Re: Mwakalebela amshinda Mizizi mahakamani

Lutala

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
848
103
Lile sakata la kesi ya rushwa iliyokuwa inamkabili Fredrick Mwakalebela mahakama ya mkoa Iringa, limehitimishwa leo baada ya Mwakalebela kumshinda tena mwanasheria wa TAKUKURU mahakamani.

Kesi hiyo ilirudishwatena mahakamani baada ya Bwana Imani Mizizi (TAKUKURU) kupinga hukumu iliyotelewa ya kumwachia huru ndg. Mwakalebela.

Kwa ufupi tunampongeza Mwakalebela kwa kuwashinda waliombambikia kesi. Na tunawaonya Takukuru kupitia kwa wanasheria wao uchwara kuacha kubambikia kesi watu
 
siku zote truth prevail na sio huu tu mambo mengi tu ya ukweli yatakuja kuwa wazi dhidi ya propaganda tunazolishwa

Pukudu@ Ilkiding'a, Arusha
 
Takukuru ndo nini???????????????????????????????????????????????????????????????

Takakuru yetu ina:mimba::mimba::mimba:
 
siku zote truth prevail na sio huu tu mambo mengi tu ya ukweli yatakuja kuwa wazi dhidi ya propaganda tunazolishwa

Pukudu@ Ilkiding'a, Arusha

Ipo right ndugu. Maana hii serikali imezidi kubambikia watu kesi kwa maslahi yao
 
Ule ulikuwa ugomvi wa ndani ya CCM tu. Na hizi kukuru kakara za Imani mizizi ni sarakasi tu za kuwadanganya watu. Fikiria Mwakalebela angehamia Chadema; sasa hivi angekuwa amehesabiwa mvua kadhaa pona yake ni kuwa alikubali kumpigia kampeni Mtu wao Mbega. Ziko wapi kesi za akina Mama Sitta, Joseph Mungai?
 
Kwani ilikuwa kesi ya rushwa au kumzuia asigombee? Si tayari uchaguzi umepita. Muda wa kumwachia umefika ila bahati mbaya waliyemtaka ashinde kashindwa!
 
Yule Norman Sigalla ambaye ni DC wa Hai alikamatwa na Takukuru akiwahonga wapiga kura huko wilaya ya Makete lakini kesi yake ikazimwa na anaendelea na uDC wake!! Mtu kama huyo kweli anaweza kupiga vita wala rushwa kama yeye mwenyewe ni mtoa rushwa? CCM ndio imetufikisha hapo!!
 
Hiyo haikuwa kesi ya rushwa ilikuwa hatua ya kwanza ya kumuokoa hawa** yao Monica mbega, hawakujua kulikuwa na kizingiti kingine Mch. Msigwa
 
Back
Top Bottom