Elections 2010 REDET kumshitaki Dr. Slaa?

Vawulence

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
1,928
2,101
Makamu mwenyekiti wa REDET Dr. Benson Benza amelalamikia kitendo cha mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA Dr. Wilbrod Slaa kudai kuwa yeye ni mshauri wa Rais aliyemaliza muda wake Bwana Jakaya kikwete (for the sake of education simwiti doctor). Pia amekanusha madai kuwa yeye ni mteule wa rais na kudai kuwa nafasi yake si ya kuteuliwa.
Katika mahojiano yaliyofanyika Star tv ya jijini Mwanza,Dr. Benson alizungumzia matokeo ya REDET na kudai kuwa matokeo yale yalikuwa ni ya muda mfupi tu. Pia alidai kuwa haikuwa sahihi kwa vyama vya siasa kulaumu matokeo ya utafiti ikiwemo ccm kwani utafiti wao ni wa kisayansi na machapisho yao hutafutwa na vyuo vya Oxford na Havard.
Katika hali iliyoonesha kuwa anataka kumshitaki Dr. Slaa , Dr. Benson alisema "Nilikuwepo Mwanza wakati Dr. Slaa aliposema kuwa mimi nafasi yangu nimeteuliwa na rais Kikwete na pia mimi ni mshauri wa rais.....ningekuwa mwanasiasa ningelizungumzia hili jukwaani ila kama political analyist NITALIWEKA HILI SAWA BAADA YA UCHAGUZI."


MY TAKE

Ataliwekaje hili sawa?
 
Itaiweka sawa baada ya matokeo ya redet kuwa sawa na matokeo ya uchaguzi
 
Anasikilizia upepo nani atachukua nchi..asije akamwaga ugali wenzake wakamwaga mboga...
 
Chizi, Jizi, Hilo Haliwezi kuweka lolote sawa, Kwanza hana uhakika kama JK atashinda thats y anasubiri matokeo.
Anaweza kufungua kesi kumbe anamshtaki Rais ajae.
 
hana lolote huyo...ataweka sawa nini!!!angedhubuti kusema lolote angeona mjenga hoja atakavyompasha!!!CHADEMA HOYEEE...DR W.SLAA HOYEEE
 
Si mwanasiasa? Alikuwa nfanya nini pale kama si kujaribu kufanya kazi ya CCM kuonyesha kwamba matokeo ya REDET yalikuwa sahihi? Nilimsikiliza nikaona hana maana. Asubiri Jumapili ajue ataliweka vipi sawa
 
Ni Jumatatu ijayo, kelele zote hizi zitafikia mwisho wake! Tutajua kama Redet na Synovate wako sawa ama online poll (iliyopatwa kupelekwa gereji kutengenezwa) ndiyo ilikuwa sahihi!

Tulizeni mizuka na punguzeni mshawashwa!
 
Huyu anastahili kufungwa jiwe la kilo 50 na kutoswa baharini hana faida yoyote, unapoona msomi wa kiwango kile akifanya mambo ya kijinga basi huyo hastahili kuishi tena
 
Back
Top Bottom