Rehema Mwakangale hayupo nasi

RIP Rehema.

Namkumbuka Rehema hususani kipindi kile wakati anaanza kusoma taarifa ya habari akiwa na Iddi Ligongo... Alianza kwa kusuasua lakini baadaye akawa mtangazaji mahiri wa habari ya TV wa ITV.

Taa na nuru iliyokuwa inang'aa imezimika ghafla.

Tutakukumbuka daima Rehema!!!
 
Inasikitisha lakini ndio njia yetu sote Kinachonihudhunisha ni ucheshi na utaratibu wa Marehemu Rehema Hapakuwa na Presenter aliekuwa mfano wake hakuwa na majivuno Ni Mtaratibu Mkimya Na Alikuwa na Busara Mwenyezi Mungu ailaze Pema Peponi Roho ya Marehemu -Aamin
 
Poleni wafiwa.
Ni safari ya wote ila kutangulia ndiko kugumu!
Pumzika kwa amani rehema.
 
duh! hakuna atakayeishi milele, sote tu wapitaji hapa duniani.
poleni wafiwa, itv na wanahabari wote.
 
Poleni wafiwa, mwakanale ni msiba wetu sote. Pia tujue kwamba kifo kimeumbwa kama tulivyoumbwa sisi. Hivyo ili kiendelee kuishi lazima binaadamu tuendelee kufa. Hii maana yake huu ndio mfumo wa maisha
 
Jamani Rehema! Its too sad.

Pumuzika kwa amani dada, nasi tuko nyuma yako
 
Jamani kabla hatujamtukuza Mungu KWA KAZI YAKE KAMILIFU ni vyema tukajiuliza maswali.

Mwenzetu alikuwa anasumbuliwa na nini? aliugua kwa kipindi gani? Ingewezekana juhudi za kibinadamu kuuokoa uzima wake?

...Ni vyema, tukawa tunajiuliza matatizo yanayowakumba wananchi wenzetu..je chanzo ni nini? na ni vipi vifo kama hivi vinaweza kuepukika? Haitoshi kusema ni mapenzi ya Mungu...we have to do more.. Leo dereva anaendesha gari kwa uzembe anasababisha ajali ya watu hamsini wote wanakufa..lakini hakuna anayeuliza hard question..wote...ni msemo ule ule.."mipango ya Mungu" really? Leo tunamzika Albino..aliyeuawa kikatili..msemo ni ule ule..ni "mapenzi ya Mungu" NADHANI HUYU MUNGU tunamsingizia mengine.

Uhai wa mtu uthaminiwe. na Kuuthamini ni kuuliza matatizo kama haya kusudi kama ni juhudi kufanyika next time..watu wajitahidi. Kama ni malaria..watu wajue namna ya kukabiliana na mbu. nk... Tuache kuchanganya imani zetu na vitu ambavyo hakika vinaepukika. Jiulize huyu dada kama ndo lets say kaolewa juzi juzi (simjui kiundani)..ameacha mme na mtoto..hii yote ni hasara tupu...mtoto atakuwa yatima..bwana atakuwa mjane nk...

RIP Rehema! You were an incredible girl full of life and energy!

Raha ya Milele umpatie ee bwana, Mwanga wa milele umwangazie.

Tunaweza pata kidogo historia fupi ya marehemu?
Jamani mwenye data p'se.
Tupo pamoja ndugu,rafiki,wapenzi wa ITV na maadui katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Ni kweli kabisa.

Wafiwa poleni sana.
 
Back
Top Bottom