Renatus Mkinga; jiandae kuchukua jimbo, unafaa sana!

akelu kungisi

Senior Member
Apr 2, 2012
115
19
Jana usiku katika kipindi cha malumbano ya hoja kinachorushwa na ITV, mwanaharakati na mzalendo wa ukweli Ndg Renatusi Mkinga aliendelea kudhihirisha na kuonyesha uwezo katika kujenga hoja zenye uzalendo na ukombozi kwa nchi yake.
Si jana tu, Ndg Renatusi Mkinga ni maranyingi kwa muda wa miaka mingi amekuwa akiwajambisha magamba kwa hoja zake mara apatapo nafasi ya kufanya hivyo! Mengi yanaweza kusemwa kuhusu yeye, lakini lililo kubwa zaidi ni kumuomba aanze kufanya maandalizi ya mapema katika harakati za kuingia mjengoni mwaka 2015. Huyu jamaa nina aminim kuwa kama atafanikiwa kuingia pale basi magamba watamkoma!
Nakumbuka Lisu kabla hajawa mbunge, naye alikuwa kama huyu mzee Mkinga, nionavyo mimi mawazo yake yatakuwa na maana zaidi iwapo atayatoa katika mfumo sahihi unaotambuliwa kisheria( bunge) kuliko huko aliko kwani magamba wanamuona mpayukaji.
Renatusi kama unachungulia humu JF naomba uyachukue na kuyapima mawazo yangu juu yako then yafanyie kazi ikibidi.
 
mzee ni kiboko,una upeo wa mbali!anatoka jimbo gani?au tumpe kigamboni,temeke au kinondoni
 
Nakumnuka alitolea ufafanuzi hizo hela japo haikuwa lazima kufanya hivyoooo. kama sikose alisema nyumba ya kuishi anayo, atasomeshae watoto wake

Uyo mzee si ndio yule alie shinda zile milion mia za voda com? kwa kuanzia apo amezifanyia nini zile pesa kama kweli aya ongeayo ana weza kuya timiza akipata nafasi.
 
mzee ni kiboko,una upeo wa mbali!anatoka jimbo gani?au tumpe kigamboni,temeke au kinondoni

Jimbo lolote ndani ya jiji la Dar huyo bwana anaweza kuchukua kwa kutumia hoja tu bila kuhonga wapiga kura, tafuteni Mbunge feki yeyote wa CCM ndani ya jiji ili ang'olewe na Mkinga
 
Huyu mzee nim mwenyeji wa mkoa Ruvuma, lakini kwa Tanzania yetu ambayo haina ukanda wala ukabila anaweza kugombea jimbo lolote lile maadamu anakubalika, na yeye ana-deserve kugombea jimbo lolote kwa namna alivyojitambulisha katika jamii. Mi nashauri aende Songea mjini au aende kinondoni akamung'oe Azan.
Habari za milioni 100 hapa sio mahali pake, siku zote tunashauri ukikosa hoja kaa kimya, huu ni uwanja wa tafakuri shadidi sio utani wa kitoto unaopwelea!
 
anatoka Ruvuma huyo, ila kwani kila mtu anayepinga utendaji wa serikali lazima agombee ubunge? aendelee kuwa mkosoaji hivyo hivyo!
 
uyu dingi namzimia ila am sure kila baada ya vipindi kama cha jana anakuwa amepungua uzito!
As anaongea with all the strength that he has!
Ninachoshukuru ni kuwa amepona maana last time wakati wa mgomo wa madr alilazwa MOI
 
huyu mzee alidhani magamba wanataka wanaharakati basi akagombea huko kwao kupitia ccm akidhani atachukua jimbo. Yani muda huu angekuwa mjengoni kupitia cdm. Bado hajachelewa
 
Its pathetic bcoz mkinga ni mgonjwa hawezi kuhimili mikikimikiki ya siasa uchwara za bongo
 
Uyo mzee si ndio yule alie shinda zile milion mia za voda com? kwa kuanzia apo amezifanyia nini zile pesa kama kweli aya ongeayo ana weza kuya timiza akipata nafasi.

Matumizi ya hizo pesa kwa vile ni za kwake "it is none of your business". Mzee huyu anajenga hoja za uhakika
 
Jana usiku katika kipindi cha malumbano ya hoja kinachorushwa na ITV, mwanaharakati na mzalendo wa ukweli Ndg Renatusi Mkinga aliendelea kudhihirisha na kuonyesha uwezo katika kujenga hoja zenye uzalendo na ukombozi kwa nchi yake.
Si jana tu, Ndg Renatusi Mkinga ni maranyingi kwa muda wa miaka mingi amekuwa akiwajambisha magamba kwa hoja zake mara apatapo nafasi ya kufanya hivyo! Mengi yanaweza kusemwa kuhusu yeye, lakini lililo kubwa zaidi ni kumuomba aanze kufanya maandalizi ya mapema katika harakati za kuingia mjengoni mwaka 2015. Huyu jamaa nina aminim kuwa kama atafanikiwa kuingia pale basi magamba watamkoma!
Nakumbuka Lisu kabla hajawa mbunge, naye alikuwa kama huyu mzee Mkinga, nionavyo mimi mawazo yake yatakuwa na maana zaidi iwapo atayatoa katika mfumo sahihi unaotambuliwa kisheria( bunge) kuliko huko aliko kwani magamba wanamuona mpayukaji.
Renatusi kama unachungulia humu JF naomba uyachukue na kuyapima mawazo yangu juu yako then yafanyie kazi ikibidi.

Tatizo ni kada wa magamba
Akiwa mbunge kelele zote hizo zitaisha bora ahame chama
 
anatoka Ruvuma huyo, ila kwani kila mtu anayepinga utendaji wa serikali lazima agombee ubunge? aendelee kuwa mkosoaji hivyo hivyo!

Sawa ila kwa mfumo mfu wa hapa tz yabidii aingie bunge hasa jimbo la kinondon,pia inasaidia kuongeza fito zaid za kutandika hawa gambaz bunge.Hebu fikir kidogo hapa Mnyika,Zitto,Mdee,Dogo janja then Renatus Mkinga hapo lazima spika akione kit cha moto,kwel kabisa huyu mzee agombee ubunge.Suala la kusema alitumiaje mia za voda halina tija,tumwambie ajiandae kuwa mbunge hakuna la zaidm
 
Mzee anatisha sema 2 aligoambea magamba songea mjini kichwa kubwa akampiga bao,hamia cdm mkinga.huwa afichifichi mambo utadhani jamaa nnaemmaind Lema
 
Sasa na wewe mbona hukutusanua jana tumsikie madini ya mwanaharakati Mkinga, roho mbaya tu hiyo!! Tatizo la Mkinga yupo upande wa Magamba,aliwahi kugombea kwao CCM wakampiga chini coz hakuwa na ile kitu ya Mwigulu(rushwa).
 
Tatizo Mkinga ni mwoga wa siasa na kwa ufupi hawezi. kwani 2010 aligombea Songea mjini kupitia CCM na alimaliza akiwa nafasi ya 3 kwenye kura za maoni nyuma ya Nchimbi na Mhaiki.
Tatizo lake katika mikutano yake hakujua aina ya wapiga kura wake na matatizo walionayo.

Nilihudhuria katika kampeni zake kipindi cha kura za maoni kwa kweli alikosa mvuto kwa wapiga kura.(Mvuto wa ushawishi sio wa sura).
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom