Referendum for Zanzibar Independence

Mimi sitaki muungano uvunjike, ila sijui mimi ni mjinga; sielewi kwa nini hakuna serikali ya Tanganyika, na baraza la mawaziri ri wa Tanganyika, na baraza la wawakilishi la Tanganyika. Mfano waziri wa nishati na madini ni wa Tanganyika na sio wa Jamhuri ya muungano. Lakini anaitwa wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lipojadili bajeti ya wizara hii wazenji wanatakiwa watoke bungeni kwa sabau suala hili haliwahusu, lakini wanabaki, sijui kwa maslahi ya nani. Sielewi kabisa.
 
Mkandara in action.. unajua uko paranoid sana. wewe wapi katika madai yao wazanzibar walieleza wanataka sultan na shamte warudi?hizo i idea zako wewe tu na kila mjadala ambao unahusu Zanzibar wewe basi utaleta Usultani na Shamte! move on Bro! tuko 2012 na siyo 60's tena.hiyo ya kung'ang'ania point moja kila wakati inaonyesha jinsi gani huna sensible arguments. nimeshawahi kukuambia huko nyuma ya kuwa huijui Zanzibar lakini unataka uonekani kama unaijua.Asilimia kubwa sana ya wazanzibar Wanakubali kabisa mapinduzi ya 64 lazima yatokee ima ya umwagaji wa damu au na siyo ya umwagaji wa damu lakini lazima yatokee,lakini kinachowaliza zaidi wazanzibari ni kwa nini baada kufanyika mapinduzi ambayo yaliacha vilio vingi sana na watu kupoteza malizao jamaa zao(waarabu na waafrika) ili kuondosha matabaka na unyonyaji zanzibar na unaenda kugawa uhuru huo kwa Tanganyika na kuwa ndiyo muamuzi wa mambo ya Zanzibar.sasa hapo kuna tofauti gani na Usultani.Sasa wanzazibar wanataka ku control their own destiny kama watauwana au vp lakini maamuzi hayatoki dodoma na usifikirie hizi ni kelele la mlango tu.. kwani hizi harakati zina gain momentum kila leo.Mwisho wacha kuwataja Sultani na Shamte.. wakati wao umepita tafuta kitu chengine cha kuzungumza ili ki support points zako

Mbona unatokwa na povu mkuu wangu taratibu.. Unasema sijui historia ya Zanzibar wewe unayeijua nambie. Unajua kwamba Mapinduzi yalitokana na mpango ulofanywa baina ya Wabara na Wazanzibar kutokana na asili ya wakazi wake. Zanzibar ilikuwa tawala toka Malindi hadi Kilwa kwa huku bara na visiwa vyake. Asili ya watu wake walikuwa wamechanganyikana ktk nchi hizi tatu leo wewe unataka kutumia Mapinduzi na mipaka ili kuonyesha dhulma iliyofanyika wakati huo huo ukisifia Mapinduzi?.. umesimama wapi weye!.

Bara inawatawala kivipi?. rais mnaye Mzanzibar na sidhani kama unaweza nionyesha wapi JK au serikali ya bara inawatawala, wapi JK ameingilia maswala ya uongozi wa Zanzibar lakini naweza kukuonyesha wapi viomngozi wa Zanzibar wamedai mamalaka ktk serikali ya bara toka muungano.. Viongozi wa Zanzibar kibao wapo ktk Udiwani, ubunge, ukuu wa mikoa na wilaya, serikali kuu huku bara na wanafanya kazi na hatuwabagui kamaWazanzibar..

Wapo Wazanzibar kibao wamehamia bara kabla hata ya Uhuru na wamesambaa hadi vijijini hawa mbona huwafikirii wao isipokuwa Uhuru wa bendera ambao sijui utakusaidia kitu gani tofauti na mlivyo leo. Unasema nisimseme Shamte na Sultan kwani Jussa alikuwa chama gani sii Hizbu huyu pamoja na huyo Seif Hamad. Hii ndio itikadi na asili ya uanasiasa wao na Shamte na Sultan ni viongozi wao wa kwanza.

