Re: Lema atangaza kampeni mpya

Mar 28, 2011
11
0
Mbunge wa Arusha mjini mh Godbless Lema ametangaza kampeni mpya ya kuleta mabadiliko katika jamii.
Kampeni hiyo aliyoipa jina la 'CHANGE ON FINGERS' inalenga kuwafanya vijana kushiriki kuleta mabadiliko katika jamii kupitia vyombo vya mawasiliano kama vile simu na kompyuta,ambapo zaidi ya mawasiliano ya kawaida watatakiwa kutumiana ujumbe wenye kuleta mabadiliko kwa manufaa ya jamii ya kitanzania.
Lema aliyatamka hayo jana wakati akizindua tawi la CHADEMA chuo kikuu cha Dodoma skuli ya Elimu.
Aliwataka wengi wajiunge na mitandao ya mawasiliano kama vile facebook na Jamii forums kwani kupitia huko wataelimishana kwa kasi zaidi na kuleta mabadiliko katika jamii.
 
Asante sana kamanda wa machalii Arusha! Change is coming soon!
 
Asante sana kamanda wa machalii Arusha! Change is coming soon!
Duh! Hiki kweli kizazi cha digital, taifa likiongozwa na viongozi machalii cjui litaongozwa kuelekea wapi?. Lakini natamani kuona hiyo hali.
 
Ukiangalia km bahrain na nchi zingine zaa kiarabu zinazo taka mabadiliko, kilichowasaidia wote kuwa kitu kimoja ni mtandao kama huu anaousema GL(Good Liberty), kwakutumia mitandao tutaweza kuwa kitukimoja kwa faida ya wote, nakuweza kulikomboa taifa letu, toka katika makucha ya mafisadi.
 
Back
Top Bottom