Rejesha Nyota yako Kimapenzi

Gagurito

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
5,600
803
je unataka kurejesha nyota yako kimapenzi? Unapaswa kutambua kuwa kitu chochote muhimu na kizuri duniani kina hitaji mbinu sahihi ya kukipata. Hivi ndivyo hata katika mapenzi ilivyo, utakapo kurejesha nyota yako ya kimapenzi, unashauriwa kuchagua marafiki wenye staha ili uweze kufurahia maisha, fanya tathimin ya mwenendo wa mapenzi yenu, wewe na mweza wako, iwapo mambo hayako sawa jitahidi urekebishe haraka ipasavyo. Fanya mambo ambayo mkeo/mchumba/mpenzi wako huyafurahia na epuka kumkwaza mara kwa mara. Jitahidi kujali mambo yote mfanyayo na mwenza wako (hapa nakushauri uwe na kumbukumbu ktk golden moments zenu), usiwe mtu wa kukuza mambo na jitahidi kusamehe pale ukosewapo... Jishughuri she kuepuka utegemezi.
Mengine ongezeni, kosoa pale uonapo sipo sawa!
 
Kwahiyo wewe ni msomaji wa nyota!?Mbona sasa hujaelezea hiyo jinsi ya “kusafisha nyota“ umeelezea tu nini kifanyike baada ?!Naomba mwongozo!
 
Kwahiyo wewe ni msomaji wa nyota!?Mbona sasa hujaelezea hiyo jinsi ya “kusafisha nyota“ umeelezea tu nini kifanyike baada ?!Naomba mwongozo!
Hiyo ndio jinsi yenyewe, nisemapo nyota sina maana ya yale madudu afanyayo sheikh yahya, namaanisha jinsi ya kung'arisha mapenzi yako!
 
natania tu baby gal...infact nyota yako inang'ara sana mpaka naogopa kukatiza mbele yake.
Nilirudi na makombora ila naona siyahitaji.Nashukuru kwamba ulikua unatania tu.Kupita we pita tu ..I don‘t bite.
 
Hiyo ndio jinsi yenyewe, nisemapo nyota sina maana ya yale madudu afanyayo sheikh yahya, namaanisha jinsi ya kung'arisha mapenzi yako!
Sasa kama sio hivyo uliona umuhimu gani wa kutumia neno nyota wakati hua haliishi kuhusishwa na mambo ya unajimu?!Au ndo unaingilia fani za watu bila kujua?!
 
Sasa kama sio hivyo uliona umuhimu gani wa kutumia neno nyota wakati hua haliishi kuhusishwa na mambo ya unajimu?!Au ndo unaingilia fani za watu bila kujua?!

Unamaanisha kaachiwa mikoba na MUFTI MKUU NA MNAJIMU AFRICA MASHARIKI<KATI NJE NA NDANI HUSSEIN YAHYA?
 
Sasa kama sio hivyo uliona umuhimu gani wa kutumia neno nyota wakati hua haliishi kuhusishwa na mambo ya unajimu?!Au ndo unaingilia fani za watu bila kujua?!
Tatizo lako wewe unawaza mambo ya unajimu sana. Ukisikia mtu kasema "yule ni nyota wa filamu" we utawaza unajimu?
 
Back
Top Bottom