Ubishani wa nini, mimi naomba kazi moja tu ifanyike. Mwambie Jussa na Seif Hamad waombe Referundum, Wazanzibar wote wapige kura ya maoni -Kubakia ktk Muungano ama kujikata! na wajulishwe wazi hasara za kuvunja Muungano ni pamoja na wao wote kurudishwa Zanzibar (kama ilivyokuwa Sudan) na wataingia bara kwa Passport. Ajira na uwekezaji wao bara wataomba Work permit kama wageni wengine halafu tuone ni Wazanzibar wangapi wanaopenda kuvunja muungano. Sisi bara hatuna matatizo kwa sababu tunachukulia hawa waliopo hapa ni ndugu zetu na udugu huu hauwezi vunjika kwa kutumia uroho wa madaraka wa hawa.
 
Its look better than the US $ or even a sterling £ .



znzpesa.jpg
 
We zanzibaris have taken our own polls on this issue. This subject needs to be addressed effectively. By today 92% of Zanzibaris want out of this UNION. We do not need the Tibaijukas to run our lives. Both CCM and Opposition parties are incapable of delivering Zanzibar's independence for fear of being marginalised or even deregistered as a political party. As Zanzibaris get fedup with corruption and oppression, it's just a mtter of time before they revolt. We can amicably compromise on this matter and live in peace or otherwise.
 
Tunawaomba wazanzibari sana tena sana huu muungano tukiuvunja wafanye haraka kuja kuwachukua hao wapemba waliojazana kariakoo(including bhakresa) bila kumsahau huyo mzee wenu mwenye wake wawili anaofanya nao kazi kila kukicha plus huyu waziri wa mambo ya ndani asie na tija nahodha......mtuachie tanganyika yetuuuu plzzz.
 
passport.jpg Hichi ndicho tunachopigania wazanzibari,sisi ni wazanzibari na tunajifahari kuwa wazanzibari ulimwenguni kote,muungano tutauvnja tu,hauna maslahi kwetu,kwanini wazanzibari wanalazimishwa kubaki katika muungano wakati hatuutaki ? Iweje wazanzibari ndio wawe waathirika wa muungano halafu tunasema hasara za muungano nyinyi watanganyika munakuwa wakali ? Inaonyesha wazi kuwa hapa kuna siri kubwa lakini siri hizo ziko wazi sasa,na zimeanza kujitokeza moja ni rasili mali za zanzbar,pia kutumia muamvuli wa muungano kimataifa na kuiwacha zanzibar ikisambaratika kiuchumi.
 
Mimi sitaki muungano uvunjike, ila sijui mimi ni mjinga; sielewi kwa nini hakuna serikali ya Tanganyika, na baraza la mawaziri ri wa Tanganyika, na baraza la wawakilishi la Tanganyika. Mfano waziri wa nishati na madini ni wa Tanganyika na sio wa Jamhuri ya muungano. Lakini anaitwa wa Jamhuri ya Muungano. Bunge lipojadili bajeti ya wizara hii wazenji wanatakiwa watoke bungeni kwa sabau suala hili haliwahusu, lakini wanabaki, sijui kwa maslahi ya nani. Sielewi kabisa.
Bwana Sanga, sisi ni nchi ndogo sana kumudu hayo ma dual and multiple institutions mengi mengi (mabaraza ya mawaziri ya huku na kule na Muungano na mahakama za huku na kule na Muungano mabunge ya huku na kule na Muungano marais na makamu wa Rais huku na kule na Muungano, hatuwezi, tunaongeza ukubwa wa serikali wa bure, ni gharama! Kwa nini hatuna uchungu na nchi yetu jamani, tunataka tuwaachie watoto na wajukuu zetu nchi yenye madeni yasiyolipika?

Lakini nimependa sana ulivyoongea ukweli, kwamba hutaki Muungano uvunjike lakini hujui kwa nini, unajiona mjinga, that's a very cogent revelation, kwa kweli hakuna Mtanzania anaeweza ku articulate sababu za nchi moja kubwa kuungana na ka-wilaya (narudia, Unguja na Pemba ni ndogo kuliko Newala na Nachingwea mkoani Mtwara, the smallest region in Tanzania next to Dar-es-Salaam) halafu eti mkajifanya mna hadhi sawa, haiwezekani, hatutaki, haikubaliki kabisa, Muungano uvunjwe.
 
na sisi wahehe watuulize maana tumechoka kuwalimia mahindi we need our own country alafuuu hihi choko choko ya kujitengaaa kwa ajili ya mafuta ya kusadikika? mkiyakosa je mtarudi? acheni hizoo bwana tukichoka tutawatosa jumla
 
Katika hisabati kuna sheria moja inayosema kuwa kama "x" ni ndogo sana kuliko "y" halafu "x" ikaunganishwa na "y" basi muungano utakaopatikana utakuwa sawasawa kabisa na "y."

