REDET na Synovate wako wapi baada ya uchaguzi?

Synovate na REDET mbona hawafanyi utafiti juu ya mgawo wa umeme ili tujue chanzo ni nini? JK tayari ameshatuambia kuwa Ngeleja si wa kulaumiwa! Eti "Ngeleja hajasababisha ukame!" Tumechoka sana kusikia juu ya "ukame," "megawati," "umeme wa dharura," nk!Hawa Synovate na REDET wanafanya utafiti juu ya mambo ya siasa tu na hawajali matatizo yanayoikumba nchi yetu! Nawashauri basi "wajivue gamba," waache kuyabeba Magamba wakati wa uchaguzi tu, wafanye tafiti zinazolenga kutatua matatizo ya nchi yetu!
 
Kwa hali iliyopo sasa ndio hizi taasisi zingepaswa kuwa zinatoa majibu ya nini hisia za watu juu ya utawala uliopo na mwenendo mzima wa mambo katika nyanja zote,zipo kero nyingi ikiwemo mfumo wa uendeshwa wa bunge,mfumuko wa bei,maisha magumu na mambo yanayofanan na hayo,ndio kipindi hizi taasisi zingekuja na majibu ya kiutafiti kuonyesha njia mbadala wa kero zinazowakabili wananchi na taifa kwa ujumla.
Ina maana hizi taasisi zinafanya tafiti zao wakati wa uchaguzi tu?hapo wanataka watu wajenge hisia gani kwa hizi taasisi?maana kwa sasa hata kusikika wala viongozi wao kutoa matamko kama ilivyokuwa wakati wa uchaguzi mkuu
 
Haaaa haaaa! Nilifikiri wewe ni BENSON BANA ili utupatie majibu ya REDET kuhusu hali mbaya ya kimaisha kwa sasa!
 
Haw wanafanya research za udaku tu. Hawa hawafanyi research bila kupewa hela kwanza. Ukiwapa pesa wana cook figures kama unavyotaka wewe period.

Kama wanabisha mbona hawafanyi research za hali ya kisiasa sasahivi maana wafadhiri wao hawako interested na hayo matokeo kwa sasa mpaka 2014/15
Utaona ndo wanaibuka sasa na figure zao za kupika zikimfurahisha mfadhiri wa research hiyo.

Lakini watambue kuwa hizo figure za kupika hazitasaidia kitu maana sasa ukweli uko wazi kila kona ya nchi hii.
 
Aibu kubwa ni kwa hawa wanaojiita wanataaluma. Akina Bana.

Mimi nimekuwa nikisisitiza kwamba kwa tabia ya binadamu ni rahisi kugundua uwezo mdogo wa kufikiri kwa kuangalia uso wa watu kama akina Bana. Nikiwaangalia ktk TV sioni dalili ya fikra nzuri. Nasikitika kama hawako hivyo lakini nawaona kama hawana uwezo wa kufikiri yaliyo mema.
 
Mpango wa Elimu ya Demokrasia wa Chuo Kikuu Dar es Salaam walikuwa na utaratibu wa kutoa ripoti ya kura za maoni, kama sikosei, kila robo mwaka. Lakini kwa muda mrefu sasa sijaona wakifanya hivyo. Nadhani tangu baada ya Uchaguzi Mkuu uliopita hawajawahi kufanya hivyo. Sijapata nafasi ya kuwauliza Redet wenyewe, lakini nadhani kuna watu humu wanajua ni kwa nini hali imekuwa hivyo.

Mwenye taarifa naomba atujuze kunani huko Redet mbona hawaifanyi kazi hii tena?
 
Iko kibiashara zaidi mkuu!

Kama unataka wakufanyie utafiti waite tuu wako huru mradi una mifeza.
 
Iko kibiashara zaidi mkuu!

Kama unataka wakufanyie utafiti waite tuu wako huru mradi una mifeza.
Mi nilidhani walikuwa wakifanya tafiti zile kama sehemu ya kukuza demokrasia nchini.
kama wako kibiashara, ni nani alikuwa akiwalipa kufanya tafiti zile za awali?
 
Wamepigwa Mkwara na wafadhili wao kwa ajili ya uchakachuaji wanaoufanya kwenye matokeo kura za maoni, Na wakuu wake ni vipenzi vya JK na CCM kwa hiyo kufanya utafiti na kupublish ukweli hawawezi so wamebaki kuduwaa tu...

Hawana jipya..
 
Mi nilidhani walikuwa wakifanya tafiti zile kama sehemu ya kukuza demokrasia nchini.
kama wako kibiashara, ni nani alikuwa akiwalipa kufanya tafiti zile za awali?

Mara ya kwanza walikuwa wakitumia hela ya wafadhili. Wafadhili walipogundua kuwa taasisi hiyo imebadilika kiutendaji kutoka taasisi ya utafiti na kufanya kazi kama taasisi ya propaganda za kisiasa ya CCM, kuanzia mwakajana wafadhili wamesimamisha misaada yao. Sasa hivi hawana fedha, na siamini kama CCM au serikali inaweza kuwapa. Nadhani baada ya muda si mrefu itakuwa ni historia tu kuwa kulikuwepo na taasisi moja iliyokuwa ikiongozwa na Prof. Mkandara akisaidiwa na kilaza mnafiki Bana, mwanzoni ilifanikiwa kuwadanganya wafadhili lakini baadaye -------
 
Genge la wahuni hili,ni waporaji wa demokrasia tena wafe kabisa sitaki hata kuwasikia
 
Mara ya kwanza walikuwa wakitumia hela ya wafadhili. Wafadhili walipogundua kuwa taasisi hiyo imebadilika kiutendaji kutoka taasisi ya utafiti na kufanya kazi kama taasisi ya propaganda za kisiasa ya CCM, kuanzia mwakajana wafadhili wamesimamisha misaada yao. Sasa hivi hawana fedha, na siamini kama CCM au serikali inaweza kuwapa. Nadhani baada ya muda si mrefu itakuwa ni historia tu kuwa kulikuwepo na taasisi moja iliyokuwa ikiongozwa na Prof. Mkandara akisaidiwa na kilaza mnafiki Bana, mwanzoni ilifanikiwa kuwadanganya wafadhili lakini baadaye -------
Alaaa, kumbe. Let me take it from here
 
Back
Top Bottom