RC ARUSHA agoma kusitisha huduma ya Loliondo

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
RC ARUSHA agoma kusitisha huduma ya Loliondo, asema
- hajapata barua yoyote kutoka wizarani
- kwa hali ya sasa na wingi wa watu ni vigumu kusitisha huduma hiyo

SOURCE : mwananchi


update: serikali ya kanusha rasmi kusitisha huduma ya loliondo. Ya sema imeunda kamati kuchunguza namna ya kuboresha huduma -source radione 8pm news


UPDATE
http://www.mwananchi.co.tz/componen...c-ni-vigumu-kuzuia-tiba-ya-loliondo-sasa.html

WAKATI Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda akieleza kuwa ameagiza Serikali ya Mkoa wa Arusha kuzuia tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Mwasapile, Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Raymond Mushi amesema ni vigumu kusitisha huduma hiyo.Mushi alisema pamoja na kutopata barua yoyote inayomwagiza asimamishe huduma za mchungaji huyo, ni vigumu katika mazingira yaliyopo katika Kijiji cha Samunge, Loliondo kufanya hivyo ikizingatiwa kwamba hivi sasa kuna maelfu ya watu hasa wagonjwa walioko hapo na wengine wakiendelea kumiminika.

“Hata mimi nimemsikia Waziri Dk Mponda, lakini siwezi kuanza kufanya kazi bila kupokea barua na maelekezo. Lakini hili jambo ni gumu kidogo kwani watu bado wanakwenda na tukipata barua tutajua jinsi ya kukabiliana na hali hii,” alisema Mushi.

Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa alisema kama akipokea barua na maelekezo watakaa na watendaji wengine kuona ni jinsi gani wataweza kukabiliana na hali ya Loliondo. “Pale yule mchungaji anasema anatoa huduma ya tiba na lile jambo ni la kiimani ndiyo sababu anasema wenye imani watapona sasa sidhani kama wataalamu wakipeleka dawa ile maabara wataona kitu,” alisema Mushi.

Mbali ya Kaimu Mkuu wa Mkoa kuonyesha wasiwasi wake juu ya utekelezaji wa agizo hilo la Waziri, Mbunge wa Ngorongoro (CCM), Saning’o ole Telele amepinga hatua hiyo ya serikali kutaka kuzuia kwa muda tiba hiyo akisema badala yake, inapaswa kusaidia watu kupata tiba.“Sikubaliani na Waziri wa Afya kuzuia tiba eti sijui mchungaji ajisajili kwanza.Tunachoomba ni serikali kusaidia watu wafike Ngorongoro, Samunge na kupata tiba katika mazingira bora,” alisema Telele.

Telele alisema watu wengi wamepona kwa kunywa dawa hiyo, hivyo Serikali inapaswa kuomba msaada wa mashirika mbalimbali kama Msalaba Mwekundu yafike kuweka mahema na kutoa huduma ya kwanza.Jana, Dk Mponda alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha, kuzuia mara moja matibabu ya magonjwa sugu yanayoendeshwa na Mchungaji Mwasapile hadi serikali itakapojiridhisha ubora na usalama wake kwa watumiaji.

Akizungumzia tamko hilo la Waziri, Msaidizi wa Mchungaji Mwasapile, Paulo Dudui alisema amepotoshwa kwa vitu vingi: "Kwanza siyo kweli kuwa wagonjwa wote wanatumia kikombe kimoja na pia si kweli kwamba wanatumia maji ya mto."

"Kila mgonjwa anatumia kikombe chake na tuna vikombe zaidi ya 100 ambavyo baada ya kutumika vinaoshwa na wagonjwa wanaona na pale kuna maji ya bomba yanayotoka katika chanzo cha maji cha Samunge.”Lakini Dudui alisema kama wakipokea maelekezo ya serikali kuhusu tiba watakaa na kujadiliana kwani wanaamini huduma ambayo wanatoa ina manufaa makubwa kwa watu na siyo uganga.

“Mchungaji mwenyewe atasema nini cha kufanya ila Waziri kapotoshwa. Hapa serikali ilitakiwa kusaidia huduma kutolewa na siyo kuzuia,” alisema Dudui.Katika hatua nyingine Dudui alisema kwamba mtoto mmoja alifariki dunia jana katika eneo hilo kutokana na kuchelewa kupata tiba.
 
Ujamalizia amesema
atakachofanya ni kuweka utaratibu waliopo wamalize ama kupungua na magari yatakuwa yakisubiria mto wa mosquito..ili kutoleta msongamano wa watu
 
Viongozi wa mkoa wa Arusha wametumia busara na ninawapongeza kwa kutokurupuka na kuzuia utoaji wa dawa hiyo. Ni muhimu kuweka utaratibu wa kuingia na kutoka kwa babu maanake punde si punde nchi nzima itahamia pale, wagonjw ni wengi waliokata tamaa.

Naibu waziri wa afya kama kawaida ya viongozi wetu wa kitaifa aliropoka tu bila hata kupata data. Amwache babu afanye kazi yake kuokoa maisha ya watu.
 
Naibu waziri kachelewa kwenda kupata dawa hivyo anataka naye akaipate maana kila akipiga hesabu za msururu wa watu hapati picha atafikaje.
 
nampongeza RC wa Arusha. Kama tulivyoikia mbona na wakuu wa nchi walienda kunywa? kwa nini na wngine wasiende? Ni afadhali wote wenye shida waende kutibiwa.
 
Naibu waziri kachelewa kwenda kupata dawa hivyo anataka naye akaipate maana kila akipiga hesabu za msururu wa watu hapati picha atafikaje.

Ha ha haaa! Hapa umenikumbusha Nicodemo aliyekuwa anazuia watu kwenda kwa Yesu lakini yeye mwenyewe akatinga usiku. Hata mimi nahisi waziri anafanya mpango wa kupunguza watu ili wao (Viongozi) waruke kwa helcopta za polisi na Jeshi wakapate dawa.
 
Ushauri wa bure kwa wilaya ya Loliondo. Kutokana na habari za babu kutangazwa kwenye vyombo vya habari, magazeti, TV nk; nadhani kuzuia watu kwenda Loliondo siyo rahisi. Cha maana Loliondo waamue kujipanga, waimarishe huduma muhimu hapo kwa babu kama vile vyoo, waanzishe migahawa, na waweke ma-tent kwa ajili ya watu kupumzika; kisha wote wanaokwenda kumwona babu wawe wanachangia kidogo uendeshaji wa huduma hasa usafi wa mazingira; lakini wakati huohuo wote wanaokuja huko watahakikishiwa kupata huduma inayokubalika ya chakula na mahali decent pa kupumzika. na wale wanaotoka nje ya nchi nao wachangie kiasi in foreign currency. Naamini hii pia ni njia ya kukuza utalii kwa sababu utalii siyo kwenda kuona nyumbu Serengeti pekee, lakini hata kwenye hiyo tiba inaweza jumuishwa kama utalii kwa njia ya matibabu ya asili. :lol:
 
Ushauri wa bure kwa wilaya ya Loliondo. Kutokana na habari za babu kutangazwa kwenye vyombo vya habari, magazeti, TV nk; nadhani kuzuia watu kwenda Loliondo siyo rahisi. Cha maana Loliondo waamue kujipanga, waimarishe huduma muhimu hapo kwa babu kama vile vyoo, waanzishe migahawa, na waweke ma-tent kwa ajili ya watu kupumzika; kisha wote wanaokwenda kumwona babu wawe wanachangia kidogo uendeshaji wa huduma hasa usafi wa mazingira; lakini wakati huohuo wote wanaokuja huko watahakikishiwa kupata huduma inayokubalika ya chakula na mahali decent pa kupumzika. na wale wanaotoka nje ya nchi nao wachangie kiasi in foreign currency. Naamini hii pia ni njia ya kukuza utalii kwa sababu utalii siyo kwenda kuona nyumbu Serengeti pekee, lakini hata kwenye hiyo tiba inaweza jumuishwa kama utalii kwa njia ya matibabu ya asili. :lol:

Unenalo ndilo muhimu haswaa
 
Mganga akiwa Mkristo ni Mchungaji akiwa Muislam ni Sheik, hii hatari sana hili swala la kunywesha watu dawa haliwezi kuwa swala la Imani hata kidogo inaonekana elimu ya Imani haitolewei vizuri Makanisani na Misikitini.

Kama hamtaki serikali ifanye kazi yake tutajuaje kama hiyo dawa inafanya kazi?? afadhali Mkuu anatumia Dawa za Marekani na Cuba naona zinampa nafuu, tutapata vipi takwimu ya watu walioponyeshwa na hiyo dawa.

Na je Mtu akijitokeza akasema ameoteshwa na Mungu kuwa anyweshe watu sumu wafe mtasema hilo ni swala la kiimani serikali hisiingile! au safari hiyo mtaguna nakuitaka Serikali imkamate huyu mtu?!
 
Ninamuomba mungu awashushie dhahama kubwa, aanze na waziri wa afya, kwa wale wote wanaojaribu kuingilia kazi za kiroho.ya mungu apewe mungu na kaisari apewe yaliyoyake.waziri wa afya anapaswa kwanza ashughulikie mamia ya vituo feki vya afya vilivyozagaa nchi nzima ambavyo vimekuwa vikitoa huduma duni na kufabya utoaji mimba kihorera kwa dada zetu.kumzuia mchungaji aache kutoa huduma hiyo kwa wahitaji na sawa kutaka wagonjwa hao waendelee kuteseka na hapo hapo ni kuingilia kazi za kiroho.
 
update: serikali ya kanusha rasmi kusitisha huduma ya loliondo. Ya sema imeunda kamati kuchunguza namna ya kuboresha huduma -source radione 8pm news
 
Back
Top Bottom