Vile vile katika hisabati ya numerali inayotumiwa na kompyuta inasema kuwa kama namba 1 ni integer, basi huwezi kuinganisha na 1.0 ambayo ni real number bila kufanya mabadiliko kadhaa ya katika vyumba vya kutunza namba hizo katika kompyuta.
 
Tatizo la referendum ni bendera fuata upepo na kuangalia nini kilichomoto wakati ule. Kupiga kura ni sura ndogo tu ambayo honyesha mtizamo wa wachache unavyoungwa mkono na 'the undecided' (Plato theory). Miungano mingi ni ya uongozi wa kisiasa uliopo madarakani unaoamua kwa 'faida' ya wengi. Upepo unaovuma sasa endapo referendum itafanywa, pande zote zitaunga kuuvunja, japo sina hakika uongozi wa kisiasa ko upande huo iwe Tanganyika au Zanzibar.
Uwezekano wakuvunja muungano kisataarabu upo na inawezekana kabisa, na kisha tukaishi na kushirikiana kulingana na matakwa ya wakati huo. Mfano mzuri ni nchi ya Czechoslovakia ilivyovunjika na kuwa Czech na Slovakia. Sasa zinashirikiana kupeleka majeshi yao nje under one command!!! Angalizo kuna miungano mingi tu inayopitia magumu ya identity kama sisi, k.m Ubelgiji. Flanders inataka kujitoa iwe huru na matokeo yake ni nchi ya Ubelgiji kushindwakuwa na serikali madhubuti kila uchaguzi unapofanyika. Matatizo ya tofauti za uwezo wa kiuchumi pia huleta mifarakano hii pale upande wenye rasilimali muhimu kuona haupati mgao stahili k.m UK na Scotland, waScot wanaamini kuwa England inawaburuza wanataka uhuru kamili. Binafsi napenda muungano uvunjike amicably kama Czech na Slovakia walivyofanya na si kama Sudan na Sudan kusini ilivyo sasa. Kwa referrendum Muungano wet tayari u kaburini, Tujadili tuachane vipi na mipaka hasa ya bahari pale economic zones zinapoingiliana iweje. There is always a sensible redivison if hot heads are cooled down.
 
Hivi kwa katiba iliyopo ya JMT, Zanzibar hawawezi kujitoa kwenye Muungano kama wanataka (i.e. "kuomba/kutoa talaka")? Kwa mfano, Zanzibar wanaweza wao wenyewe wakaitisha referendum na kuuliza wazanzibari kama wanataka kuendelea na muungano ama la....kama hawataki, kupitia BLW na baaade Bunge si wanaweza kujitoa tu? Maana naona kama kuna kuzunguka zunguka au pengine tunaweza kuita 'kisebusebu na kiroho papo'!
 
Tunawaomba wazanzibari sana tena sana huu muungano tukiuvunja wafanye haraka kuja kuwachukua hao wapemba waliojazana kariakoo(including bhakresa) bila kumsahau huyo mzee wenu mwenye wake wawili anaofanya nao kazi kila kukicha plus huyu waziri wa mambo ya ndani asie na tija nahodha......mtuachie tanganyika yetuuuu plzzz.


Mimi nafikiri wenye nafasi kubwa ya kuvunja muungano ni waTanganyika. Kwani wao ni wengi na kila siku wamekuwa watu wa kulalama kuwa Znz inawadhulumu kiuchumi.

Sasa nafikiri wakti umefika au mnanufaika nini nyie? au kuwadhulmu waZnz na kulinda amani zenu . Kwani nje ya Znz , Tanganyika hakukaliki kabisa Udini kila kona.

Poleni sana Wadanganyika
 
Strangely,Maalim Seif is trying to be clever by half, So rather than playing a game of bluff to force a break-up of the union (kama wanavyoongea in the backroom), I think he is just being fabulously cack-handed and on a collision course with his very staunchly unionist back-benchers friends in the CCM (yes Maalim's DNA is 100% CCM).
 
Back
Top Bottom