Masako ameshajifanyia nini yeye mwenyewe na familia yake mpaka sasa anadhani anaweza kuwafanyia chochote wengine? Yeye aseme amegundua kuwa ubunge ni ajira yenye kulipa vizuri, na mara nyingine Rais anaweza kukuongeza ulaji - ama uwaziri, ukuu wa mkoa au wilaya, ubalozi, uenyekiti wa bodi nk. Umefika wakati wanasiasa wa Tanzania waache usanii, wawe wakweli. Hakuna anayeomba kugomembea ubunge kwa tiketi ya CCM, anayefanya hivyo kwa 'sababu ana nia ya kumfanyia yeyote chochote.