Sasa angalia wanasiasa wetu! wanamshupalia huyu mama badala ya kuangalia namna wanavyoweza kumwezesha kupata nyenzo za kufanyia kazi ( jiji lina magari mawili, ameomba mawili zaidi wakati anahitaji kumi.)! Au walitegemea atazunguka mwenyewe na kutoa uchafu kwa mikono yake? Wao,, ndiyo wawajibike kwa kutompa mtendaji nyenzo na support ya kumwezesha kufanya kile walichotarajia! Ndiyo yale ya kuwa na mlinzi kavaa kata mbuga na upinde halafu anapokimbia wakija watu wa kazi unamlaumu na kudai kuwa alishirikiana nao! Hatutafika kwa mwendo huu.
Kwa sasa wanahitaji bulldozer kwa haraka mno, na ukirejea kikao chao kilikuwa kinahusu Barabara na sio tatizo la taka katika Jiji hilo changa. Landfill yao haina bulldozer hivyo taka hizo chache zinazokusanywa huishia kurudi tena barabarani.......wataalamu wetu huwa wanakabiliana na wakati mgumu sana kutoka kwa wanasiasa...mara nyingi wanasiasa ni watu wanaoangalia sifa..kuliko ukweli halisi...
nani ambaye hajuwi kwa dunia ya leo na idadi ya watu inakuwa kwa kasi ..jiji lazima liwe na miuondombinu ya kuondoa taka ngumu na maji????
..mitaro...,magari ya maji taka,mabwawa ya maji taka[stabilization ponds or waste treatments ponds,garbage collection vehicles[ratio 1:5,000]-jiji lenye wakaazi milioni linahitaji anglau magari 20-nadhani mkurugenzi ameomba 10 kwa sababu mbeya bado wanamaeneo ya kuchimba mashimo ya taka kwenye ngazi ya familia,...mbeya watahitaji dampo la kisasa [lenye matrekta na bulldozer ya kutosha].....
..,bulldozer lenye uwezo wa kuchimba na ku load weka kama 200m........na pesa za utekelezaji [vifaa vinginevyo ]at least 200million......that is the best you can do ..tena hapo kama watanunua vifaa moja kwa moja kwa wazalishaji[single souce]...
...mwakipesille au mkuu wa mkoa hana ubavu wa kumfuta kazi mkurugenzzi...hawa wote bosi wao mmoja....
..huyu mama kasema kweli ila lugha aliyotumia haikuwa muafaka...ila amewambia ukweli unaouma...kama hakuna resources ni ngumu kufikia malengo..thats not romours...
Hawezi kufanya kazi under limited resources? Hawezi kama mkurugenzi kukaa na kubuni mbinu mbadala za kuhakikisha taka zinazolewa hata kama jiji halina gari hata moja la kuzoa taka? Ina maana huyo mama hajui kuwa kuna mbinu mbadala au kama hajui anataka nani ambunie hizo mbinu na kumpelekea yeye? Hajui kuwa ukurugenzi ni pamoja na kutafuta mbinu mbadala za utatuzi wa tatizo kama una limited resources? Kusema sababu hakuna magari na bajeti ya uzoaji takataka ni excuse ya kutozolewa takataka nadhani kunaonyesha huyu mama uwezo wake wa kufikiri na kupanga mipango ya uzoaji taka under limited resorces hana.
Iko miji haina vitendea kazi vya kuzoa takataka lakini hutumia mitindo mbadala kama ya watu binafsi kuzoa na kulipwa na wale wenye takataka.Ziko njia mbadala kibao ambazo angeitumia kuhakikisha taka zinazozolewa.
Jibu huyo mama alilompa Mwakipesile ingekuwa mimi ndio mkuu wa mkoa ningemtandika kibao huyo mama na mihasira yangu.Jibu alilotoa huyo mama liko chini ya kiwango cha mkurugenzi na msomi.Ni jibu ambalo hata mtu ambaye hakwenda shule hakustahili kulitoa.Mama kama huyu ndio wanaaibisha wasomi waonekane kuwa vituko na watu waone kuwa wasomi ni mbumbumbu wasiokuwa wabunifu kwenye kutafuta ufumbuzi wa matatizo kunapokuwa na constraint ya limited resources.
operesheni sio kazi.... kazi inahitaji mipango. Hii ni hata kwa ukusanyaji wa taka. Wengi wanaiga opereshi za usafi katika Jiji la DSM. Hili ni kosa, tena kosa kubwa sana katika utendaji. Si Munua wala Mwakipesile mwenye kosa hapa. Tatizo ni hao Wadiwani ambao wanawajibu wa kupisha bajeti na ndio watunga sera.
Mkurugenzi wa Jiji anafuata sera za madiwani, na iwapo Waheshimiwa Madiwani wameamua kuwa wachafu - "we can do nothing about that.."
Na huyo Mkuu wa mkoa aibu ya uchafu ipo juu yake vilevile... Mbeya kuna JKT, Mageraza, Polisi na asasi binafsi ambao wanaweza kutoa magari yao kukusanya taka.. aidha makontraka wanaweza kutoa bulldozer kuhakikisha Jaa kuu lipo katika hali nzuri...
Ukirudi kwenye ushirikishwaji wa wananchi katika tatizola taka utaona wazi kuwa kuna uzembe fulani katika watendaji wa idara ya afya...
Hebu wasafiri kidogo hadi Iringa na waone mafanikio yao.. au waende hadi Kilimanjaro na kuangalia juhudi zao katika taka... Mwisho wanaweza hata kutembelea Jiji la Mwanza na kujifunza namna ya kukusanya taka katika kiwango cha upungufu wa vitendea kazi.
Au wanaweza kwenda katika halmashauri ya Mji wa Kinondoni na kusoma namna ya ukusanyaji wa taka kwa kuwashirikisha wananchi.
Iwapo ni tatizo la sehemu ya kutupia taka hizo, ni vema wakawasiliana na Halmashauri ya mji wa Zanzibar, ambao kwa upeo mkubwa wameweza kutatua tatizo kama hilo...
Mantiki ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ni tabia ambayo ipo kwa viongozi wengi ambao kwa namna moja ama nyingine wameshindwa kukubali kuwa kuna tatizo katika suala zima la ukusanyaji na utupaji wa taka katika Miji mingi ya Tanzania. Hiki ni kiburi cha hali ya juu na ulimbukeni wa madaraka.
Iwapo Jiji la Mbeya linasimamiwa na Mkuu wa Mkoa, Meya na Mkurugenzi, huku Waheshimiwa Madiwani wakiwa ndio watunga sera, ilikuwa ni jambo la busara kwa Mkuu huyo wa Mkoa kutuma shitima zake kwa Madiwani badala ya Mkurugenzi wa Jiji...
Kilio cha Madiwani kuajili Mkurugenzi wanamtaka wao kinafaa sana kulinganishwa na tukio hili. Huu ni wakati wa serikali kuu kuona ukweli wa matakwa ya Madiwani kudai kuajili Mkurugenzi wao badala ya kusubiri ateuliwe na Rais...
Nyani wacha utani wako, kwani hii mada imekuja kwa lugha gani?Hivi wewe Kibs lugha inapanda kweli maana sijawahi hata siku moja kusoma bandiko lako lililo ktk lugha ya kiingereza. Dizaini lugha haipandi wewe.....
Nyani wacha utani wako, kwani hii mada imekuja kwa lugha gani?
AhsanteMkuu wa Mkoa hana ubavu wa kumfukuza kazi mteule wa Rais, kumbuka wakurugenzi ni presidential appointee hivyo anayeweza kumfukuza kazi ni Waziri wa TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Rais.
Mnuo kama ninavyomjua mimi ni mtendaji mzuri, ebu watu wa Iringa waseme hapa maana kabla ya kuhamishiwa Mbeya alikuwa Manispaa ya Iringa.
Hapa mwandishi anakuza tu mambo ili kumharibia mtu either mama Mnuo au Mwakipesile. Hizi politics za Tanzania, zisizo angalia ujenzi wa Taifa na kujikita katika mifarakano, fukuza fukuza nk, haziwezi kutusaidia kujenga nchi.
Tatizo letu tunaweka siasa mbele kuliko taaluma.