Refa Aisimamisha Mechi Hispania Kumfumania Mwizi Wake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
3052990.jpg

Refa Madrigal Soria akitoka uwanjani baada ya kusikia kuna mwizi anajaribu kuiba kwenye gari lake Thursday, September 10, 2009 8:11 PM
Ungefanyaje kama wewe ungekuwa refa ukichezesha mechi ya ligi halafu unasikia tangazo uwanjani kuwa kuna mwizi anaiba kwenye gari lako la kifahari? Tukio hilo lilitokea nchini Hispania wakati wa mechi ya ligi daraja la tatu kati ya timu ya Jumilla na Puente Tocinos.

Refa Madrigal Soria aliisimamisha mechi hiyo kwenye dakika ya 63 baada ya kusikia tangazo uwanjani kuwa kuna mtu alikuwa akijaribu kuiba kwenye gari aina ya Audi A4 nje ya uwanja.

Baada ya kutangazwa kwa rangi na namba ya gari hilo, refa Soria aliisimamisha mechi hiyo na kuwaambia wachezaji "Hilo ni gari langu, hilo ni gari langu".

Rafa huyo aliwafuata waamuzi wa akiba na kuwaambia tukio hilo na kisha kutokomea nje ya uwanja huku washabiki uwanjani wakishangilia kwa nguvu.

Baada ya dakika tano kupita, refa huyo alirudi uwanjani na kuendelea na mechi.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3052990&&Cat=6
 
Kudadadeki!! ataningekuwa mimi ningewahi haraka nje ....sasa kwanini hao wanausalama wasingetoa msaada wa kumkamata huyo kibaka?!
 
Back
Top Bottom