwa moja kijana kupata stadi zitakazomwezesha kujiajiri mwenyewe. Lazima vijana bila kujali kiwango chao cha elimu, wapatiwe aina hii ya mafunzo yanayotolewa na SUGECO ili kuwafanya vijana wetu watamani zaidi kujiajiri badala ya kusubiri ajira za Serikali au mashirika.

Nakumbuka katika mafunzo hayo mbali na kujifunza mnyoro wa thamani wa kuku na Sungura, masomo yaliyoendeshwa kwa nadharia na vitendo, pia washiriki waliweza kujifunza kilimo cha mbogamboga na utengenezaji wa bidhaa mbalimba kama vile dawa za chooni, sabuni, shampoo, mishumaa, mafuta ya kupakaa ya mgando pamoja na nguo aina ya batiki.

Lakini somo jingine lililofundishwa siku hiyo ni somo la kubadilisha mtazamo wa kijana kutoka kwenye kasumba ya kutaka kuajiriwa na kupewa mbinu mpya zitakazo msaidia kijana aweze kujiajiri wenyewe na kusimamia mradi wake kikamilifu.

Mkurugenzi wa SUGECO Bwana Revocatus Kimario wakati anatoa salamu zake za jioni kwa washiriki kabla ya kuwasilisha mada yake ya *Namna ya Kumuhudia Mteja,* alianza kwa nukuu ya mwalimu wa kubadilisha mtazamo wa vijana Mr Masimba *“a mindset changer”* iliyosema “Tusaidiane kuondoa kutu vichwwani kwetu.” Nukuu hii ukiitafakari vizuri utaona ni kwa namna gani ilivyojaa ukweli, vichwa vyetu vina kutu nyingi, tunahitaji kusaidiwa kuondolewa.

Bwana Kimario aliniendelea kuwatanabaisha vijana kwa kuwaambia kuwa “tukiwa hapa (kambini) degree zako zote tunaziweka pembeni kwasababu degree zako hazina maana sana kama hauna uwezo wa kutengeneza pesa.” Kimsingi Bwana Kimario alisisitiza sana ubunifu na kujiongeza. Katika hili alisema “aliyejaribu na akashindwa, anafaida kubwa kuliko asiyejaribu. Kufeli haina maana umeshindwa bali utatafuta namna nyingine ya kujaribu.” Bwana Kimario katika kuongezea uzito hili, alimnukuu Bwana Jeseph Chilton Pearce aliyeelezea thamani ya ubunifu aliyosema, to live a creative life we must lose our fear of being wrong.” Kwa taafsiri isiyo rasmi akimaanisha kwamba kuishi maisha ya ubunifu kunahitaji kuondoa hofu ya kukosea.

Baada ya utangulizo huo aliyoutoa kwa washiriki, Mkurugenzi aliendelea na somo lake la *Namna ya Kumuhudumia Mteja.* Somo lilikuwa nzuri na kila mshiriki alivutiwa nalo. Laiti nafasi ingeruhusu ningeweza kulidadavua somo hilo kwa upana wake kadiri ya mafundisho yalivyotolewa Mkurugenzi ndugu Kimario.

SUGECO imeundwa na vichwa vinavyojua kufikiria. Vinavyojua kiini cha tatizo la ajira kwa vijana na namna ya kuondoa tatizo hilo kupitia mafunzo ya kilimo Biashara. Kwahiyo wahenga walisema usione vyaelea, vimeundwa. Mambo yote mazuri yanayofanywa na SUGECO ni matokeo ya uratibu mzuri wa watu wafuatao: Kuna Dokta Anna Temu, ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi na Dokta Flugence Mishili Makamu mwenyekiti. Kwenye kamati ya utalaam na ufundi kuna Dokta Daniel Ndyetabula, Dokta Betty Waized, na Dokta Felix Nandonde. Kwenye utawala utakutana na Bwana Revecatus Kimario, ambaye ni Mkurugenzi wa SUGECO, Bwana Joseph Masimba Mratibu wa Miradi, Bwana Ayubu E. Mundekesye meneja wa Mafunzo, Dickson Alex Mseko Meneja wa shamba na Prekseda Melkior kaimu meneja wa shamba.

Vichwa vyote hivyo kwa pamoja ndivyo vilivyotengeza wajasiriamali vijana wengi nchini katika sekta ya kilimo. Kila kona ya nchi ukipita utakutana na vijana wengi waliyonolewa na SUGECO wakishughulika na mafundo mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa kilimo. Kuna wale wanaolima alizeti na kuchakata mafuta, kuna wanaozalisha asali, kuna wanaolima mbogamboga kupitia shamba kitalu, kuna wanaozalisha mbegu za viazi lishe na kulima viazi. Kuna waliyosaidiwa kuanzisha viwanda mbalimbali vya usindikaji. Kuna wanao jishughulisha na ufugaji wa kuku, Samaki na Mifugo mingine. Ukipita SUGECO kwahakika lazima utabadilika kifikra na kimtazomo.

Kwa ajili ya kuwafikia vijana wengi nchini ilifaa sana kama Wizara ya Kilimo na Ushirika, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi pamoja na Wizara ya Vijana, kazi na ajira wangeangalia namna bora ya kushirikiana na SUGECO ili kuanzisha kambi mbalimbali za mafunzo ya kilimo kwa vitendo na kubadilisha fikra na mitazamo ya vijana. Kwa kufanya hivyo tutajenga taifa la kutenda badala ya kuwa taifa la kulalalamika. Na mwishowe matokeo chanya ya kiuchumi kwa vijana wetu na nchi kwa ujumla yangeonekana hasa katika kipindiki hiki ambacho nchi inaelekea kwenye uchumi wa viwanda.

Aman Ng'oma
Mkurugenzi Mtendaji
Kinasoru East Africa Tanzania Ltd
Info@kinasoruea.co.tz or amanngoma@gmail.com
0767989713 or 0715989713
Nduka Street, Chamwino Bonanza
Dodoma
*TANZANIA.*
 
Back
Top Bottom