Redio E-Fm wanapika data kujiongezea ubora, ukweli ni huu

Wenye akili zao wanajua wazi kwamba EFM inaendeshwa ki-propaganda! Mwanzoni walianza kutembeleea nyota ya Lady Jay Dee hadi pale ilipokuja kufahamika kwamba Jide hausiki!

Wakati wanatembelea nyota ya Jide ilikuwa ni kipindi cha beef kati ya Jide na Clouds... beef ambalo Sugu nae akaingia kati! Kwahiyo haters woooooote wa Clouds, wakaanza ku-support "radio ya Kamanda Jide...!" aliyekuwa anapata support toka kwa Kamanda Sugu! Siasa za EFM hapa ndipo zilianzia! Wale wanaojifanya hawasikilizi Clouds (lakini utashangaa leo mtu anahoji "yaani hadi leo unasikiliza Clouds" baada ya siku mbili tatu huyo huyo anaanzisha mada ya kuponda mtangazaji fulani katika kipindi cha Clouds... mtu unashangaa kamsikiaje wakati hasikilizi Clouds) ndio wakaanza kuwa wapiga kelele in favor EFM!!!

Inabidi uwe ni yule jamaa mmoja katika wanne ndipo uweze kuamini EFM ina wasikilizaji wengi kuliko Clouds!!!!!
Acha kupotosha Uma, kipindi cha vinega na Antivirus mixtape wala EFM haikuwepo. Kipindi kile ilikuwa inatumika times fm mkuu.
 
E fm hawa jamaa ni wabunifu sana aisee....kwa mtazamo wangu ndo radio inayoongoza kusikilizwa mjini dar....
 
RFA naamka nayo,clouds michezo TBC FM kama wanatangaza mpira na niko mbali na runinga otherwise RFA na Clouds ndizo radio zangu
 
Acha kupotosha Uma, kipindi cha vinega na Antivirus mixtape wala EFM haikuwepo. Kipindi kile ilikuwa inatumika times fm mkuu.
We jamaa vipi? Hujui kusoma, au? Wapi nimesema suala Antivirus? Kwahiyo kusema kwenye bifu ya Jide na Clouds ambayo Mr. II akaingia kati; kwako wewe hiyo ni issue ya Vinegar na Antivirus?
 
We jamaa vipi? Hujui kusoma, au? Wapi nimesema suala Antivirus? Kwahiyo kusema kwenye bifu ya Jide na Clouds ambayo Mr. II akaingia kati; kwako wewe hiyo ni issue ya Vinegar na Antivirus?
Mbona unachanganya madesa, bifu ya jide na clouds imeanza mwaka gani?? Na E fm imeanza mwaka gani??
 
Kwa wakazi wa uswazi hata hatutaki ligi kama unabisha pita mtaa kwa mtaa dsm usikie e fm inavyochana mawimbi ila ww unaetembelea ki ist endelea tu kubishana na ukweli
 
mamia ya wasikilizaji mh!
mimi ntachojua wamemshtaki PJ kwa kuvunja mkataba.. alipe fidia mamilioni
Hayo mamilioni PJ atayapata wapi hata akiuza spanner mkononi yake hawezi pata hata milioni moja,wamuache PJ wa watu aendelee kupata urabu pale kwenye kibaa cha machangu wa Mikocheni B nyuma ya Clouds Mikocheni,pale anachoropoka tu kutoka studio kama anaenda dukani kumbe anakuja kamata maji ya Mchikichini ,nadhani EFM walikuwa hawampi nafasi ndio maana kaona isiwe taabu.
 
Acha kupotosha Uma, kipindi cha vinega na Antivirus mixtape wala EFM haikuwepo. Kipindi kile ilikuwa inatumika times fm mkuu.
Ni kweli Vinega enzi zile walikuwa wapo bega kwa bega na Times FM.. Na hata ile show yao iliyovuruga mapato ya Clouds , Times Fm ndio walioirusha hewani..
 
Thatha mleta mada, umetumia kigezo gani kusema ulizoleta za ukweli na za wenzako zilipikwa!
Hapo kwenye hizo data, wasikilizaji waliohesabiwa ni Watanzania nzima na kwa upande wa Efm ni wasikilizaji wa Dar pekee. Kwa mfano, siku ya J3 (0600-0800) kwa kuzingatia taarifa za kwanza kwenye jedwali, Clouds walikuwa na wasikilizaji 1,288,000 (Tanzania nzima) wakati Efm (Dar pekee) 570,000.
Hii ina maana kama iwapo Clouds ina wasikilizaji wengi kwa Tanzania, Efm bado ni radio pendwa kwa wasikilizaji wa Dar. Kama iwapo Efm wakiongeza masafa, sidhani kama Clouds itaendelea kulitawala soko la wasikilizaji wa Tanzania.
Hata hivyo napata mashaka sana na hizo idadi za wasikilizaji, hivi ilikuwa ni 1,288,000 kamili na hakukuwa na 1,284,971? Au 570,000 na kulikosekana 568,523?
Hizo hesabu zilikuwa zinakadiriwa au zilipikwa, yaani hiyo mashine iliyotumika kukokotoa haitoi idadi kamili na ilikuwa inakokotoa namba kwa makadirio na kuzikaribisha (round-off to nearest hundred)? Yaani hiyo teknoloji imeshindwa kutoa idadi halisi!?
 
Clouds kitu gani ,mikelele ya Mbwiga nani anaitaka siku hizitunaenda EFM na mwendo wa Bwakila na Mkude Simba.
Nani wewe !Bwakila!Bwakila ndio nani,mtoto wa Mkude Simba ahaaa Bwakila baba yako kaenda wapi,hebu ongea kiswahili wewe .
 
Cha kwanza cha kushangaza ni kwamba hiyo taarifa ya E. FM imegawanya (weekly) data in 3-hour blocks wakati Geopoll wanagawanya (daily) data zao in 2-hour blocks. Hiyo tayari ni makosa. Haiwezekani.
 
market strategy ya Efm, inamfanya msikilizaji ajihisi ni sehemu ya kipindi, muda mwingi wanamgusa yule mtu wa kipato cha kawaida, kule upande wa pili wanajifanya wamarekani. ndo hapo wanapoisoma namba. mama ntilie, bodaboda, daladala majumbani uswazi wote wameteka.
 
Sio Kweli Mkuu nadhani unatakiwa kujua kuhusu Kazi za Geopoll
Kwani GeoPoll hawawezi kutumika kama wanavyotumika TWAWEZA? Kwa namna EFM wanavyofanya kazi sioni hata sababu ya wao kupika takwimu, kwani wanakubalika sana. Simaanishi wanaweza wasipike takwimu, bali sioni sababu ni kwanini wapike. Angalizo langu ni kwamba, tusiwaamini GeoPoll kwa asilimia 100! ni lazima tujiongeze..
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom