Re: Ajabu madodoso ya sensa yaisha,zatumika photocopy!

buyegiboseba

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
535
145
Nimemaliza kuhesabiwa kama dakika moja iliyopita,karani aliyenihesabu ametumia dodoso lililotolewa photocopy, amedai wameambiwa yameisha na wamepewa kopi.

Ni hapa manisapaa ya Lindi. Je hii ni halali kutumia dodoso kopi wakati dodoso zina serial number?

Kiukweli hali hii imenigutua sana na kuwa ha hofu na ufanisi wa zoezi hili.
Wadau mnasemaje juu ya hili.
 
Mkuu,ukistaajabu ya musa... Hii ndio tanzania yetu. Kama kawa watu washapiga mpunga wao wametulia.

Wewe unashangaa photocopy ya dodoso? Je sisi tuliohesabiwa kwa kuandikwa kwenye 'vinotibuku' vile vidogo tusemeje? Ndipo tulipofikia ingawa haizoeleki.
 
si zoezi linafanyika ili mradi tu limalizike...mwisho wa siku watakuja jikuta watanzania waliohesabiwa ni milioni 20 tu
 
Pamoja na mbwembwe zote tumejiandaa vya kutosha...kila kitu kiko tayari! kweli dhaifu,authentic ya taarifa hizi za copy au za vinotibook inatia shaka,kuna uwezekana tukapata takwimu za kupikwa
 
Nimemaliza kuhesabiwa kama dakika moja iliyopita,karani aliyenihesabu ametumia dodoso lililotolewa photocopy,amedai wameambiwa yameisha na wamepewa kopi.
Ni hapa manisapaa ya Lindi
Je hii ni halali kutumia dodoso kopi wakati dodoso zina serial number?
Kiukweli hali hii imenigutua sana na kuwa ha hofu na ufanisi wa zoezi hili.
Wadau mnasemaje juu ya hili.

Zoezi zima litaighalimu serikali
karibu Billion200
 
Usishangae huko, kunajamaa huko Mpwapwa walipewa madodoso marefu kumi tu katika eneo lenye zaidi ya kaya mia moja, baada ya masaa mawili wakawa wameyamaliza yote, since that sunday mpaka leo wapo tu hakuna madodoso! Usichangae yakatokea ya Ngoswe na mazoea!
 
Heri yenu mmehesabiwa mimi sijakutana na huyo Karani wa SENSA!,

Na kama aliyekataa kuhesabiwa anashitakiwa je mimi ambaye sitahesabiwa kwa uzembe wa wahusika nichukue hatua gani?.
 
Heri yenu mmehesabiwa mimi sijakutana na huyo Karani wa SENSA!,
Na kama aliyekataa kuhesabiwa anashitakiwa je mimi ambaye sitahesabiwa kwa uzembe wa wahusika nichukue hatua gani?.
Kwasababu kuhesabiwa ni haki yako...inabidi ufungue kesi....lol
 
Phbotocopy!! Mbeya walikuwa wanatumia daftari tu kama la mwanafunzi wa shule ya msingi ambalo karani alijitolea kununua kwa pesa zake binafsi.
 
kati ya sensa zote zilizowahi fanyika hii imesuasua ile mbaya kwa kukosa support ya waislam. Albina upo?
 
Mkuu wenu na speach zake, na mbwembwe nyingi eti bila sensa utakosa vitambulisho vya uraia ooh vikaenda vikarudi mara tumejiandaa vya kutosha tumeshachapisha madodoso.

Mi nawambia takwimu zitakazo toka hapo ni za ki propaganda ya magamba tu, wait and see. Mpaka leo toka sensa ianze mtaani kwetu hata huyo mwenye notebook hajatokea.
 
Sikujua kama tatizo ni kubwa kiasi hiki! sasa cha kupeleka hadi watu mahakamani nini? kama tu waliotayari kuhesabiwa hawajafikiwa!

Ingekuwa Serikali ni kama kocha,mkataba wake ungesitishwa mara moja,hii ni hatari sana,bilions zimetumika halafu dodoso notebook na daftari?we real cant be serious,May God rescue us!
 
masasi mkuu wa wilaya kakiri madodoso kuisha na kufanya zoezi hilo huko masassi kuwa gumu.sasa kweli sensa itasaidia kupanga maendelo kweli kama hata kupata data yenyewe ni shida mwisho wa siku siku zitaisha na watajiondokea zao maana perdiem sizitakuwa zimeshakwisha au wanafanya hv ili watake pesa zingine.hii yaweza kuwa kusudi tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom