Invarbrass
JF-Expert Member
- Feb 25, 2011
- 504
- 111
Hivi what are we? unajua mpaka sasa inafika wakati tunakuwa kama wendawazimu. Kwanini tunapenda kurudi zama za giza? Kweli sasa nimeamini wadau wa elimu wamekuwa wakiimba kuwa elimu inashuka sasa ndo tunaaanza kuona matokeo halisi ya tahadhari ya wadau wa elimu. Imekuwa ikisemwa kwamba hali ya elimu ni mbaya kuanzia shule ya msingi mpaka vyuoni, kuwa kiwango cha elimu kinashuka na taifa linaelekea ujingani sasa naamini ndo linaanza kufika ujingani. Eti serikali itoe pesa za tambiko la jiwe? siamin! Na inaweza kutoa si tunaona inochofanya na inachopanga kufanya loliondo. Nchi zenye elimu zao zina fadhiri utafiti sisi tunahamasishana kufadhiri miujiza. Hiyo miujiza mbona isije na pesa? Na watu wameshaweka akili zao kimiujiza miujiza wakisikia tu dalili ya muujiza hao..Na mtaibiwa sans mwaka huu Wahenga walisema Kazi ya mjinga ni kuumia na wale wasomaji wa bible nadhani kuna mstari (si mjuzi wa bible lakin) kuwa, "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" NIHATARI KUKOSA ELIMU KATIKA DUNIA YA LEO INAYOENDESHWA KWA ELIMU.