Re: International Passport

Straight corner

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
385
132
Poleni na majukumu wakuu!
Nimeona ni busara nirejeshe matokeo kama nilivyokuja kuomba msaada hapa jamvini (wale mlioweza kusoma thread "International Passport") ukiachilia mbali kuwa ni muda mrefu kidogo umepita na hii ni kutokana na majukum ya hapa na pale!
Wana JF nilienda kufanya mchakato wa Pass 24 May 2011 (Jumatano) nikiwa na documents zote na nikafanikiwa kuitia mkononi 30 May 2011 (Jumatatu) ambapo ni takribani siku 5. Kufikia Ijumaa namba ya Pass ilikuwa tayari imeshajulikana ila niliambiwa Pass yenyewe isingeweza kutolewa kwa sababu zisizoweza kuzuilika. Hii ni baada ya kufanya ufuatiliji wa karibu na kwa taratibu zinazotakiwa.
Kwa ujumla nilipata Pass yangu japo si kwa muda ambao ungefaa kutatua tatizo langu!
Nawashukuru wote kwa misaada yenu wakuu.
Nawasilisha!
 
Back
Top Bottom