RC, Mbunge, DC majembe shambani Ludewa, mfano kwa vitendo

Watu tunaojua kilimo hamna kitu hapo.Waswahili wanaita show game kubali kataa ndo ukweli wenyewe
 
Enzi za kumwaga sera majukwani zimeshapitwa na wakati. Tunataka viongozi wanaofanya kazi kwa vitendo, si kutandikiwa mikeka wanapopanda miti kwa ajili ya picha, ila wazame kwenye tope na kuchimba mashimo ya kupanda kahawa. Kiongozi akiingia jikoni avae aplon, na akiwa michezoni vulana za michezo. Tumechoshwa na usanii wa majukwani.

DSCF8091.JPG
DSCF8125.JPG

Picha Kushoto:
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma (kulia) akishirikiana na viongozi na wanachama wa kikundi cha umoja Mawengi kinachojishughulisha na uoteshaji wa miche ya kahawa kupalilia kahawa jana kushoto kwake ni mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe, na mkuu wa wilaya ya Ludewa Geogina Bundala pamoja na wanachama wa kikundi hicho

Picha Kulia:
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kushoto na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma kulia wakitazama shamba la kahawa na mkulima wa kijiji cha Mawengi

DSCF8095.JPG
DSCF8180.JPG

Picha Kushoto:
Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Ishengoma aking'olea nyasi mche wa kahawa,

Picha Kulia:
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Ludewa MOnicha Mchilo ,mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Ishengoma wakitazama mashine ya kukoboa kahawa kata ya Mawengi

Katika picha ya chini kushoto hapo ambapo Mama Ishengoma anangóa nyasi CHUNGUZENI vizuri mkono wa kushoto wa Deo ameshikaje Jembe. Sisi huku kwetu Namtimbwilimbwi hatulimi hivyo. Napita tu lakini!!!!!!!
 
Ingekuwa maigizo wangetandikiwa kanga au mikeka kama baadhi ya viongozi wanavyofanyiwa wanapojifanya wanashiriki upandaji wa miti, huo ndio usanii wa maigizo, lakini hii ya kushika jembe na kuzama topeni huku waking'oa nyasi na kuzikung'uta kwa mikono vigumu kunisakikisha kwamba ni fani ya uigizaji. Bora tu tuungane kuwapongeza, maana hata Nyerere ndivyo alivyokuwa na hulka ya kushiriki maendeleo ya wananchi.

Hawa hawawezi kulinganishwa na Mwalimu Nyerere. Hawa wanaigiza kulima lakini Mwalimu Nyerere alikuwa analima. Nilikaa Butiama kwa miezi miwili wakati wa ujenzi wa nyumba ambayo jeshi lilimzawadia Mwalimu baada ya kustaafu. Nilimshuhudia Mwalimu Nyerere akipalilia shamba la mahindi na mihogo. Akienda asubuhi na kurudi mchana saa 8, na jembe lake begani akiwa amechoka kawa wakulima wa vijijini. Alienda shambani akiwa amevaa gum boots, suruali na shati la kaki, na mara nyingi akiwa ameikunja suruali yake. Hakuongozana na wanahabari wala wapiga picha, na wala hakuwahitaji. Alikuwa akiwapa wakati mgumu sana walinzi wake, kama waendelee kumlinda kwa kumfuata nyuma wakati yeye akilima au nao washike majembe kama yeye! Huwezi kulima ukiwa umevaa koti, huo ni uwongo mkubwa. Hao akina Filikunjombe walikuwa wakihimiza kilimo lakini hawakuwa wakilima. Mwalimu alipokuwa akitoka shambani, hata wakati alipotukarisha kwa chakula nyumbani kwake, sisi kila mmoja alipewa sahani yake, tulikaa mezani lakini yeye na wajukuu zake (wengi si wajukuu katika maana ya watoto wa watoto wake) alikaa kwenye kigoda akila pamoja na watoto wa hapo kijijini kwenye chombo kimoja. Na uliweza kuona wazi kabisa kuwa kila alichokifanya alikuwa anakifanya kama sehemu yake ya maisha siyo kwa maigizo.
 
