Refa Aisimamisha Mechi Hispania Kumfumania Mwizi Wake

Babuji

Senior Member
Nov 27, 2008
197
3
Ungefanyaje kama wewe ungekuwa refa ukichezesha mechi ya ligi halafu unasikia tangazo uwanjani kuwa kuna mwizi anaiba kwenye gari lako la kifahari?

Tukio hilo lilitokea nchini Hispania wakati wa mechi ya ligi daraja la tatu kati ya timu ya Jumilla na Puente Tocinos.

Refa Madrigal Soria aliisimamisha mechi hiyo kwenye dakika ya 63 baada ya kusikia tangazo uwanjani kuwa kuna mtu alikuwa akijaribu kuiba kwenye gari aina ya Audi A4 nje ya uwanja.

Baada ya kutangazwa kwa rangi na namba ya gari hilo, refa Soria aliisimamisha mechi hiyo na kuwaambia wachezaji "Hilo ni gari langu, hilo ni gari langu".

Rafa huyo aliwafuata waamuzi wa akiba na kuwaambia tukio hilo na kisha kutokomea nje ya uwanja huku washabiki uwanjani wakishangilia kwa nguvu.

Baada ya dakika tano kupita, refa huyo alirudi uwanjani na kuendelea na mechi.

Source: Nifahamishe.com
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom