RC Arusha ampongeza jaji aliemvua ubunge Godbless Lema...

Namuonea huruma sana huyu jamaa sijui mnamuita RC au ni Remote Control? Hajajua anaongoza watu wa aina gani? Tunaelewa ni kwanini yuko A town ila hayo maslahi aliyo tumwa kuyalinda A town yatafichuka tu! Aelewe pia hana wadhifa wowte CDM na hutuhitaji ushauri wake. Kwani hata kabla hajaongelea rufaa tayari watu makini walishakata rufaaam na ataona aibu sana siku ikifika.
 
Anampongeza jaji au Sheria iliotumika?Lema akishinda Rufaa, atampongeza akim huyo au atapongeza jopo la majaji wa rufaa?
Magesa aliwahi kua kiongozi wa bweni huko mara......kumbukumbu zake zinaonyesha yuko kimaslai zaidi pale alipokua shushushu wa walimu kuliko haki za wanafunzi wenzake
 
hata kama akimpongeza ajue siku inakuja atapo tafuta pa kujificha lakini asipate na ataomba mhamaha haitawezekana ajiandae kwenda jela maana ndio wanaohalibu nchi yetu
 
Mungi.

Jaji Rwakibiria alimtia Lema, hatiani kwa kosa la 'Illegal Campaign' kwa kutoa kauli za kumbagua kijinsia Dr Burian.

Kwa mujibu wa sheria za uchaguzi makosa yote yaliyokuwa yanamkabili Lema, makosa mawili yanaangukia kwenye kifungu cha 108, kifungu kidogo cha pili aya 'A' ambayo huruhusu aliyevuliwa ubunge kukombea kwenye uchaguzi mdogo.

Kifungu cha 114 cha sheria ya uchaguzi kinazungumzia 'Illegal' kwa hiyo Jaji alitoa hukumu sahihi.

Thinking in the Pandora box that has a total darkness. I am very sorry.
 
Anaanza kujikomba kwa magamba kwani amekaribia kustaafu? Maana ndo hao wanataka baada ya kustaafu waje angalao wapewe ukuu wa wilaya/mkoa na sitoshangaa chadema wakichua dola akahamia kuwa upande wao. Hivi nae kasahau kazi yake kaingia kwenye siasa ama police nao ni wanasia?

Magesa ni kijana sana. Hawezi kuwa wa kustaafu karibuni hivi.
Alipata cheo cha kisiasa kwa kujikomba na aliendelea kujikomba hivi hivi hadi kufikia ngazi aliyopo. Na bila shaka anategemea ataendelea kufanikiwa kwa kujikomba. Amekosea. Waliofanya hivi zamani wako hoi kisiasa na kimaisha. Hawakubaliki wala kukumbukwa kwa lolote!
 
Kwa kauli hiyo ya Mulongo, sasa nimekubaliana na maneno ya Lema kwamba ile hukumu ilichongwana na ikulu (JK) ili kuleta "amani Arusha".
 
Ukimwona mkuu wa mkoa anafurahia kuvuliwa madaraka kwa kiongozi aliyechaguliwa na wananchi wengi wa eneo husika ujue ana tatizo kubwa up stairs. Nani amefaidi nini kwani hata CCM wakirudia uchaguzi bado watabwagwa na wakirudia tena na tena bado watapigwa chini na kuzidisha hasira za wapiga kura. Furaha yake inge make sense kama jimbo lingerudi CCM lakini anachompongezea jaji siku si nyingi atajiona b.wege
 
Yuko makini, anajua maisha yake Arusha yako delicate kama - cable za ICU ROOM.
 
Back
Top Bottom