DSCF8208.JPG
DSCF8204.JPG

Picha Kushoto:
Msafara wa mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma ukiwa umekwama kwa muda mlima wa Kigasi Milo Ludewa huku mvua kubwa ikinyesha jana
Picha Kulia:
Askari polisi wa wilaya ya Ludewa akinyeshewa na mvua wakati akishughulikia njia ya kupita msafara wa mkuu wa mkoa wa Iringa na mbunge wa jimbo la Ludewa ambao walikuwa wakielekea katika ziara ya kikazi zaidi

Asante kwa maelezo mazuri, jambo ambalo linanivutia kwa hawa viongozi hata zile dakika chache walizotumia kushiriki shughuli za kijijini ni jambo ambalo linaleta maana nzuri. Tusiwe na thana ya tafsiri mbaya tu kwa kila lifanywalo, hapa hatuongelei itikadi, bali utendaji wa viongozi hawa.

Kama nilivyosema hapo juu kama ingekuwa kwa ajili ya picha tu huko huko Iringa kuna mashamba mengi tu wangepiga picha na kutangaza kwenye vyombo vya habari. Lakini hapa wamesafiri mbali na kukwama kwenye tope njiani kuelekea Ludewa lakini wengine tunaona yote ni mabaya tu, kwa mwendo huu hatuwezi kujenga nchi ila kukatishana tamaa kwe wenye moyo wa kujituma.

Fransis Godwin ni mwandishi mahiri anayejituma katika kazi yake. Hachagui wapi kwa kwenda hata kuwe na mazingira magumu. Nampa big up, habari hizi tusingeweza kuzipata ni kutokana na kazi kubwa ya mwandishi huyu pamoja na washirika wake katika fani yao ya uandishi. Vyombo vingine vinachuja habari ndio maana hawako tayari kuweka hadharani mambo kama hayo kwa sababu wanazozijua wenyewe.

Kama kuna viongozi wengine wanafanya mazuri kama hawa tungeweka habari zao hapa, ila tatizo vyombo vya habari sehemu zao vimelala, hapo ndio tatizo lilipolala, hakuna sababu ya kurushiana mawe katika hili. Tuondokane na wivu wa kurudishana nyuma ila tujenge wivu wa kimaendeleo ndio kitu damudamu kwa kizazi kipya.

Waigizaji tu hawa, Shambani huendi na suti wala huchomekei, kama wewe si mkulima danganyika!

Huo ndiyo ukweli. Huyo mbunge Deo Filikunjombe ni msanii tu. Hapa Dar watu wengi wanamfahamu na kwa kuthibitisha hilo kumbukeni FILIKUNJOMBE ni mmoja wa wabunge wa CCM ambaye ALIUNGA MKONO tamko la nyongeza ya posho kutoka sh. 70,000 kuwa sh. 200,000 kwa kikao. Huyo anafahamika hapa mjini LABDA AWADANGANYE HAO WANAVIJIJI HUKO LUDEWA ambao HAWAMFAHAMU VIZURI !!!!!
 
Pole sana, tunajadili hapa msafara wa mkuu wa mkoa Iringa, Mbunge wa Ludwa na Mkuu wa wilaya ya Ludwa kushiriki na wanakijiji cha Mawengi katika kuandaa shamba la miche ya kahawa. Sasa mashambulizi yanayoelekwa kwa Filikunjombe yameanzia wapi? Tujadili hoja iliyoletwa na si kumshambulia mtu binafsi hii ni dalili ya kuishiwa hoja.

