Regia alimkwepesha pacha wake na ajali

Pole Remija.

Pumzika kwa amani Regia, tulikupenda ila Mungu kampenda zaidi.
 
Death is not a full stop. It is just a commer. kila kifo hupangwa na Mungu, Regia ameondoka lakini yale mambo aliyoifanyia dunia yataendelea kuwepo vizazi na vizazi. kwa mfano, Jina la Regia litaendelea kuwepo kwamba alikuwa mbunge na mwakilishi wa jimbo la kilombero kupitia viti maalum chadema. Kumbukumbu hii ni miongoni mwa nyingi ambazo zitaendelea kuishi kwa jina la Regia Mtema.

R.I.P
 
Hadi sasa sijajua niseme nini!
Ni mgumu wa kutoa machozi, lakini kila nikisoma post kuhusu dada yangu RM machozi yanatoka yenyewe.
...anyway, umeacha legacy kubwa mpiganaji wetu mpendwa Regia Mtema.
 
Pole sana Regima....R.I.P Regia.....Poleni Familia....Poleni JF member wote na watanzania wote ....inauma sana kwa kweli..Taifa limepoteza kifaa....katika umri mdogo kabisa
 
Pole sana binti kwa kumpoteza pacha wako.

Lakin siku zote yanapotokea mambo kama haya lazima tujifunze kitu.

Kwa mujibu wa picha nilizo ziona kule kwa Issa Michuzi inaonyesha wazi Dereva alikuwa hajafunga mkanda wake (Safety belt) na pasi na shaka yoyote aliowapakia walikuwa wamefunga.

Vile vile ni lazima iwekwe sheria kwa viongozi kama wabunge wasiruhusiwe kuendesha magari wenyewe bali wawe na ma driver ambao watawaendesha hii sio tu kuwakinga na ajali bali pia kuwapa ajira madereva ambao ni professional.

Ni vizuri mzingatie sheria za barabarani mara mnapotumia barabara.

 
Poleni sana ndugu na familia nzima kwa kuondokewa na mpendwa wenu/wetu. Mungu awabariki na kuwatia nguvu katika kipindi hiki kigumu. Nawapeni ujumbe huu:- The LORD is a refuge for the oppressed, a stronghold in times of trouble. PUMZIKA KWA AMANI REGIA
 
Poleni sana kwa Kifo cha Mh.Mbunge Regia,

Tumepoteza Kiongozi kijana ambaye alikuwa ni mtetezi wa wanyonge,

Wana Familia ya Regia ninawapa pole zangu za dhati kutoka ndani ya uvungu wa moyo wangu,

Pacha wa Marehemu pole sana na Mungu akutie nguvu,

Kazi ya MUNGU haina makosa,

Tumuenzi Regia kwa kuacha UFISADI hapa TANZANIA.

R.I.P REGIA
 
Kwanini kafa yeye peke yake kwenye ile ajali? Ina maana alilengwa tu yeye? Dah, najiuliza maswali mengi na napatwa hasira alichotufanya huyu dada. Any way siwezi mrudisha duniani lakini watu wenye potential kubwa wanapaswa kujifahamu na kujilinda sana, Tanzania nzima inawahitaji sana. Mafisadi hawafi, wanakufa watu muhimu. Hatuwezi kuafford kupoteza watu wengine muhimu kwa ajali kama hivi ilivyotokea kwa Reggia.
 
Pole sana Remija na familia nzima kwa msiba wa mwenzetu Regia.Tulikupenda sana Regia ila mwenyezi Mungu amekupenda zaidi.
 
mungu akupe moyo wa subira dada remija katika kipindi hiki kigum neno la mungu linasema tushukuru kwa kila jambo basi nasi tushukuru kwa hili pia bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe.
 
nasikia maumivu tu rohoni, poleni wafiwa na taifa kwa ujumla
 
Back
Top Bottom