Speaker
JF-Expert Member
- Aug 12, 2010
- 6,324
- 2,238
- Thread starter
- #101
Mh. Regia wengi mmemuelezea hapa na kuonyesha jinsi mnavyo mkubali. Nami namkubali vivyo hivyo na zaidi ya yote sijawahi kutana nae hata siku moja. Lakini kwa dhati kabisa huyu dada Mh. ndani ya wiki moja iliyopita amenipa msaada mkubwa sana kwa mzazi wangu tena kwa kutumia pesa zake kunifanyia huo msaada bila kujali kama ningeweza kumrudishia pesa zake au la!
Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru kwa jambo ilo na hata nilipofanikiwa kuongea nae, nilimwambia asante kwa msaada huu mkubwa na Mungu amuongee zaidi na zaidi.
Mh. Regia asante sana kwa msaada na Mama yangu (kule Lindi) ameshukuru sana kwa huduma uliyomsaidia.
Nikifika Dar nitakuja Makao Makuu kuja kukusalimia.
She has a heart of giving too?
Tena hata kwa wasio wananchi wa jimbo lake maana tungesema anasaidia wampe kura lakini nop,hachagui!
God bless you regy,keep it up and have the heart of fearing God always and He will guide you