Elections 2010 Regia Mtema kupata ushindi wa kishindo Kilombero

josiah2008

Member
May 22, 2010
51
23
Mgombea ubunge katika jimbo la Kilombero kwa tiketi ya CHADEMA Regia Mtema atapata ushindi mkubwa dhidi ya mgombea wa CCM Abdul Mteketa. Regia Mtema ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja kushawishi na kuwa na majibu ya matatizo ya muda mrefu ya wananchi wa jimbo la kilombero.

Mgombea wa CCM hana uwezo wa kujieleza kabisa hali iliyolazimu makada wa chama kuja kujaribu kukinusuru.Sofia Simba,Kingunge,Getrude Lwakatare pamoja na mjumbe wa halmashauri kuu CCM wote hawakuweza kubadili upepo wa mabadiliko.Hata JK alipokuja alishindwa kumnadi na kuishia kumwagia sifa mgombea udiwani wa kata ya Ifakara.

Regia Mtema amemalizia kampeni zake kwenye kata ya Lumemo mkutano ambao umevunja rekodi kwa idadi ya watu waliohudhuria.Kila mtu hapa anataka mabadiliko kitu ambacho huwezi kuamini kwani jimbo hili CCM walikuwa wamejichimbia mizizi sana.Walidiriki kusema hata ukiweka koti kwa tiketi ya CCM litashinda.

Kwa hali ilivyo Regia Mtema atapata kura za CHADEMA ,CUF na CCM kwani katika wagombea wote yeye pekee ndiye mwenye uwezo wa kuleta maendeleo hapa Kilombero na anakubalika.

Tumeshajiandaa vizuri majina yetu tumeshayaona asubuhi na mapema tunakwenda kutoa hukuma kwa kosa la kututawala kwa miaka 50 tukiwa kwenye nyumba za Tembe.

KILOMBERO4CHANGE
 
it seems God is on our side, Let's go and vote for change.

YES WE CAN
 
Heshima kwako mkuu
Hiyo ni habari njema sana kuona kuwa kuna kila dalili za mpiganaji kuchukua hilo jimbo kwa ajili ya maendeleo yenu mnatakiwa kuwa makini tu na akila aina ya uchakachuaji ambao utafanywa kujaribu kuzuia ushindi. KILA LA HERI
 
Ngoja aje hater wake hapa lol. Na ikitokea kweli sisteri akashinda...patakuwa patamu hapa maana alikejeliwa saana hapa. Vilevile itokee ashindwe....someone will gloat and scream to high heavens 'i told you so'....cant wait to see this one plays out
 
Hahaha ahaha ahaha! aisee naisubiri sana kwa hamu hiyo siku!
 
Nimeshapiga kura yangu kwa Regia Mtema vijana ni wengi hamasa ni kubwa tofauti na miaka iliyopita.Nilipokuwa kwenye foleni ya kupiga kura wale waliokuwa wakiondoka baada ya kumaliza kupiga kura walikuwa wakisema "tumeshaua".Ushindi ni dhahiri.Kama wewe bado wahi ili baadaye wasije na visingizio karatasi zimekwisha.
 
Regia mpaka hapo ni mshindi....
Hukusubiri upate kwa huruma, uliona unaweza ndo maana ulithubutu. Wewe ni mwanamke jasiri.
Kila la kheri .
 
go gender sensitive gooooooo

Na wewe? Mbona anasema ni uwezo wake wa kujenga hoja na wala siyo kwa sababu yeye ni mwanamke. Wewe bado una fikra za kuonewa huruma na kupendelewa wakati watu wanachagu mtu mwene uwezo
 
Regia mpaka hapo ni mshindi....
Hukusubiri upate kwa huruma, uliona unaweza ndo maana ulithubutu. Wewe ni mwanamke jasiri.
Kila la kheri .

umesema sawa kabisa dear....ameweza kujaribu, na ameonyesha anaweza.......wakwetu umeshapiga kura?...hope hujalipa dudu liumalo kidole
 
umesema sawa kabisa dear....ameweza kujaribu, na ameonyesha anaweza.......wakwetu umeshapiga kura?...hope hujalipa dudu liumalo kidole

Preta... you never stops to amaze me... Kumbe dudu liumalo kidole ndo lile...???!!!!

Kweli a second can add millions to our lives
 
Gender Sensitive, wishing you all the best to bring change we can believe in Kilombero!!
 
umesema sawa kabisa dear....ameweza kujaribu, na ameonyesha anaweza.......wakwetu umeshapiga kura?...hope hujalipa dudu liumalo kidole
Wakunyumba, sikupata wasaa kuhakiki jina langu, I have been all over udsm natafuta jina langu silioni. Narudi nilipoanzia sasa nicheki upya.
 
Back
Top Bottom