:msela:Kama mmegundua jinsi watu wanavyozidi kuelekeza mashambulizi yeye ndio anazidi kupangua gear kwa ajili ya gari kushika kasi zaidi.:msela:
 
Kitu kimoja naweza kujifunza katika tukio hili ni kwamba, wamediriki kuondoka maofisini kwao tena kutoka Iringa mjini kwenda porini huko kando ya milima ya Livingstone kuteremkia Ziwa Nyasa. Kama ni kwa ajili ya kupiga picha tu wasingepoteza muda mwingi na kupangua gear kwenye matope wakati Iringa kuna mashamba na wakulima wengi tu ambao wangeweza kwenda kupinga picha hizo kwa gharama nafuu.

Nasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

Nimeanza kuwa na wasiwasi na wewe Candid Scope, unavyojitetea hapa haina shaka wewe ni mmojawao. If my instincts are rights, then you are right kwa kila kitu ulichosema ni sahihi. Binafsi sitaki viongozi wanafiki kama ninyi halafu mnakuja kutafuta sifa hapa JF, kama mlikuwa na nia ya dhati ,mlitakiwa mwondoke ofisini siku nzima muidedicate shambani ....siyo haya maigizo
 
Waigizaji tu hawa, Shambani huendi na suti wala huchomekei, kama wewe si mkulima danganyika!

Habari toka iringa zinasema hiyo ni timu ya wasanii maarufu kama iringa comedians. 2010 mbolea ya ruzuku iliibiwa ludewa dc hana jibu hadi leo. Ishengoma anazurura hatulii. Anachofanya mbunge ni kuunganisha nguvu ya rc na dc dhidi ya Chana. Siasa rahisi
 
Kumbe mbunge tumpongeze kuunganisha nguvu za viongozi kwa kujenga maendeleo ya taifa hayo ndiyo tunayoyataka.
 
Huo ndiyo ukweli. Huyo mbunge Deo Filikunjombe ni msanii tu. Hapa Dar watu wengi wanamfahamu na kwa kuthibitisha hilo kumbukeni FILIKUNJOMBE ni mmoja wa wabunge wa CCM ambaye ALIUNGA MKONO tamko la nyongeza ya posho kutoka sh. 70,000 kuwa sh. 200,000 kwa kikao. Huyo anafahamika hapa mjini LABDA AWADANGANYE HAO WANAVIJIJI HUKO LUDEWA ambao HAWAMFAHAMU VIZURI !!!!!

Msimamo wa Filikunjombe kuhusu posho ameufafanua vizuri tu kama ifuatavyo toka kwenye webpage yake ya face book;

Deo Filikunjombe;Nilipozungumza na gazeti la mwananchi nilisema ninachokiamini. Kwamba ninaamini kuwa hili swala la posho linapashwa kutazamwa kwa upana zaidi.

in a nutshell mie nilisema watumishi wote wa umma wanalipwa mishahara midogo mno isiyokidhi mahitaji muhimu na msingi ya familia. why should we as mps get paid these poshos if we were paid well kukidhi mahitaji ya msingi?

why leo mie kama mbunge nilipwe 200,000/- per day wakati nurse kule kijijini kwangu analipwa 180,000/- kwa mwezi? this is unfair, that's what i said.

na hii ndo ilikuwa hoja yangu. kuwe na usawa. mwalimu alipwe vyema. polisi alipwe vyema. na mganga alipwe vyema. na mwanafunzi asome. kuwe na malipo stahiki.

and in actual fact what i was saying is pay us better salaries and not sitting allowances. why do we get paid to sit? tanzania is the only country in the world whereby people are getting paid to sit.

my concern was, kama kweli, malipo hayo ni halali basi yawe pegged katika mshahara. na ukishafanya hivyo basi haki hiyo itendeke kwa watumishi wote wa umma hasa wale wa kada za chini, na wanafunzi. Na sisi wabunge tutakatwa kodi; kodi hazikatwi kwenye posho.

Wengine wamenipigia simu wakinambia 'brother ungekauka tu' meaning ningekaa kimya. huenda wapo sahihi. lakini ni heri na mie ninayesema ukweli na kuwapigania kuliko wale wanaopinga posho kwa midomo lakini kimya kimya wanazisaini na kuzichukua. huku wanazipinga. na huku wanazichukua.

any way, we need a rational and an accountable govt that respects and takes care of her people; of her workers, of her students and of her wabunge.

nimeona nilitolee ufafanuzi, tu, ili kuliweka vizuri, kwa future reference. Filikunjombe, MP, Ludewa.
 
Ngoja na mie niingie huko nishuhudie alichokisema kuhusu posho, maana hapa mashabulizi si ya kawaida, hata chema kinachofanya na mbunge huyu ni kama hakuna.
 
DSCF8208.JPG
DSCF8204.JPG

Picha Kushoto:
Msafara wa mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christina Ishengoma ukiwa umekwama kwa muda mlima wa Kigasi Milo Ludewa huku mvua kubwa ikinyesha jana
Picha Kulia:
Askari polisi wa wilaya ya Ludewa akinyeshewa na mvua wakati akishughulikia njia ya kupita msafara wa mkuu wa mkoa wa Iringa na mbunge wa jimbo la Ludewa ambao walikuwa wakielekea katika ziara ya kikazi zaidi

Asante kwa maelezo mazuri, jambo ambalo linanivutia kwa hawa viongozi hata zile dakika chache walizotumia kushiriki shughuli za kijijini ni jambo ambalo linaleta maana nzuri. Tusiwe na thana ya tafsiri mbaya tu kwa kila lifanywalo, hapa hatuongelei itikadi, bali utendaji wa viongozi hawa.

Kama nilivyosema hapo juu kama ingekuwa kwa ajili ya picha tu huko huko Iringa kuna mashamba mengi tu wangepiga picha na kutangaza kwenye vyombo vya habari. Lakini hapa wamesafiri mbali na kukwama kwenye tope njiani kuelekea Ludewa lakini wengine tunaona yote ni mabaya tu, kwa mwendo huu hatuwezi kujenga nchi ila kukatishana tamaa kwe wenye moyo wa kujituma.

Fransis Godwin ni mwandishi mahiri anayejituma katika kazi yake. Hachagui wapi kwa kwenda hata kuwe na mazingira magumu. Nampa big up, habari hizi tusingeweza kuzipata ni kutokana na kazi kubwa ya mwandishi huyu pamoja na washirika wake katika fani yao ya uandishi. Vyombo vingine vinachuja habari ndio maana hawako tayari kuweka hadharani mambo kama hayo kwa sababu wanazozijua wenyewe.

Kama kuna viongozi wengine wanafanya mazuri kama hawa tungeweka habari zao hapa, ila tatizo vyombo vya habari sehemu zao vimelala, hapo ndio tatizo lilipolala, hakuna sababu ya kurushiana mawe katika hili. Tuondokane na wivu wa kurudishana nyuma ila tujenge wivu wa kimaendeleo ndio kitu damudamu kwa kizazi kipya.

Nchi haijengwi kwa kuushabikia unafiki wa Viongozi, hilo hata wewe unalijua. Kama nilivyosema huko awali wewe ni mmoja wao na umajitahidi sana kupiga Picha..Hogera Sana!
 
Ni dhana potovu kushabikia kiongozi au mtu, tunachofanya ni kutangaza mazuri yanayofanywa na viongozi. Nadharia na falsafa hii ndiyo msingi wa utume wangu kwa watanzania wenzangu. Wale wenye kuathiriwa na ushabiki ndio wenye kuweka pazia jeusi hata mazuri yaonekane na kutafsiriwa mabaya, tutafikaje kwa mwendo huu?
 
weeee candid scope kila siku unamsifia huyu filikunjombe anakulipa hela ?

Kiwango cha kufikiria hivyo ndio upeo wa wengi wenye hoja ya kukosa utaifa, ila kufanya kwa malipo, hiyo ni palpet stuff ambayo wenye dhamiri safi katika maoni yao watakushangaa kuja na hoja mbovu kama hiyo. Jitahidi kujibu hoja badala ya tuhuma zisizotusaidia kujenga nchi yetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom