RC Mbeya amtimua Mkurugenzi

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,949
4,444
na Christopher Nyenyembe, Mbeya
MKUU wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile, katika hali iliyoonyesha kutoridhishwa na utendaji wa kazi wa Mkurugenzi wa jiji hilo, Elizabeth Munuo, amemwamuru aondoke kwenda kutafuta kazi nyingine kama kazi aliyonayo imemshinda.

Mwakipesile alitoa kauli hiyo jana mara baada ya Munuo kulalama katika kikao cha bodi ya barabara kilichokutana mjini hapa kuwa anajuta na kujilaumu kuhamishiwa Jiji la Mbeya, lenye uchafu uliokithiri na lisilo na vitendea kazi.

Munuo alitoa kauli hiyo alipotakiwa na wajumbe kuelezea mikakati ya kukabiliana na tatizo la uchafu katika jiji hilo, ambalo limekithiri kwa uchafu kila kona na kwenye lango kuu la kuingilia eneo la Uyole ambako kuna dampo kubwa la kutupia taka, lakini zinamwagwa taka hadi barabarani.

Huku akisikilizwa kwa makini na wajumbe hao, mkurugenzi huyo badala ya kuelezea mikakati yake, alijikuta akiweka wazi uchungu alionao wa kujutia uamuzi wa serikali wa kumhamishia hapo, huku akidai kuwa mikoa aliyotoka haikuwa hivyo.

“Hapa kwenu Mbeya, nilipokuja nilikuta hakuna wahisani, nasikia waliondoka baada ya kusumbuliwa na matukio ya ujambazi, nilikuta halmashauri ikiwa katika hali hiyo na tumeendelea hivyo hivyo na magari mawili ya kuzolea taka, bajeti ya mwaka huu tumeweka magari mawili ya taka angalau yatusaidie lakini jiji hili linahitaji magari 10,” alisema Munuo.

Munuo alikiri kuwa jiji hilo limekithiri kwa uchafu ambao hauwezi kuondolewa kwa kutumia magari mawili, tena mabovu na kwamba ukosefu wa magari mapya umetokana na tatizo lililowaondoa wahisani.

“Hata mimi mwenyewe najilaumu ilikuwaje nikahamishiwa katika mji huu waliofukuzwa wahisani na nimekuta hali chafu, miji yote niliyokaa ilikuwa na hali nzuri, si Mbeya ndugu mwenyekiti,” alisema mkurugenzi huyo.

Ndipo Mkuu wa mkoa huo, Mwakipesile akionyesha wazi kuchukizwa na kauli ya mkurugenzi huyo ya kuubeza uamuzi wa serikali wa kumhamishia kwenye jiji hilo, aligonga meza na kumpasha kuwa kama ameshindwa kazi aondoke.

“Kama huwezi kazi nenda, go goo, ondoka, katafute kazi sehemu nyingine, Where you think you can do a better job, go, go hatuwezi kufanya kazi kwa kubembelezana, go nenda, takataka zinatupwa hadi barabarani unatuletea utetezi hata mifereji mnashindwa kuzibua, no,” alisema Mwakipesile kwa ukali.

Mbali ya mkuu wa mkoa huyo, kauli hiyo pia iliwafanya wajumbe wengine wa kikao hicho akiwemo Mbunge wa Viti Maalumu, Hilda Ngoye, ambaye alitahadharisha kuwa uchafu wa jiji hilo haupaswi kufumbiwa macho kwani unaweza kuwa chimbuko la matatizo mengi.

Aliyefuatia alikuwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Benson Mpesya, ambaye hakuridhishwa na hoja ya ukosefu wa vifaa vya usafi, isipokuwa alidai kuwa watendaji wa halmashauri hiyo hawajajipanga kukabiliana na tatizo hilo, hivyo kusababisha takataka zizagae kila kona.

Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi, alisema inatia shaka kwa mtendaji wa serikali kudai kuwa kule alikokuwa, kulikuwa kusafi kuliko Jiji la Mbeya alikohamishiwa kwani hali hiyo inaonyesha upungufu wa uwajibikaji.

“Hii ni changamoto kwako mkuu wa mkoa, kwa kuwa watu hawa unaishi nao kila siku na hali ya uchafu unaiona, ulichopaswa ni kutoa maagizo ya jiji liwe safi, unakumbuka Jiji la Dar es Salaam liliwahi kuvunjwa na kuwa mamlaka, sasa hatuoni sababu ya utetezi huu unaotolewa hapa wa kujutia kuhamishiwa Mbeya, ” alisema Zambi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, John Mwankenja, alimuomba, mkuu wa mkoa huo amtake mkurugenzi huyo afute kauli yake, kwa madai kuwa inadhalilisha utendaji mzima wa serikali katika jiji hilo.

Mstahiki Meya wa jiji hilo, Athanas Kapunga, aliingilia kati kwa kukiri upungufu wa kuwapo kwa uchafu katika jiji leo.

Alisema yote yaliyosemwa na wajumbe katika kikao hicho, yatazungumzwa na madiwani wa halmashauri hiyo, huku akielezea wazi kuwa mji huo umekuwa ukiendelea kushuka hadhi tofauti na miaka ya nyuma.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Zelothe Stephen, alilitaka jiji hilo kuhakikisha linaweka taa za barabarani kama urembo, lakini zitakuwa sehemu muhimu ya ulinzi kwa kupunguza vitendo vya uhalifu.

“Mimi sitaki kujikita huko kwenye uchafu, mimi nahamia upande wa taa za barabarani, kwetu sisi taa ni ulinzi mkubwa, zinasaidia kupunguza upigaji wa nondo, hii inatia aibu badala ya Mbeya kuwa jiji, linakuwa zizi,” alisema Kamanda Stephen.


Tanzania Daima
 
"Kama huwezi kazi nenda, go goo, ondoka, katafute kazi sehemu nyingine, Where you think you can do a better job, go, go hatuwezi kufanya kazi kwa kubembelezana, go nenda, takataka zinatupwa hadi barabarani unatuletea utetezi hata mifereji mnashindwa kuzibua, no," alisema Mwakipesile kwa ukali.
Ni hapa alimfukuza Mbeya.
Hatujajua amesha fungasha au lah
 
Ni hapa alimfukuza Mbeya.
Hatujajua amesha fungasha au lah

Kuna kajineno: Kama huwezi kazi.......Angekuwa amemfukuza kasingekuwepo. RC hana uwezo wa kumfukuza kazi Mkurugenzi maana si mwajiri wake. Anachoweza ni kumshitaki kwa wakubwa wake. Vile vile, mtu anafukuzwa kwa barua na si kwa maneno katika mkutano. Kinachofanyika hapa ni posturing ili mtu aonekane mbabe wakati uwezo wa kufanya kweli hana!
 
Mkuu wa Mkoa hana ubavu wa kumfukuza kazi mteule wa Rais, kumbuka wakurugenzi ni presidential appointee hivyo anayeweza kumfukuza kazi ni Waziri wa TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Rais.

Mnuo kama ninavyomjua mimi ni mtendaji mzuri, ebu watu wa Iringa waseme hapa maana kabla ya kuhamishiwa Mbeya alikuwa Manispaa ya Iringa.

Hapa mwandishi anakuza tu mambo ili kumharibia mtu either mama Mnuo au Mwakipesile. Hizi politics za Tanzania, zisizo angalia ujenzi wa Taifa na kujikita katika mifarakano, fukuza fukuza nk, haziwezi kutusaidia kujenga nchi.

Tatizo letu tunaweka siasa mbele kuliko taaluma.
 
...mwakipesille au mkuu wa mkoa hana ubavu wa kumfuta kazi mkurugenzzi...hawa wote bosi wao mmoja....

..huyu mama kasema kweli ila lugha aliyotumia haikuwa muafaka...ila amewambia ukweli unaouma...kama hakuna resources ni ngumu kufikia malengo..thats not romours...
 
“
“Hata mimi mwenyewe najilaumu ilikuwaje nikahamishiwa katika mji huu waliofukuzwa wahisani na nimekuta hali chafu, miji yote niliyokaa ilikuwa na hali nzuri, si Mbeya ndugu mwenyekiti,” alisema mkurugenzi huyo.


Hii nayo kituko itangia kwenye record! Yaani anasema huko alikotoka alikukuta kusafi, nanin alisafisha? Kama mji aliotoka ni Iringa, basi lazima uwe msafi. Ni mji mdogo sana tena ulio stagnant kwa muda mrefu sana.

Mbeya is second fasted growing city in Tanzania after Mwanza. Kwa hiyo watendaji lazima wawe fast as much. Short of that ndiyo kauli kama hizo
 
...ningekuwa mimi ndio mkurugenzi ....ningemjibu hapo hapo mkuu wa mkoa ...lazima viongozi waache kufanya kazi kwa vitisho...mnakumbuka yule mkuu wa wilaya aliyempasha....lowassa...akanywea..

...
 
Sasa angalia wanasiasa wetu! wanamshupalia huyu mama badala ya kuangalia namna wanavyoweza kumwezesha kupata nyenzo za kufanyia kazi ( jiji lina magari mawili, ameomba mawili zaidi wakati anahitaji kumi.)! Au walitegemea atazunguka mwenyewe na kutoa uchafu kwa mikono yake? Wao,, ndiyo wawajibike kwa kutompa mtendaji nyenzo na support ya kumwezesha kufanya kile walichotarajia! Ndiyo yale ya kuwa na mlinzi kavaa kata mbuga na upinde halafu anapokimbia wakija watu wa kazi unamlaumu na kudai kuwa alishirikiana nao! Hatutafika kwa mwendo huu.
 
Hawana maana hawa I thought walikaa kudiscus katizo la umeme Mbeya.
Ni week sasa na siku kadhaa hamna umeme mbeya lafu wandiscus uchafu.
Priotization zero kabsaaaaaaaaaaaaaaaa though uchafu ni agenda muhimu ila umeme currently ni issue.Watu wanakula hasara viwanda ndo usiseme
 
Sawa yote tisa nayakubali lakini diplomasia ya uongozi kwa wote wawili iko wapi?Wakati wa Mwalimu Nyerere Kiongozi alikuwa mtu aliyeandaliwa kuongoza watu katika mambo yote.Hapa nasema kiongozi akishika kurunzi wengine wanafuata!!Sasa hawa tukiwafuata tutafika???Si Mwakipesile Si Munuo wote wanaonyesha hawana diplomasia mbele ya wale wanaowaongoza.Ina maana kabla ya kuja kwenye kikao hawana vikao vyao vya ndani kusemana na kurekebishana kabla ya kuja kutoleana uvivu kwenye kikao chenye waandishi wa habari na watu wengine mashuhuri?JK angalia timu uliyo nayo!!!Hata na pahala fulani wakati wa Waziri Mkuu Lowasa kulizuka vijembe vya hadharani tena nusura Mkurugenzi azikunje na Mkuu wa Wilaya.Haya mambo ya kuumbuana hadharani hayako katika maadili ya viongozi kwani uongozi huandaliwa ,kuchujwa na kufundwa na wala siyo Masters na Ph.Ds.IDM ilikuwa established kwa ajili ya viongozi.
 
Mwakipesile ameshindwa kuongoza mkoa wa Mbeya ndio maana anataka kutumia ubabe kwa huyu mama ambaye sehemu zote alizokaa amefanya kazi nzuri tuu.; Kilosa, Morogoro na hata Iringa. Hawa viongozi wa mkoa wa Mbeya ni wanafiki sana , halmashauri haina vitendea kazi sasa mnafikiri mkurugenzi atafanya nini? Mliwahi kumshauri njia mbadala ya kufanya usafi wa jiji in the absence of vehicles na hakufuata maana huo ndio uongozi;kama kuelezea jinsi atakavyolikabili tatizo amewaambia kuwa yanahitajika magari kumi na katika bajeti hii wameagiza mawili!! Mkuu wa mkoa huyu ni bomu hajui hata kama hawezi kumfukuza kazi mkurugenzi wa jiji; katika uongizi wa nchi wowote makini huyu mpambe wa fisadi Lowassa angekwishafukuzwa kazi siku nyingi sasa muungwana bado analea tu hizi mafia za Lowassa. Kiongozi huonyesha njia, sio ubabe wa kugonga meza huo ni utovu wa nidhamu kwenye kikao chochote kile!!
 
“Hapa kwenu Mbeya, nilipokuja nilikuta hakuna wahisani, nasikia waliondoka baada ya kusumbuliwa na matukio ya ujambazi, nilikuta halmashauri ikiwa katika hali hiyo na tumeendelea hivyo hivyo na magari mawili ya kuzolea taka, bajeti ya mwaka huu tumeweka magari mawili ya taka angalau yatusaidie lakini jiji hili linahitaji magari 10,” alisema Munuo.

