Wana jamvini ripoti pokeeni.
Kwanza kabisa nashukuru sana kwa ushauri wenu-yote yenye mitazamo tofauti, kwa kweli imeniwezesha kujitazama upya kama tatizo na si kumwangalia mtu mwingine. UAMUZI NIMECHUKUA. Kwa wale wote walionishauri chapa ilale nawashukuru sana lakini nasikitika kuwataarifu kuwa ushauri wenu nimeuweka kapuni, wale wenye ushauri tofauti na huo wenye malengo ya kuheshimu ndoa yangu, familia yangu, watoto wangu na mke wangu nawashukuru maradufu na huo ndio ushauri nilioamua kuufuata katika mazingira yafuatayo;
Cheers!

- Kwanza kabisa, sitamtimua/kumfukuza kazi katika mazingira ya hisia za kumtega bosi wake. Kwa ushauri wenu nimeweza kujitazama zaidi na kuamini katika kushinda majaribu
- Nimemuita na kumkanya juu ya mitego yake isiyokuwa na tija, pia kuongea nae kuhusu maisha kwa ujumla na maisha yake. Seriously nimemkanya na kumuamuru aniheshimu kama muajiri wake na si vinginevyo. Mkutano huu nimeufanya nikiwa na mdhamini wake wa kazi ambaye ilibidi nimuite aje tuweze kuliongelea hili tukiwa wote. Sikumshirikisha wife katika hatua hii kwa sababu sipendi apate maumivu yoyote juu ya mapenzi hasa kwa wakati huu, pia nilihisi akijua hata kwa nia njema lazima angedemand kumfukuza kazi, jambo ambalo niliona kwamba si haki katika hatua hii ambayo inaongozwa na hisia. Katika kuongea nae alishindwa kukiri au kukataa, lakini akaomba sana msamaha kama alikuwa katika mienendo inayokwaza
- Nimempatia muda wa probation wa miezi mitatu-katika muda huo nitakuwa namchunguza tabia na mienendo yake, akikengeuka kazi hana on the spot na hilo nitalisimamia mimi mwenyewe katika namna ninayojua kuhakikisha adhabu inatekelezeka
- Katika kuongea nae, tulimuuliza juu ya future ya maisha yake badala ya kutegemea/kuamini katika kupata mwanaume ndio maisha yaende, naye alisema anapenda kupata msaada wa kuendelea kielimu-elimu ya Hotel Management. Maamuzi niliyofikia, akimaliza muda wa miaka mitatu bila matatizo, nitamgharamia elimu hiyo aliyopendekeza au nyingine kwa kipindi na wakati husika
Cheers!