Re-Admission form for UDSM

May 16, 2008
74
7
Wakuu nimeiona form nadhani ukiiangalia kwa umakini utagundua hata hawa maprofessor wetu wameshaacha taaluma zao na kukimbilia kwenye siasa.
Hebu kila mtu ajionee mwenyewe utumbo ulioandaliwa na jopo la maprofesa wa Bongo.
 
Attachments

  • FOMU%20YA%20UDAHILI-MAIN%20CAMPUS_2_.pdf
    24.2 KB · Views: 221
Kweli mkubwa huko kwenye ofisi ya mtaa, kata,wilayani na hiyo picha ya mzazi ya nini
 
Hawa jamaa sielewi kama huwa wanafikiria vizuri......! Hilo zoezi la kuizungusha hiyo form ni two expensive hasa kwa wale wanaotoka vijijini cause utakuta umbali kati ya kijiji na makao makuu ya Kata inaweza hata kufikia 200km no reliable transport pia kati ya kijiji na makao makuu ya wilaya like 300km.....no reliable transport! Did they think about that?

Pili, hao viongozi wa mitaa, kijiji, kata .......wametengenezewa ulaji fulani, hapo watataka wapewe fedha ili kuzisaini fomu hizo na huwa ni warasimu sana...so will cause another problem kwa vijana!

Also mimi nadhani migomo chuoni haiwezi kumalizwa kwa mikwara ya aina hii....kinachotakiwa ni kutafuta suluhisho la muda mrefu!
 
Nakumbuka maisha ya Kijijini miaka hiyo mtu unajikwaa badala ya kutafuta dawa unachukua udongo na kuweka kwenye jeraha. Hivi hao walioandaa hiyo fomu hawajui maisha halisi ya Mtanzania wa kawaida yalivyo!. Kipengele cha 'V' kwenye maelekezo na sehemu 'E' vimewekwa kwa ajili ya watu gani. Ina maana wale ambao hawana uwezo wa kujilipia ndiyo mwisho wao wa kuliona darasa?. Kama Watanzania wote wangekuwa na uwezo wa kujilipia kungekuwa na haja ya kuunda Bodi ya Mikopo?, Madai ya wanafunzi wakati walipogoma yameangaliwa japo kupata undani wake? Kwa kuweka masharti ya vitisho Serikali inafikiri ndiyo itamaliza tatizo la migomo kwenye vyuo vya elimu ya juu?. Naamini kwa mtindo huu Serikali inazidi kufisha mfumo wa elimu na kudumaza vipaji vya wataalamu watarjiwa hapa nchini.
 
Mficha maradhi.......! Sijaona umuhimu wa hiyo form wakati migomo ya wanafunzi wa elimu ya juu haina ufumbuzi.
 
Picha ya mzazi ni kituko zaidi, kama amefariki ama umezaliwa na single parent utaweka picha ya nani? UD kuna foreign students kwanini form zipo kiswahili? ama ndo politik kila mahali

Poleni sana....miaka yetu tuliambiwa twende na sahihi za makatibu kata na wakuu wa wilaya....nakumbuka wazee hao walikuwa wanajaza form kwa nyodo kweli ....kwanini mnagoma ilikuwa kazi kuwaelewesha!!!.

Ushi
 
Eti hao hawakugoma
 
Hawa jamaa sielewi kama huwa wanafikiria vizuri......! Hilo zoezi la kuizungusha hiyo form ni two expensive hasa kwa wale wanaotoka vijijini cause utakuta umbali kati ya kijiji na makao makuu ya Kata inaweza hata kufikia 200km no reliable transport pia kati ya kijiji na makao makuu ya wilaya like 300km.....no reliable transport! Did they think about that?

Wapi huku unakotembea kilomita 300 kumkuta mkuu wa mtaa? Kama la, basi acha exaggeration, kilomita 200/300 unaenda wapi? Kwa taarifa tu matakwa ya namna hii katika kujaza form nyingi tu za serikali hufuata hatua hizi. Kutafuta mwenyekiti wa kata si kwa wanafunzi wa chuo tu.

Eti kijijini ni expensive, wewe umeshawahi kuwafikiria wale ambao hawakimbii umande vijijini? Unajua walikuwa na wengine mpaka leo wanatembea kilomita ngapi kwenda shule, tena kila siku? sembuse hii kitu ya season? Acheni maneno, tafuta mwenyekiti wako ajaze fomu hiyo, halafu mrudi darasani !
 
Back
Top Bottom