RC Mbeya awaonya watumishi wasimseme Mkapa

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
825
Kuna habari kuwa rc wa mbeya amewaita wafanyakazi walioko chini yake akiwaonya wajiepushe kumsema rais wa awamu ya tatu bwana mkapa kwa kuwa watamletea shida,

mama ana mkapa anatuhumiwa kuuziwa kinyemelea nyumba 12 za serikali mkoani hapa, hali wanaoishi kwenye nyumba hizo wakiwa wamezilipia tayari

bwana mkapa anatuhumiwa kujiuzia mgodi wa kiwira mkoani mbeya akiwa na mshirika wake bwana yona.

Inasemekana mkuu wa mkoa alikaripiwa vikali na bwana mkapa, kuhakikisha kuwa mbeya haiwi kimbelembele kwa kumnyima usingizi, bwana mkapa alimwonya bwana mwakipesile walipokuwa kwenye msafara pamoja, kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa rais wa zambia bwana levy mwanawasa, aliyezikwa lusaka zambia, mwezi uliopita,
 
Mwizi ukimwita mwizi anakasirika sana lakini ukimwita shapu anafurahia. MKAPA NI MWIZI NA HAKUNA JINA LINGINE LINALO FANANA NAE.
 
Mara nyingi ukiwaambia watu wasiseme ndio kama umewasha moto kwenye majani makavu. Yesu alipokuwa akiponya watu aliwambia nenda lakini usiseme yeyote aliyekuwa ameponywa hukuweza kujizuia kusema na matokeo yake walisema sana!
 
Kuna habari kuwa rc wa mbeya amewaita wafanyakazi walioko chini yake akiwaonya wajiepushe kumsema rais wa awamu ya tatu bwana mkapa kwa kuwa watamletea shida,

mama ana mkapa anatuhumiwa kuuziwa kinyemelea nyumba 12 za serikali mkoani hapa, hali wanaoishi kwenye nyumba hizo wakiwa wamezilipia tayari

bwana mkapa anatuhumiwa kujiuzia mgodi wa kiwira mkoani mbeya akiwa na mshirika wake bwana yona.

Inasemekana mkuu wa mkoa alikaripiwa vikali na bwana mkapa, kuhakikisha kuwa mbeya haiwi kimbelembele kwa kumnyima usingizi, bwana mkapa alimwonya bwana mwakipesile walipokuwa kwenye msafara pamoja, kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa rais wa zambia bwana levy mwanawasa, aliyezikwa lusaka zambia, mwezi uliopita,

Duh! Jamaa bado ana 'remote control' ya kuhakikisha wakuu ndani ya serikali wawadhibiti wote wanaomsema fisadi vibaya. Fisadi hyu hana haya wala hajui vibaya haoni kasoro yoyote ya ufisadi alioufanya dhidi ya Watanzania. Kichwani mwake ufisadi alioufanya ulikuwa na halali yake!!!
 
huyu RC anamatatizo ya kifundi...JK watendaji wako hawa
 
Inasemekana mkuu wa mkoa alikaripiwa vikali na bwana mkapa, kuhakikisha kuwa mbeya haiwi kimbelembele kwa kumnyima usingizi, bwana mkapa alimwonya bwana mwakipesile walipokuwa kwenye msafara pamoja, kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa rais wa zambia bwana levy mwanawasa, aliyezikwa lusaka zambia, mwezi uliopita,

??????? Hivi ni mara ngapi Mkapa amewahi kusemwa Mbeya mpaka akose usingizi?
 
Uyu RC nae ana technical problem sasa kama kweli kwa nini watu wasimseme.
Tena kwa ilo bit ndo kaaribu,izo news zitazagaa mpaka basi na mkapa anabaki kwenye top ten ya mafisadi Tz na ata historia italitambua ilo.
Uyu mzee bwana au nae kapewa % amfagilie Mkapa,yaani mafisadi wana mikono mirefu ya kunyamazisha watu mpaka unachoka.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom