Re: Gharama ya nauli kuanzia ijumaa ijayo ni 500

Gudboy

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
867
77
kuna habari zisizo rasmi ambazo zinadai kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta chama cha mabsi kina mpango wa kuongeza nauli kwa rout fupi kuwa sh 500 kuanzia ijumaa ijayo. Habari hii nimeiskia kwenye kituo cha radio cha clouds fm je yeyote mwenye data kamili jamani. Maana maisha kwa sasa yanazidi kuwa magumu na hii ni kutokana na kupanda kwa bei za vyakula pamoja na vitu vingene kama mafuta
 
Kweli kuwekeza kwenye daladala ni biashara kichaa. Mpaka leo nauli haijavuka 500? Ukweli ni kwamba hata serikali yenyewe haiwezi kuendesha huduma hii kwa kutoza 500!
 
No comment!!
Lakini mkuu ina maana wewe hujawahi kupanda dala dala? Kwasababu ulivyosikia kuawa nauli bado haijafiki 500. umepata kwmshangao kidogo.
 
cha ajabu ni kwamba, mimi hapa ulaya, natumia nauli ndogu kwa mwezi kuliko ningetumia hapo bongo...nikiwa na euro 32 tiketi yangu ya mwezi, ndo imetoka hiyo...lakini hapo bongo, ukianza kuunganisha mabasi matatu au manne kwa siku kwenda na kurudi, unaweza kumaliza laki mbili kwa mwezi nauli tu...haya maisha magumu watz tutajikomboa lini?
 
Kwa kipato kipi alichonacho mfanyakazi wa kima cha chini?
kuna habari zisizo rasmi ambazo zinadai kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta chama cha mabsi kina mpango wa kuongeza nauli kwa rout fupi kuwa sh 500 kuanzia ijumaa ijayo. Habari hii nimeiskia kwenye kituo cha radio cha clouds fm je yeyote mwenye data kamili jamani. Maana maisha kwa sasa yanazidi kuwa magumu na hii ni kutokana na kupanda kwa bei za vyakula pamoja na vitu vingene kama mafuta
 
Kweli kuwekeza kwenye daladala ni biashara kichaa. Mpaka leo nauli haijavuka 500? Ukweli ni kwamba hata serikali yenyewe haiwezi kuendesha huduma hii kwa kutoza 500!

Hapo umenena! Serikali inawaonea sana wenye daladala, gharama za uendeshaji ni kubwa sana ukifananisha na nauli, biashara haiwezi kujiendesha ipasavyo. Ndo maana mabasi hayatoshi na ni mabovu.
Na serikali ikija na hiyo Rapid Transit itabidi ipandishe bei au itumie kodi kufidia gharama.

Swala la wananchi kuwa na kipato kidogo haibadilishi gharama za kuendesha biashara.
 
Jamani swala kubwa tunalikosa sisi wananchi ni kufikiri.

Kupandisha nauli si suluhisho, kwani mpaka sasa hivi mfumo mzima wa daladala ni mfumo wa kijima.

Mtu unamiliki daladala, hujui matumizi yake halisi, haumlipi dereva wala konda, unakwepa kodi halafu unataka hesabu. Kwa hali hii hawa madereva na makonda ndio wanaopanga nauli ili wajilipe na matajiri koko (nawaita koko kwa sababu hawana elimu juu ya usafirishaji) waendelee kuwaaminisha magari yao.

Napinga kupanda kwa nauli, napinga tena napinga!
 
Back
Top Bottom