Hizi 'tetesi' anazosema 'anazisikia' ndizo zinamfanya anauchamba mkoa wa Mbeya namna hiyo kweli? Je tangu afike ni kitu gani kafanya kubadili hali hiyo yeye kama mkurugenzi wa jiji?
Halafu anasema 'wameendelea hivyo hivyo', kisa?
Business as usual! Huyu ni wa kutimuliwa kabisa.


“Hata mimi mwenyewe najilaumu ilikuwaje nikahamishiwa katika mji huu waliofukuzwa wahisani na nimekuta hali chafu, miji yote niliyokaa ilikuwa na hali nzuri, si Mbeya ndugu mwenyekiti,” alisema mkurugenzi huyo.
[/QOUTE]

ok, sasa kwa nini hakukataa uteuzi wa mheshimiwa raisi?
Na hiyo miji mingine anayodai aliikuta misafi anafikiri haikufanyiwa juhudi kuisafisha? Anataka nani amsafishie jiji?
Ni mzembe huyu!
 
Waliichezea programu ya Miji Endelevu, sasa ndio wakati wa kuvuna walichopanda...
 
...ningekuwa mimi ndio mkurugenzi ....ningemjibu hapo hapo mkuu wa mkoa ...lazima viongozi waache kufanya kazi kwa vitisho...mnakumbuka yule mkuu wa wilaya aliyempasha....lowassa...akanywea..

...
Yule Mkuu wa wilaya ya Nyamagana kweli walijibishana na Lowasa halafu baada ya hapo ikabakia "bifu"kati yake na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza nadhani hadi leo hawaivi ila sema kwa vile wanaume sometimes hawaonyeshi sana vinyongo vyao.

Kuhusu huyo dada wa Mbeya ni kwamba alijikuta ameongea ukweli wake ile over and above maskini. ajirekebishe siku nyingine asitoe utetezi wa kitoto bali achape kazi, kama akiona namna gani vipi basi amuambie mwajiri wake ampangie kazi nyingine
 
How did it come that a Regional Commissioner does not know his responsibility. This is absence and misapplied authority (ultra vires). He should therefore apologize immediately.
 
Hii article inawakilisha kisahihi aina ya viongozi ambao nchi yetu inao.

Kuna mambo mkurugenzi kayasema ambayo yako chini ya wajibu wake, kama kuna tatizo ni failures zake badala ya kulaumu watu wengine.

Hivyo hivyo mkuu wa mkoa, ina maana anakuja kuyasikia hayo maneno kwenye vikao? Hana mikutano ya pamoja na mkurugenzi wa mkoa?

Ni ubabaishaji ule ule ambao tumeuzoea. Kwenye halmashauri za wilaya na mikoa, capacity ni tatizo na bila kutatua hilo, pesa zitaendelea kumwagwa na kupotea.

Inatakiwa mkoa wamshukuru huyo mama kwa kuwaambia ukweli, ni kwa kujua ukweli, mtu unaweza kujisafisha. Vinginevyo ni kupeana masifa ambayo hayana maana kabisa.

Hivi nafasi za ukuu wa mkoa zinaombwa wapi na wengine tupeleke maombi? kwi kwi kwi!!!!
 
Mkuu wa Mkoa hana ubavu wa kumfukuza kazi mteule wa Rais, kumbuka wakurugenzi ni presidential appointee hivyo anayeweza kumfukuza kazi ni Waziri wa TAMISEMI baada ya kupata kibali cha Rais.

Mnuo kama ninavyomjua mimi ni mtendaji mzuri, ebu watu wa Iringa waseme hapa maana kabla ya kuhamishiwa Mbeya alikuwa Manispaa ya Iringa.

Hapa mwandishi anakuza tu mambo ili kumharibia mtu either mama Mnuo au Mwakipesile. Hizi politics za Tanzania, zisizo angalia ujenzi wa Taifa na kujikita katika mifarakano, fukuza fukuza nk, haziwezi kutusaidia kujenga nchi.

Tatizo letu tunaweka siasa mbele kuliko taaluma.



Kwa nini basi Raisi huwa hamsimamishi mbele ya hadhara mkurugenzi kwenye zile geresha zake kwenye mikutano yake mikoani?
Waziri mkuu naye anawagonganisha wananchi na mabwana shamba tu, kwanini si mkurugenzi?


Afadhali Reginald Mengi anatafuta umaarufu kwa kupiga vita ufisadi. Baada ya serikali kuendelea kuzembea, issue ya maalbino ni vyombo vya habari vinalivalia njuga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom