Redio Free Afrika, magazeti na Kiswahili

Unajua maana ya majungu wewe au umekariri! Hoja hapa ni usahihi wa lugha na sio lafudhi. Kama amekuwa affected kiasi hicho basi hiyo nafasi haimfai maana ata affect ňa wengine kama ilivyo ku-affect wewe.
Mtu analeta hoja ya maana wewe unaita majungu! Eti yasiyo na maana, kwani kuna majungu yenye maana! Ulipewa masikio mawili na mdomo mmoja ili usikilize zaidi kuliko kuongea.

Sikiliza ujifunze punguza ujuaji...
bwana mdogo si vibaya ukienda kwenye ofisi za redio free africa kuileta hapa ni majungu kama nilivyosema hapo juu.....
 
Immaculate Kilulya bomba sana. Nadhauri RFA wawe na format ya kusoma magazeti siyo kila mtu kivyake. Ila Imaculate Kilulya pamoja saana.
 
Hivi hii radio bado ipo? Maana Tabora ni miezi takriban mitatu haisikiki.
 
Mbona anasoma vizuri tu? Tatizo nini? Leo tarehe 08 Julai nimemfuatilia Star TV na nimeelewa. amesoma vizuri tu. au ameimprove?
 
Mleta mada unatamani kiswahili fasaha? redio (free afraca) je unaamini ktka kukosea? anza upya hata ww hujatimia
 
Hivi hii radio bado ipo? Maana Tabora ni miezi takriban mitatu haisikiki.

Ipo mkuu ila menejimenti sijui wapoje, inaweza kupotea kwa miezi hata 3 kama usemavyo, Iringa haikua hewani kwa zaidi ya miezi 4 ikarudi mwezi April 2015 na jana (julai 7) ikakata tena mpaka sasa
BBC swahili asubuhi naisikia kupitia radio one na one local radio ya hapa (Nuru fm 93.5) ila magazeti ndio tunayakosa
 
CC: Mhariri Amos Gomba tubadilishieni Mbezi arekebishe kwanza matamshi masikio yanawasha kumsikiliza 'l' na 'r' zilishamshinda kutofautisha...
 
Ajabu ni kwamba uongozi ama wahariri hawachukui hatua!! kama umeshaona mtangazaji fulani ana tatizo fulani, kwa nini asipewe mahala ambapo hapahitaji kusoma sana!!!!!!! au ashauriwe awe mwandishi badala ya kutangaza!!

Kama hawezi kusoma na kutamka vizuri uandishi wake utakuwa mbaya zaidi.
 
Ajabu ni kwamba uongozi ama wahariri hawachukui hatua!! kama umeshaona mtangazaji fulani ana tatizo fulani, kwa nini asipewe mahala ambapo hapahitaji kusoma sana!!!!!!! au ashauriwe awe mwandishi badala ya kutangaza!!

ni kweli issue si laaafudhi! maana kama ingekua hivyo then kina Ufoo saro na Monyo au Maratu wangeisha lalamikiwa!
 
Mimi sijawahi kumsikia Zuberi msabaha akisoma magazeti au taarifa ya habari.

Namkubali sana Ahmed Ally kwa kusoma magazeti huko njema.
 
Kuna jamaa huwa ananichekesha sana anasema wamejaa kama pishi la mchele.
Alafu anamalizia makinika nasi.
Lakini uchambuzi wao ni mzuri sana mm naupenda sana.

Wanaudhi pale utakapokuwa umeamka ukawasha karadio kako alafu unasikia tunashidwa kuwapata wa darsalamu hivyo tusikilize kwanza burudani....khaaaa
 
Kuna mtangazaji wa kitambo TVZ, niliwahi kumuona akisoma taarifa ya habari, miaka ya 90, ile kutamka zanzbar yeye anasema zyanzyibar, nilipata hasira ajabu.
 
Mimi ni aaahhhhhmed ally nikiwa na binti..... HHahhahaa jamaa ananifurahisha sana, hasa kwen habari za michezo
 
kuweni waungwana bana hayo ni mambo ya lafudhi tu na ndo maana hata kiingereza kinatofautiana kutokana na mahali kinapozungumzwa so la muhimu pale ni kwamba ujumbe unafika kwa wakati muafaka acheni kuwa wakosoaji wa kila kitu as if nyie ndo waswahili wa kweli.
Tafadhali usichokoze wafia lugha ,ndugu yangu sifa ya msingi ya mtangazaji ni ufasaha na usanifu wa lugha anayoifanyia kazi,kama hiyo ndio lafudhi yake basi ni kigezo tosha cha kumweka pembeni ,lafudhi inalenga kwenye matamshi kisauti si muundo wa neno zima-unaweza kusema kwa lafudhi ya kisukuma,kigogo,kingoni neno RAHISI na ikawa fasaha ,lakini huwezi ukatamka neno LAHISI kwa maana ya RAHISI ukadai ni fasaha kwa kuwa tu una lafudhi ya kingoni n.k!
 
Kaka hata siku moja huwezi kuchenji lafudhi ya mtu,. Na ndo maana hata katika mada ya Asili ya kiswahili kuna mada ndogo iitwayo lafudhi. Inafahamika wazi kabisa kuwa kiswahili kimetokana lugha za kibantu. Hivo bas kiswahili cha mngoni na kiswahili cha mangi wa arachuga lazma viwe na lafudhi tofauti. Hebu angalia lafudhi ya kiswahili cha mzanzibar unaweza mfananisha na mswahili wa tarime? Ndo maana ktk kiswahili tunasema kuna sabab ambazo znamfanya mtu asiwe mahiri katka lugha ya kiswahili.; mfano, athari ya lugha mama, mfano ukikutana na mnyakusa aliyekulia unyakyusani badala ya kukwambia, Naomba viatu vyangu. Atakwambia, Naomba fiatu fyangu. Kwake yeye yuko sawa na kumrekebsha huwez sabab keshaathirika na lugha mama. Hivo bas naomba nihitimishe kwa kusema Christina Mbezi co anapenda kusema hvo bali ndivo alivo na kumbadilisha huwezi. Na hiyo haimaanishi lugha ya kiswahili haitakuwa,, bro kwani wewe unauhakika kuwa huwa unaongea kiswahili kwa ufasaha bila kuharibu sarufi ya kiswahili hata siku moja? Imposible.
Mkuu nadhani kuna kitu hujakifahamu hapa,katka lugha yeyote mtu anaweza kuongea kwa lafudhi yeyote ile na akawa hana makosa katika usanifu au ufasha wa lugha,na lugha yeyote haiundwi kwa lafudhi tofauti japo lafudhi tofauti zinaweza kutumika,mfano wako utakuwa unamaanisha "lahaja"si "lafudhi" mchina ,mzungu, wanaweza kuongea kiswahili fasaha katika lafudhi zao bi maana tuna kiswahili kwa lafudhi ya kichina lakini kamwe hatuwezi kuwa na kiswahili chenye lahaja za watu wa mataifa hayo !kwa mifanoyakohiyo hao wannyakyusa tutawaelewa nini wanamaanisha pia hatuweza kumwajiri mnyakyusa mwenye lahaja za kinyakyusa kuwa mtangazaji tunataka mnyakyusa mwenye lafudhi ya kinyakyusa!
Yote juu ya yote mwenyewe umekiri kuwa lafudhi mi naongezea na lahaja zina athiri umahiri wa lugha ,sasa hapo hata wewe umeafiki kuwa huyu bi dada hafai kuwa mtangazaji na siye wakosoaji hata kama tunakosea sisi si wanahabari kwa hiyo hatuwezi kuiathiri lugha.
 
Back
Top Bottom