Rehema Mwakangale hayupo nasi

Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Rehema.Pole mzee Mwakangale na familia yote na wajukuu wote wa Mzee John Mwakangale (Mwenyekiti wa zamani wa CCM-Mbeya). Steven popote ulipo nakupa pole sana katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na binamu yako.
 
Kazi ya Mungu haina makosa...poleni wanafamilia na wapenzi wa ITV dada alikuwa msomaji mzuri wa taarifa za habari

Inna lilahi waina ilaihi Raajiun
 
P.I.P Rehema. Mungu awape faraja familia ya Mwakangale. Binafsi nilivutiwa sana na kazi yake ya utangazaji kwa lugha fasaha na tabasamu juu. Binadamu tu mavumbi na mavumbini tutarudi.
 
RIP Rehema. Poleni wafiwa. Bwana ametoa na Bwana ametwaa. Jina la Bwana Lihimidiwe.
 
She was a very confident presenter especially during Taarifa Habari ITV usiku saa 2!

RIP!

Over Massanja's Concern: Jamani hivi kwa madaktari..Pumu husababishwa na nini na mtu unawezaje kujikinga? Dalili zake ni zipi?
 
Mungu ailaze roho ya marehem mpendwa wetu mahali pema peponi, amina

Please Family members and JF accept my condolences.
 
She was a very confident presenter especially during Taarifa Habari ITV usiku saa 2!

RIP!

Over Massanja's Concern: Jamani hivi kwa madaktari..Pumu husababishwa na nini na mtu unawezaje kujikinga? Dalili zake ni zipi?


Mungu ailaze roho ya marehemu (Rehema Mwakangale) mahala pema peponi.
 
Msiba upo sinza karibu na sinza delux hotel kwa watakaoweza kuhudhuria,mwenyezi mungu mwema akukumbatia katika mikono yake na akupumzishe kutokana na shida zote ulizopata hapa duniani
 
Inauma sana, kweli vizuri havidumu, REHEMA hakuwa na majivuno kabisa kama ilivyo kwa wasichana wengine walio maarufu, alisalimia kila mtu mtaani hata watoto, yeye kwake ni tabasamu tu muda wote!! aliwapenda watoto sana!! basi tena bwana ametwaa jina lake libalikiwe.
Nasi tujiandae kwa safari ambayo hatujui muda wala saa.

Nawapa pole sana sana wafiwa woote.
 
Back
Top Bottom