Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 988
Mkuu,
Hii dunia ngumu sana, hawa watu wa mataifa yaliyoendelea wanapoleta project zao huwa wa nani ya kurudisha pesa zao kwao.Mfano wanapo ipa nchi fulani masaada wanaipa na masharti kwamba consultation lazima apewe mtu kutoka kwao na tena kwa dau kubwa.Hii ni kuhakikisha tu 80% inarudi kwao.
Lazima uelewe kuwa uelewa wa mwenye phd ni narrow band but sharp. wakati walio chini ni broad but butu. Na hata hivyo experience kubwa kazini nayo unaweza kuwa awarded phd. Na mambo ya consultation yana miono mingi sana kiuchumi,u active wa mtu husika kwa vitendo ktk hiyo kazi inayohitaji consultation nk.
Na hata hivyo je ulishawahi pia kujuuliza kwamba project za RESEARCH hawa unaowataja wanaowaletea consultation huwa mnaletewa pia ninyi undergraduate? Na pia ipi kati ya hizo ina uzito mzito?
Mkubwa,
Sasa naona tunaanza kukubaliana na ninachosema. Lakini kabla ya kukisema naomba nikusisitize kwamba sifanyi kazi kwenye kampuni ambayo ni aid oriented. Na mimi sijatoa mfano kwenye institution ambayo ni aid oriented. Hizo zinaangukia kulekue kwenye NGOs. Nimefanya kwenye service na production oriented.
Kumbuka kampuni za siku hizi ni globa oriented. Kampuni iko Tz lakini imesambaa nchi kadhaa duniani. Ninachowafahamisha hapa wenzangu ni kuwa kampni siku hzi zimeamzisha academic institutions zao kwa ajili ya trainings mbalimbali. Zingine zinatoa hadi degree kwenye discpline ya eneo au biashara hiyohiyo inayoendeshwa.
Tuje kwenye point yako nzuri. Umesema kuwa experience ya kazni inaweza kuwa PhD. Hili ndilo wengi duniani ambalo hawajaliona. Kuna kampuni zimeanzisha research department baada ya kutambua wameajiri vijana wazuri kwa research. Sasa kama mtu ndani ya kampuni amefanya research kadhaa na zikaongeza efficiency kwenye kampuni kwa nini kampuni isimuone ni equivalent na PhD kama unavyosema.
Nimesema kuwa mimi nina graduate na sina hata masters. Si kwamba siwezi kusoma masters bali hata pesa ya kujilipia au mwajiri kunilipia si tatizo. Lakini kutkana na ukweli aliosema Regia na ninaoufhamau kuwa niende University kuingiza nini kichwani ambacho nikikaa chumbani kwangu ninashindwa kukielewa nikikisoma?
Maoni yangu ni nini? Maoni yangu ni kwamba tukubali kwamba assesment mode zimekuwa nyingi na ndiyo maana hata wewe unasema dunia imekuwa ngumu. Assesment ya zamani ilikuwa ni University na huko award unayopata ni masters, Phd na Uprofessa. Sasa hivi assesors ni wengi wakiwemo employers, viwanda na centre nyingi za production.
Watakaoendelea kulinganisha PhD na upreofessor kama nguzo pekee za performance basi waendelee hvyohivyo kulala usingizi wa pono watajikuta wamechelewa kuamka. Tena wataamka na kugundua kuwa hata watumie mbio zipi wameshachelewa.
Kuna jamaa hapa juu kasema darasa la saba anajenga nyumba wakati proffessa anashindwa. PhD zijiuze kokote zishiishie kwenye Academic Institutons, NOG na Public Organs. Waje na hizo PhD zao tushindane kwenye soko la ajira watuthibitishie ukali wao.
Nakubaliana na wewe kuwa PhD ni narrow lakini sharp. Hiki ndicho kimewaua. Mtu anapata PhD anajifungia chuoni. Phd is about research. Kupata Phd ni kwamba umefanya research. Maana yake ni kwamba you are capable of conducting a convicing research. Sasa kama wako hivyo waje huku kwenye makampuni. HUku kuna maeneno mengi yanahitajia resrach.
Lakini wakiishia kujifungia vyuoni wakisubiri wafuatwe matokeo yake tutawaona wanatembea na ndala na kuishia kunywa pombe kila siku kwa frustrations.
Nasubiri mchango wako.